KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, June 7, 2016

MAISHA YA MAREHEMU MUHAMMAD ALI PICHANI

Muhammad Ali, ambaye alifariki dunia Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 74, pia alikuwa akijulikana kwa jina la The Greatest, kutokana na umahiri wake katika masumbwi ya kulipwa.
Ali, wakati huo akijulikana kwa jina la Cassius Claty, akiwa na umri wa miaka minne (kulia) akiwa na kaka yake, Rahman, wakati huo akiwa na umri wa miaka miwili (kushoto).
Ali akiwa na mkewe wa kwanza, Sonji Roi mwaka 1964, kabla ya kutengana.

Cassius Clay akiwa ameungukwa na mashabiki wake mwaka 1963 baada ya kushinda medali ya dhahabu ya Olimpiki.
Ali akiwa na mkewe wa pili, Belinda Boyd. Hapa wakiwa na watoto wao wawili mapacha, Jamillah na Rasheda mwaka 1974.
Ali akiwa na mkewe wa tatu, Veronica Porsche mwaka 1977. Aliishi naye kwa miaka minane kabla ya kutengana.
Muhammad Ali akiwa na mkewe wa nne, Lonnier mwaka 1999. Aliishi na mkewe huyo hadi mauti yalipomkuta.
Ali akipokewa na kundi la mashabiki alipowasili mjini London kwa ajili ya pambano la marudiano dhidi ya Henry Cooper, mwaka 1966.
Ali akizungumza jambo na Malkia wa Uingereza, alipotembelea Marekani mwaka 1976.
Ali akiwa na wanamuziki wa kundi la The Beatles mjini Miami baada ya kundi hilo kufanya onyesho. Wanamuziki hao walijawa na furaha kubwa baada ya kukutana na bondia huyo.
Ali alisababisha msongamano mkubwa wa watu kila alipokwenda. Hapa akipiga picha akiwa amevaa kofia ya polisi mwaka 1980.
Wazimu wa pesa. Hapa Ali akiwaamekaa juu ya kitita cha fedha alizozawadiwa kwa kushinda pambano lake la kwanza la ngumi za kuliwa

Ali akiwa nchini Uingereza mwaka 1977, alikokwenda kuhudhuria uzinduzi wa filamu inayoelezea maisha yake, akiwa na bintiye Hana, anayekunywa maziwa wakati mkewe Ronnie akiwa amekwenda kufanya manunuzi.

No comments:

Post a Comment