Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imeondoka saa 9.45 alfajiri ya leo Juni 30, 2016 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia kwenda Visiwa va Hame-Shelisheli kwa ajili ya kuwavaa wenyeji katika mchezo wa marudiano kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana.
Serengeti Boys inaondoka na matumaini makubwa ya kuiondoa Shelisheli katika mbio hizo baada ya kuvuna ushindi mnono wa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Jumapili ya Juni 26, 2016. Ili ifuzu, Serengeti Boys inahitaji kusimama imara katika matokeo hayo ama kwa kupata sare ya aina yoyote, kushinda au ikitokea kupoteza, basi isifungwe zaidi ya mabao 2-0.
Lakini Kocha Mkuu wa vijana hao, Bakari Shime maarufu kama Mchawi Mweusi kutoka Tanga, amesema, “Nawaheshimu Shelisheli, lakini vijana wangu hawawezi kuwapa nafasi hata kidogo wapinzani wetu. Hapa tulishinda, na kwako tunakokwenda tunakwenda kushinda. Vijana wangu wa Serengeti Boys wako vizuri. Nawapenda na wao wanatupenda makocha wao na viongozi wote wa TFF.”
Katika mchezo wa Dar es Salaam waliozifumania nyavu walikuwa Nickson Kibabage, Ibrahim Abdallah na Ally Hussein ambaye alifunga ambao kila mmoja amepania kufunga kama kocha akiwapa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza kwa sababu Mchawi Mweusi amefunga safari hiyo akiwa na kikosi cha nyota 20 wa timu hiyo inayolelewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Rais Jamal Malinzi.
Nyota waliosafiri ni pamoja na makipa, Ramadhani Awm Kabwili na Samwel Edward Brazio wakati mabeki wako Kibwana Ally Shomari, Nickson Clement Kibabage, Israel Patrick Mwenda, Dickson Nickson Job, Ally Hussein Msengi, Issa Abdi Makamba.
Viungo ni Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamisi Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali, Syprian Benedictor Mtesigwa, Ibrahim Abdallah Ali, Yassin Muhidini Mohamed, Shaban Zuberi Ada huku washambuliaji wakiwa ni Rashid Mohammed Chambo, Mohammed Abdallah Rashid, Yohana Oscar Mkomola, Muhsin Malima Makame na Enrick Vitalis Nkosi.
Serengeti Boys ambayo haina mdhamini badala yake ikihudumiwa na TFF yenyewe ilikuwa kambini tangu Juni 14, 2016 kujiandaa na mechi hizo za kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Shelisheli na Afrika Kusini ambayo itapambana nayo baadaye mwezi ujao.
Katika kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki. Ilishika nafasi ya tutu nyuma ya Korea Kusini na Marekani.
'
Thursday, June 30, 2016
KOCHA TWIGA STARS ATANGAZA KIKOSI KITAKACHOMENYANA NA RWANDA
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake Tanzania, Nasra Juma ametangaza majina ya wachezaji 23 watakaounda kikosi cha Twiga Stars.
Kikosi hicho kinatarajiwa kwenda Kigali, Rwanda Julai 15, 2016 kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda ikiwa ni mwaliko maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Rwanda (Ferwafa).
Wakati Ferwafa likiingiza mchezo huo wa Julai 17, 2016 kwenye orodha ya michezo inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira na Miguu la Kimataifa (Fifa), lakini Mheshimiwa Rais wa Rwanda Paul Kagame kuwa sehemu ya burudani ya burudani mbele ya wageni wake ambao ni wakuu mbalimbali wanaounda Umoja wa Nchi za Afrika (AU) ambao watakuwa na mkutano wao nchini Rwanda.
Mbali ya soka kama burudani, pia Rais Kagame atatumia mchezo huo kama hamasa kwa wakuu wa nchi ili kutoa kipaumbele kwenye soka la wanawake ambako kwa sasa ni ajira ambayo inakwenda sambamba na kuitikia wito wa kupambana na changamoto za malengo ya millennia (MCC) ambayo pia yanataka wanawake wapate nafasi.
Makipa:
Fatma Omary
Belina Julius
Najiat Abbas
Walinzi:
Stumai Abdallah
Fatma Issa
Anastazia Antony
Happuness Henziron
Maimuna Khamis
Viungo:
Donisia Daniel
Amina Ali
Amina Ramadhani
Fatuma Bashiri
Wema Richard
Fadhila Hamadi
Mwajuma Abdallah
Anna Hebron
Sophia Mwasikili
Washambuaji:
Tumaini Michael
Johari Shaaban
Fatma Idd
Shelder Bonifdace Mafuru
Asha Saada Rashid
Mwanakhamisi Omar
Wednesday, June 29, 2016
YANGA YACHEZEA KICHAPO KWA TP MAZEMBE
LICHA ya kuwaruhusu mashabiki wake kuingia uwanjani bure, Yanga jana ilishindwa kutamba mbele ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0.
