KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, June 29, 2016

YANGA YACHEZEA KICHAPO KWA TP MAZEMBE


LICHA ya kuwaruhusu mashabiki wake kuingia uwanjani bure, Yanga jana ilishindwa kutamba mbele ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0.

Katika mechi hiyo ya hatua ya makundi ya ligi ya Kombe la Shirikisho, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, TP Mazembe ilipata bao hilo la pekee na la ushindi kipindi cha pili.

Mshambuliaji Marvelle Bope ndiye aliyewafanya maelfu ya mashabiki wa Yanga waliofurika kwenye uwanja huo watoke vichwa chini baada ya kuifungia bao hilo la pekee dakika ya 75.

Ushindi huo ni wa pili kwa TP Mazembe, ambayo katika mechi yake ya kwanza, iliilaza Adeama ya Ghana bao 1-0 mjini Accra.

Kwa upande wa Yanga, kipigo hicho ni cha pili baada ya kupoteza mechi yake ya awali dhidi ya MO Bejaia kwa kichapo cha bao 1-0.

Yanga iliuanza mchezo huo kwa kasi na kutawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza, lakini ilishindwa kuzitumie vyema nafasi ilizopata kufunga mabao.

No comments:

Post a Comment