KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, June 7, 2016

DIAMOND AKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 600 KWA WANAFUNZI WA DAR

MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul 'Diamond', amekabidhi msaada wa madawati 600 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Madawati hayo yatatolewa kwa shule za mkoa wa Dar es Salaam, ambapo Diamond alimtaka Makonda asiwasahau wanafunzi wanaosoma maeneo ya Tandale. Diamond alisema ameamua kutoa msaada huo kwa lengo la kuwakumbuka watanzania wenzake, kutokana na ukweli kwamba wamekuwa wakimuunga mkono kimuziki. Amesema lengo lake ni kusaidia madawati katika mikoa mbalimbali nchini na kwamba ameanzia na mkoa wa Dar es Salaam kwa sababu ndiko anakoishi.



No comments:

Post a Comment