Katika mechi hiyo ya hatua ya makundi ya ligi ya Kombe la Shirikisho, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, TP Mazembe ilipata bao hilo la pekee na la ushindi kipindi cha pili.
Mshambuliaji Marvelle Bope ndiye aliyewafanya maelfu ya mashabiki wa Yanga waliofurika kwenye uwanja huo watoke vichwa chini baada ya kuifungia bao hilo la pekee dakika ya 75.
Ushindi huo ni wa pili kwa TP Mazembe, ambayo katika mechi yake ya kwanza, iliilaza Adeama ya Ghana bao 1-0 mjini Accra.
Kwa upande wa Yanga, kipigo hicho ni cha pili baada ya kupoteza mechi yake ya awali dhidi ya MO Bejaia kwa kichapo cha bao 1-0.
Yanga iliuanza mchezo huo kwa kasi na kutawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza, lakini ilishindwa kuzitumie vyema nafasi ilizopata kufunga mabao.
Monday, June 27, 2016
SERENGETI BOYS YAIPIGA SHELISHELI MABAO 3-0
TIMU ya soka ya Taifa ya vijana wa chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys jana ilijiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kucheza fainali za Afrika baada ya kuichapa Shelisheli mabao 3-0.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Serengeti Boys ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0.
Kwa ushindi huo, Serengeti Boys sasa inahitaji sare ya aina yoyote katika mchezo wa marudiano utakaochezwa wiki mbili zijazo nchini Shelisheli.
MASHABIKI KUZISHUHUDIA YANGA NA MAZEMBE KESHO BILA KIINGILIO, KAMISAA ATAKA WATAZAMAJI 40,000 PEKEE
YANGA SC imefuta viingilio katika mchezo wa Jumanne wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DRC na sasa mashabiki wataingia bure.
Taarifa ya Yanga SC jioni hii imesema lengo la kufuta viingilio ni kuvutia mashabiki wengi zaidi uwanjani wajitokeze kuishangilia timu ya nyumbani dhidi ya timu kutoka DRC.
Awali, Yanga ilitaja viingilio viwili tu katika mchezo huo ambavyo ni Sh. 7000 kwa majukwaa ya mzunguko na Sh. 30,000 kwa VIP na tiketi ilikuwa zianza kuuzwa kesho.
Huo utakuwa mchezo wa pili wa Kundi A kwa Yanga, baada ya Jumapili kufungwa 1-0 na wenyeji Mouloudia Olympique Bejaia Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia Jumapili.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limechanganya marefa watatu kutoka nchi tatu tofauti kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.
Hao ni Janny Sikazwe wa Zambia atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Jerson Emiliano Dos Santos wa Angola na Berhe O'michael wa Eritrea.
Wakati huo huo, wanachama wa klabu ya Simba wameahidi kuiunga mkono Yanga katika mechi yao ya kesho dhidi ya TP Mazembe.
Wakizungumza jana mbele ya Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Murro, wanachama hao walisema wamefikia uamuzi huo ili kuonyesha uzalendo kwa taifa lao.
TFF YATOA TAHADHARI KWA YANGA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea taarifa juu ya mpango na kauli za baadhi ya viongozi wa Young Africans SC kushawishi mashabiki wao kufanya vurugu dhidi ya warushaji matangazo ya televisheni ya moja kwa moja wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho la Afrika ngazi ya Makundi kati ya Young Africans ya Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) utakaofanyika Juni 28, 2016 saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Dar es Salaam.
TFF ikiwa msimamizi mkuu wa mpira wa miguu Tanzania, inawajibika na mara moja inachukua nafasi hii kuwatahadharisha baadhi ya viongozi wa Young Africans, wanachama na mashabiki wao kutofanya hivyo kwani itakuwa ni kinyume na kanuni za mashindano na mikataba ya udhamini katika hatua hii.
Ikumbukwe kwamba CAF inamiliki asilimia mia moja ya haki za habari na masoko katika ngazi hii ya makundi na jaribio lolote la kukwamisha matangazo ya biashara au utengenezaji na urushaji wa matangazo ya televisheni au ukwamishaji wa shughuli zingine kama hizo kwa CAF au wakala aliyeteuliwa na CAF kutaigharimu klabu mwenyeji si kwa kutozwa faini tu lakini pia uwezekano wa kuondolewa mashindanoni.
