KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, June 11, 2016

IBADA YA MAZISHI YA MUHAMMAD ALI YAJAWA NA MIHEMKO

RAIS wa zamani wa Marekani, Bill Clinton akizungumza wakati wa ibada hiyo
BAADHI ya mbondia wa zamani wa ngumi za kulipwa wakiwa na mwanamuziki Willy Smith wakati wa ibada hiyo
MKE wa Muhammad Ali, Ronnie wakati wa ibada hiyo
UMATI wa watu ukiwa umefurika wakati wa ibada hiyo
MSAFARA wa gari lililobeba jeneza la Ali

Ibada ya ukumbusho iliojawa na mihemko ya aina yake kwa bondia Mohammed Ali imefanyika katika mji alikozaliwa wa Louisville, Kentucky.

Umati watu 14000 ulisikiliza kwa makini watu wa tabaka na dini tofauti wakimuomboleza mohammed ali kutokana na umahiri wake katika ulingo wa michezo na pia alivyoitunza jamii, huku wakisifu mchango wake katika kuimarisha amani duniani na haki za binadam.

Mkewe Ali, Lonnie Ali, anasema mumewe alikabiliwa na masaibu si haba, bila kuonyesha hasira, na kuwataka watu kufuata mfano wake.

Katika taarifa, rais wa Marekani Barrack Obama, alimtaja Ali kama mtu shupavu, aliyeng'aa na aliyekuwa na ushawishi mkubwa kuliko mtu yeyote wa kizazi chake.

Rais wa zamani Bill Clinton, alikumbuka utanashati, ucheshi na utu aliooonyesha marehemu Ali, wakati akikabiliana na machungu ya ugonjwa uliomdhoofisha.

No comments:

Post a Comment