Pia TFF inatoa tahadhari hiyo ikiwamo ile ya utamaduni wa kukaa uwanjani ili kuepusha aina yoyote ya vurugu kwenye michezo yake hususani hii ya hatua ya makundi. TFF inafahamu kuwa tayari viongozi wa Young Africans walikwisha kusoma nyaraka na taarifa mbalimbali kuhusu kanuni na masuala ya udhamini kwa timu zinazofuzu hatua ya Nane Bora.Wapenzi wa Yanga wanaombwa kufika kwa wingi na kuishangilia kwa nguvu timu yao ikiwa ni njia ya kuitia hamasa.Hata hivyo shamrashamra hizo zifanyike kwa kufuata sheria,kanuni na taratibu za Mpira wa Miguu na sheria za nchi.
Vitendo vya kuashiria vurugu na kufanya vurugu vikithibitishwa katika taarifa ya Mwamuzi, Janny Sikazwe wa Zambia; Kamishna wa mchezo, Celestin Ntangungira wa Rwanda na Mratibu Mkuu Maalumu kutoka Msumbiji, Sidio Jose Mugadza, hatua zake zitachukuliwa dhidi yake ikiwamo KUONDOLEWA KWENYE MASHINDANO. Vilevile vitendo vya kutishia amani,kudhuru mwili au kuharibu mali vitachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za kijinai.
Katika mchezo huo wa kimataifa Na. 107, Mwamuzi Sikazwe atasaidiwa na Jarson Emiliano dos Santos kutoka Angola atayekuwa kwenye mstari wa kulia (line 1) na Berhe O’Michael wa Eritrea atayekuwa upande wa kushoto (line 2) huku Wellington Kaoma wa Zambia akiwa ni mwamuzi wa akiba.
Wakati huohuo, kikao cha Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini kinatarajia kukaa siku ya Jumamosi tarehe 2 Julai 2016. Taarifa zaidi itatolewa karibuni.
TFF ikiwa msimamizi mkuu wa mpira wa miguu Tanzania, inawajibika na mara moja inachukua nafasi hii kuwatahadharisha baadhi ya viongozi wa Young Africans, wanachama na mashabiki wao kutofanya hivyo kwani itakuwa ni kinyume na kanuni za mashindano na mikataba ya udhamini katika hatua hii.
Ikumbukwe kwamba CAF inamiliki asilimia mia moja ya haki za habari na masoko katika ngazi hii ya makundi na jaribio lolote la kukwamisha matangazo ya biashara au utengenezaji na urushaji wa matangazo ya televisheni au ukwamishaji wa shughuli zingine kama hizo kwa CAF au wakala aliyeteuliwa na CAF kutaigharimu klabu mwenyeji si kwa kutozwa faini tu lakini pia uwezekano wa kuondolewa mashindanoni.
Pia TFF inatoa tahadhari hiyo ikiwamo ile ya utamaduni wa kukaa uwanjani ili kuepusha aina yoyote ya vurugu kwenye michezo yake hususani hii ya hatua ya makundi. TFF inafahamu kuwa tayari viongozi wa Young Africans walikwisha kusoma nyaraka na taarifa mbalimbali kuhusu kanuni na masuala ya udhamini kwa timu zinazofuzu hatua ya Nane Bora.Wapenzi wa Yanga wanaombwa kufika kwa wingi na kuishangilia kwa nguvu timu yao ikiwa ni njia ya kuitia hamasa.Hata hivyo shamrashamra hizo zifanyike kwa kufuata sheria,kanuni na taratibu za Mpira wa Miguu na sheria za nchi.
Vitendo vya kuashiria vurugu na kufanya vurugu vikithibitishwa katika taarifa ya Mwamuzi, Janny Sikazwe wa Zambia; Kamishna wa mchezo, Celestin Ntangungira wa Rwanda na Mratibu Mkuu Maalumu kutoka Msumbiji, Sidio Jose Mugadza, hatua zake zitachukuliwa dhidi yake ikiwamo KUONDOLEWA KWENYE MASHINDANO. Vilevile vitendo vya kutishia amani,kudhuru mwili au kuharibu mali vitachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za kijinai.
Katika mchezo huo wa kimataifa Na. 107, Mwamuzi Sikazwe atasaidiwa na Jarson Emiliano dos Santos kutoka Angola atayekuwa kwenye mstari wa kulia (line 1) na Berhe O’Michael wa Eritrea atayekuwa upande wa kushoto (line 2) huku Wellington Kaoma wa Zambia akiwa ni mwamuzi wa akiba.
Wakati huohuo, kikao cha Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini kinatarajia kukaa siku ya Jumamosi tarehe 2 Julai 2016. Taarifa zaidi itatolewa karibuni.
Sunday, June 26, 2016
KOCHA SHELISHELI AIHOFIA SERENGETI BOYS
Kocha Mkuu wa timu ya soka ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ya Shelisheli, Gavan Jeanne ameonesha kuihofia Serengeti Boys ya Tanzania katika mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Jeanne alionesha hofu hiyo leo Juni 25, 2016 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na mbele ya Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime ambao kwa pamoja walikuwa wakmizungumzia namna walivyoandaa timu zao kwa ajili ya mchezo huo wa kesho.
“Hatujawahi kushiriki michuano ya vijana. Hii ni mara yetu ya kwanza. Tumekuja kujifunza kwa wenzetu Tanzania ambao wana uzoefu,” alisema Jeanne ambaye pia alithibitisha kuwa hawajawahi kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
Kwa upande wa Bakari Shime wa Serengeti Boys, alisema ameindaa mechi hiyo vema kiakili na kimwili kwa ajili ya kuikabili Shelisheli katika mchezo huo ambao hamasa yake imekuwa kubwa kwa kuwa kikosi hicho kinaandaliwa kuwa timu ya taifa baada ya miaka miwili.
Wachezaji wa Serengeti Boys wamesema, watafanya vema kwenye mchezo huo. Wachezaji hao ni Anthony Shilole ambaye alisema: “Tumejifunza mambo mengi, ushindi ni lazima kwa sababu tutafuata maelekezo ya walimu wetu. Tutajitahidi tushinde.”
Ally Ng’anzi: Maandalizi ni mazuri. Mechi ya Jumapili tumejiandaa vema. Tunashinda tena kwa magoli mengi.”
Ally Msengi: “Watanzania watarajie ushindi baada ya maandalizi ya muda mrefu. Timu iko kambini kitambo.”
Kennedy Nashony: Tutapambana kadiri ya uwezo. Kila mechi kwetu ni fainali. Hatuko tayari kupoteza ili kukosa mechi zijazo.”
Shelisheli ilitua Ijumaa usiku saa 7.45 usiku ikiwa na viongozi 25 na imefikia hoteli ya Southern Sun iliyoko katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Waamuzi wanne kutoka Ethiopia, ndio watakaochezesha mchezo huo. Waamuzi hao ni Belay Tadesse Asserese ambaye ni mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Tigle Gizaw Belachew upande wa kulia na Kinfe Yilma Kinfe upande wa kushoto huku mwamuzi wa akiba atakuwa Lemma Nigussie. Kamishna wa mchezo huo atakuwa ni Bester Kalombo.
Serengeti Boys ilikuwa kambini tangu Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo huo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2, 2016 huko Shelisheli.
Katika kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
SHELISHELI YATUA DAR
Timu ya soka ya Vijana ya Shelisheli, imeingia Dar es Salaam, Tanzania usiku wa kuamkia leo Juni 24, 2016 saa 7.45 usiku wa kuamkia leo Ijumaa Juni 24, 2016, kwa ajili ya mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Timu hiyo imeingia wachezaji na pamoja na viongozi 25 ka ujumla wake na imefikia hoteli ya Southern Sun iliyoko katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Waamuzi wanne kutoka Ethiopia, ndio watakaochezesha mchezo wa kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ na Shelisheli utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo ni wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Waamuzi hao ni Belay Tadesse Asserese ambaye ni mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Tigle Gizaw Belachew upande wa kulia na Kinfe Yilma Kinfe upande wa kushoto huku mwamuzi wa akiba atakuwa Lemma Nigussie. Kamishna wa mchezo huo atakuwa ni Bester Kalombo.
Serengeti Boys ilikuwa kambini tangu Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo huo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2, 2016 huko Shelisheli.
Katika kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
TFF YAIZODOA YANGA
Kumekuwa na taarifa za upotoshaji kuhusu uratibu na ushiriki wa klabu za Tanzania katika mashindano ya kimataifa hususani ushiriki wa Young Africans SC katika mashindano ya Kombe la Shirikisho kwa msimu wa 2015/2016.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limekuwa likitoa kila aina ya msaasa uliowezekana kuisaidia klabu za Young Africans na Azam ambazo ziliwakilisha nchi katika mashindanmo ya kimataifa. Kwa upande wa Young Africans awali walishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na upande wa Azam ilishiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Mtakumbuka, Azam FC ilitolewa na Esperance ya Tunisia katika michuano hiyo na kwa upande wa Young Africans iliposhindwa kufuzu kwa hatua ya Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikashushwa na kucheza na Esperanca Sagrada ya Angola na kuitoa hivyo kufuzu kwa hatua ya Nane Bora ya Kombe la Shirikisho au kwa lugha nyingine, hatua ya Makundi. TFF ikaendelea kuisaidia Young Africans kuhakikisha inashiriki vema katika mashindano hayo.
Sasa, Aprili 21, 2016 Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) lilitoa waraka kwa timu zilizokuwa zinacheza kuwania kuingia hatua ya Makundi (Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho) kupeleka majina ya maofisa watakaohudhuria warsha ya namna ya kuratibu mechi hizo kuelekea fainali. Kadhalika walitakiwa kupeleka vivuli (photocopies) vya hati zao za kusafiria.
Maofisa walihitajika ni meneja wa timu, daktari wa timu na ofisa habari wa timu. Taarifa hiyo ilikuja kabla ya Young Africans kucheza na Esperanca ya Angola. TFF iliwaataarifu Young Africans kwa kuwataka kutuma nyaraka hizo kati ya Aprili 26 na Aprili 28, 2016.
Lengo la warsha ilikuwa ni kujadili maswala ya uratibu, ufundi, udhamini na kanuni za mashindano. CAF ilijitolea kugharamia usafiri, malazi na gharama zote kwa watu watatu kutoka Young Africans SC.
Taarifa hizi na hata ukumbusho (reminders) zilipelekwa kwa baruapepe, simu na hata kuonana ana kwa ana kwa Katibu Mkuu wa Young Africans, Ofisa Habari na Viongozi wengine wa klabu.
Maofisa wa TFF kwa nyakati tofauti tofauti waliwasihi Young Africans na pia kuwakumbusha kutuma majina CAF na vivuli vya hati hati ya kusafiria, lakini kwa sababu wanazoweza kuzielezea wenyewe kwa nini hawakupeleka majina.
Mei 22, 2016 ikiwa ni siku mbili kabla ya warsha kuanza hapo Mei 24, 2016, Kaimu Katibu Mkuu wa Young Africans, Bwana Baraka Deusdedit alituma majina CAF yakiwa hayana vivuli yaani photocopies vya hati ya kusafiria.
Siku moja kabla ya washiriki kuanza kuwasili Cairo, Misri, Kaimu Katibu Mkuu wa Young Africans alituma nyaraka kama zilivyotakiwa na wakatumiwa tiketi tatu (3) na CAF. Pamoja na tiketi kuletwa Young Africans bado watu hao hawakusafiri wakidai klabu haijatoa ruhusa.
Maofisa wa TFF wamekuwa wakifanya kazi mpaka muda wa ziada wakiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Young Africans, Baraka Deusdedit ili timu iweze kushiriki vema pamoja na upungufu wa kiutawala ndani ya sekretarieti yake yanayojidhihirisha wazi.
Masuala yote yanayolalamikiwa na Ofisa Habari wa Young Africans, yaliyotolewa kwa timu zote kwenye semina ya Cairo, Misri.
TFF itaendelea kuvitembelea kusaidia klabu kujenga weledi kupitia mradi wa leseni za klabu na vilevile kuratibu ushiriki wa mashindano mbalimbali.
Hata hivyo, TFF haitasita kuchukua hatua za kinidhamu kwa maofisa wa klabu wanaochafua jina la shirikisho ili kuficha madhaifu yao ya kiutawala (Administrative inefficiencies).
TFF YAKATAA OMBI LA YANGA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limekataa ombi la Young Africans ya Dar es Salaam juu ya kubadili siku na muda wa mchezo dhidi ya T.P. Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Katika taarifa ya CAF iliyofika TFF imesema mchezo huo utafanyika Jumanne Juni 28, 2016 saa 10.00 jioni kama ulivyopangwa awali kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Young Africans kwa upande wao waliomba mchezo huo ufanyike Juni 29, 2016 saa 1.30 usiku.
Kadhalika, kikao cha maandalizi katika mchezo huo kiliochofanyika leo Juni 23, 2016 kimeagiza uongozi wa Young Africans kuwaelimisha mashabiki wao kukaa katika eneo la mazoea tofauti na mipango yao ya kutaka kukaa eneo lote la Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo wa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), utachezeshwa na Mwamuzi Janny Sikazwe wa Zambia.
Sikazwe atasaidiwa na Jarson Emiliano dos Santos kutoka Angola atayekuwa kwenye mstari wa kulia (line 1) na Berhe O’Michael wa Eritrea atayekuwa upande wa kushoto (line 2) huku Wellington Kaoma wa Zambia akiwa ni mwamuzi wa akiba.
Kamishna wa mchezo huo atakuwa Celestin Ntangungira wa Rwanda. Pia mchezo huo utakuwa na Mratibu Mkuu Maalumu kutoka Msumbiji, Sidio Jose Mugadza.
Tuesday, June 21, 2016
DRFA YAINYOOSHEA KIDOLE TFF
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kimesitushwa na kufadhaishwa na maamuzi yaliyofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kutangazwa kwenye vyombo mbali mbali vya habari bila ya kufuata misingi ya KATIBA na KANUNI zinazoongoza katika usimamizi wa mpira katika nchi yetu.
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kupitia KATIBA na KANUNI za TFF, DRFA, na KIFA kimejiridhisha kwamba maamuzi yaliyofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ya kufuta matokeo halali ya uchaguzi wa Chama Cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni uliofanyika siku ya Jumapili tarehe 12/06/2016 katika bwalo la maofisa wa polisi Oysterbay bila hayakuzingatia KATIBA na KANUNI za TFF, DRFA na KIFA.
Maamuzi hayo ya TFF yamevunja katiba ya TFF, DRFA na KIFA pamoja na kanuni zake ambazo ndiyo mwongozo wa mpira wetu hasa katika upatikanaji wa mamlaka za uendeshaji wa mpira katika ngazi mbalimbali za taifa, mkoa na wilaya.
Katiba ya TFF ibara ya 52(2) na ibara ya 52(6)(a) zinaeleza wazi kazi na majukumu ya kamati ya uchaguzi ya TFF ni kwa chaguzi za TFF na wanachama wake ambao ni vyama vya mikoa, vilabu vya ligi kuu na kusimamia uchaguzi wa Board ya ligi pamoja na kuishauri kamati ya utendaji mambo yanayo husiana na chaguzi hizo.
Kwa mujibu wa katiba ya TFF ya 2013 kamati yake ya uchaguzi haiwajibiki na lolote kwa vyama vya mpira wa miguu vya wilaya ambao si wanachama wa TFF. Lakini pia Ibara ya 3(i) ya kanuni za uchaguzi za TFF za 2013 inaeleza kuwa kamati ya uchaguzi ya TFF itaendesha na kusimamia uchaguzi wa TFF na Bodi ya Ligi.
Ibara ya 6 ya kanuni za uchaguzi za TFF za 2013 pia inaeleza majukumu ya kamati ya uchaguzi na katika majukumu yake hakuna popote inapoonyesha kuwa ina mamlaka ya kusimamia na kutolea maamuzi chaguzi za vyama vya mpira wa miguu vya wilaya ambao si wanachama wa TFF.
Kwa mujibu wa Katiba ya KIFA ibara ya 47 na kanuni za uchaguzi kipengele (b) inasema Kamati ya Uchaguzi ya KIFA itafanya kazi kwa kushirikiana na sekretarieti ya Chama na chini ya uangalizi na Miongozo ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA. Kwahiyo ni jukumu la kamati ya uchaguzi ya DRFA kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kugundua kwamba Kamati yake ya Uchaguzi haina mamlaka ya KIKATIBA kuweza kusimamia chaguzi za vyama vya wilaya, miongoni mwa mapendekezo ya mabadiliko ya KATIBA waliyoleta katika Mkutano Mkuu wa TFF wa mwisho uliofanyika Tanga ni pamoja na hilo kuuomba MKUTANO MKUU wa TFF uweze kufanya hilo badiliko ili waweze kusimamia chaguzi za WILAYA lakini BAHATI mbaya marekebisho ya KATIBA hayakuweza kupitishwa na wajumbe wa MKUTANO Mkuu.
Katiba ya KIFA katika kanuni zake za uchaguzi 5 (h) inatamka kwamba RUFAA zote zihusuzo uchaguzi zitawasilishwa kwenye kamati ya RUFAA ya Wilaya na hatimae kama Mrufani hakuridhika basi atakata RUFAA katika kamati ya RUFAA ya Mkoa ambapo uamuzi wake utakuwa ndio wa MWISHO.
Baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya KIFA kutangaza matokeo ya uchaguzi huo tajwa hapo juu na kutuletea ripoti yake, mmoja wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti Bwana Thomas Mazanda aliamua kukata RUFAA katika Kamati ya uchaguzi ya Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kama katiba ya KIFA inavyoelekeza KUPINGA matokeo yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi wa KIFA. Lakini cha kushangaza wakati kamati ya uchaguzi ya DRFA ikipanga kusikiliza RUFAA hiyo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) likaitisha kikao 18/06/2016 na kuamua KUFUTA uchaguzi huo bila kufuata taratibu za KIKATIBA na KIKANUNI zinazotuongoza.
Kamati ya Uchaguzi ya Chama Cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni kwa mujibu wa Ibara ya 47 inaundwa na wajumbe watano. Wajumbe wa kamati hii watateuliwa na Mwenyekiti. Na Mwenyekiti wa kamati hii lazima awe ni mwanasheria na wajumbe wengine wane lazima wawe ni watu wenye ujuzi na upeo katika masuala ya michezo. Kwa mujibu wa katiba ya KIFA haina makamu mwenyekiti wala katibu wa kamati. Na maadam KATIBA inatamka wazi Mwenyekiti lazima awe mwanasheria TAFSIRI yake ni kwamba bila uwepo wa Mwenyekiti kamati haiwezi kuendelea na kazi zake kwa sababu ukiondoa Mwenyekiti wajumbe wengine waliobaki wa kamati ya KIFA hawana taaluma ya SHERIA.
Katika kuakikisha uchaguzi huo wa KIFA una kuwa huru na haki Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya KIFA alialika watu tofauti tofauti kuhudhuriailia katika uchaguzi huo wakiwemo mwakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwenyekiti wa SPUTANZA Taifa na Mjumbe Mmoja wa Kamati ya Utendaji ya TFF katika uchaguzi huo.
Kwa mlolongo huu wa matukio ni dhahiri TFF imepora mamlaka ya kamati ya uchaguzi ya KIFA na DRFA kwa kuingilia na kufuta uchaguzi wa KIFA ambaye KIKATIBA ni mwanachama wa DRFA. Lakini pia TFF hii imefanya MAAMUZI yanayofanana na hayo katika uchaguzi wa Chama Cha Mpira Miguu Wilaya ya Temeke.
Uporaji huu wa madaraka ya mwanachama wa TFF ni HATARI, BATILI na KINYUME cha utaratibu tuliojiwekea hivyo kufanya hata MAAMUZI hayo yaliyofanywa na TFF kuwa BATILI. Hii inatokana na ukweli kuwa kutokana na katiba zetu TFF haina nguvu yoyote ya kikatiba wala kikanuni ya kutolea maamuzi mchakato wa uchaguzi wa chama cha wilaya ambaye ni mwanachama wa chama cha mpira wa miguu cha mkoa.
kwa haya yanayoendelea katika TFF ni dhahiri kuwa taasisi hiyo sasa inaondokana na utaratibu wa kuendesha mambo yake kwa kuegemea misingi ya KATIBA na KANUNI zake na badala yake kuendesha mambo yake ki – imla. Ni jambo la hatari kwa taasisi kubwa kama TFF kuendesha mambo yake ki – imla kwani itapoteza heshima iliyojijengea kwa miaka mingi.
Ni matumaini yetu kuwa HAKI itasimamiwa ipasavyo
Imetolewa na
Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
Monday, June 20, 2016
YANGA YAPIGWA 1-0 NA WAALGERIA
YANGA jana ilianza vibaya michuano ya soka ya ligi ya Kombe la Shirikisho baada ya kuchapwa bao 1-0 na MO Bejaia ya Algeria karika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia.
Katika mchezo huo, Yanga ilipata pigo dakika ya 90 baada ya beki wake, Haji Mwinyi kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kjadi ya pili ya njani.
Bao pekee na la ushindi la Waalgeria lilifungwa na beki Yassine Salhi dakika ya 2, kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Ismail Belkacemi.
Kutokana na matokeo hayo, MO Bejaia inashika nafasi ya pili katika kundi hilo, nyuma ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, ambayo juzi iliichama Adeama ya Ghana mabao 3-1.
Katika mechi zijazo za kundi hilo, Yanga wataikaribisha TP Mazembe kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati MO Bejaia watakuwa wageni wa Adeama mjini Accra.
Tuesday, June 14, 2016
VIWANJA LIGI KUU YA VODACOM NA DARAJA LA KWANZA
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa taarifa kwa barua kwa timu zote zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Ligi daraja la Kwanza ya StarTimes kwa msimu wa 2016/17 kwamba kila timu imetakiwa kuwasilisha jina la Uwanja ambao utatumia kama uwanja wa nyumbani kabla ya Juni 20, 2016.
Barua hiyo iliyotumwa kupitia Bodi ya Ligi (TPLB) ya TFF imeagiza jina la uwanja huo uende sambamba na taarifa za:
– Vipimo vya uwanja
– Iwapo unaweza kutumika kwa mechi za usiku au la
– Idadi ya vyumba vya kubadilishia nguo ‘dressing rooms’
– Uwezo wa uwanja kuingiza mashabiki
– Mmiliki wa uwanja huo
– Aina ya nyasi (asili au bandia)
Tumezielekeza kwamba iwapo timu haina uwanja wa nyumbani unaofaa kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom inaweza kuchagua uwanja mwingine katika mji au mkoa wa jirani. Hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 6 (3) Ligi Kuu Tanzania Bara toleo la 2016/17.
Tayari TFF, limetoa kalenda ya msimu mpya wa mashindano na matukio ambako usajili kuanza Juni 15, 2016. Usajili huo unaanza na uhamisho wa wachezaji ambako utaanza Juni 15, 2016 hadi Julai 30, 2016.
Kwa mujibu wa Kalenda hiyo, timu ambazo hazishiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 zitaanza kutangaza wachezaji walioachwa kuanzia Juni 15, 2016 hadi Juni 30, mwaka huu.
Kwa upande wa timu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), watatumia kipindi cha Juni 15, 2016 hadi Juni 30, 2016 kutangaza usitishwaji mkataba wa wacheaji. Usajili wa utaanza Juni 15 hadi Agosti 6, kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Pingamizi itakuwa ni Agosti 7 hadi 14, 2016 kabla ya kuthibitisha usajili kwa hatua ya kwanza kati ya Agosti 15 na Agosti 19, 2016 wakati usajili hatua ya pili utaanza Agosti 17, 2016 hadi Septemba 7, 2016 na kitafuatiwa kipindi cha kipindi cha pingamzi hatua ya pili kuanzia Septemba 8 hadi Septemba 14, 2016.
Septemba 15 hadi Septemba 17, 2016 itakuwa ni kipindi cha kuthibitisha usajili hatua ya pili,
Ratiba hiyo inasema kwamba timu zinatakiwa kuandaliwa kuanzi Juni 15 2016 hadi Julai 15, 2016 ambako kuanzia Julai 16, 2016 hadi Agosti 14 ni kipindi cha mechi za kirafiki za ndani na nje. Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itatoka kati ya Julai 16 hadi Agosti 14.
SERENGETI BOYS WAINGIA KAMBINI LEO
Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kinaingia kambini leo Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2, 2016 huko Shelisheli.
Makipa:
Kelvin Deogratius Kayego,
Ramadhani Awm Kambwili na
Samwel Edward Brazio.
Mebeki wa Pembeni:
Kibwana Ally Shomari,
Israel Patrick Mwenda,
Anton Shilole Makunga na
Nickson Clement Kibabage.
Mabeki wa Kati:
Dickson Nickson Job
Ally Hussein Msengi na
Issa Abdi Makamba
Viungo wa Kuzuia:
Kelvin Nashon Naftal
Ally Hamis Ng’anzi na
Shaban Zuberi Ada
Mawinga:
Mustapha Yusuph Mwendo
Yassin Muhidini Mohammed
Syprian Benedictor Mtesigwa na
Gadafi Ramadhan Said
Viungo wa kushambulia:
Asad Ali Juma
Mohammed Abdallah Rashid na
Muhsin Malima Makame
Washambuliaji:
Ibrahim Abdallah Ali
Enrick Vitaris Nkosi
Rashid Mohammed Chambo na
Yohana Oscar Mkomola
Katika kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
Kadhalika Serengeti Boys ilicheza mfululizo michezo saba ya kimataifa bila kufungwa dhidi ya Misri (2), India, Korea Kusini, Malaysia na Marekani (USA). Kabla ya hapo timu hiyo ilicheza michezo kadhaa ya ndani na timu za chini ya umri wa miaka 20 bila kupoteza hata mchezo mmoja.
Katika mashindano ya AIFF, timu hiyo pekee kutoka Afrika na ambayo ilikua kipenzi cha mashabiki katika jiji la Goha ilicheza na timu ambazo ziko juu katika hatua za juu katika mtoano wa kuwania kushiriki Kombe la Dunia kupitia mabara yao yaani CONCACAF (USA) na AFC (India, Korea na Malaysia).
Sunday, June 12, 2016
USWISI YAIPIGA ALBANIA 1-0
Switzerland imejipatia ushindi wake wa pili katika michuano ya bara Ulaya baada ya kuilaza Albania 1-0.
Mapema Albania ilionekana kubabaika pale mlinda lango wao Etrit Berisha alipofanya makosa kufuatia Krosi iliopigwa na Xherdan Shaqiri na hivyobasi kuwa rahisi kwa Schar kufunga kwa kichwa.
Lakini baadaye Armando Sadiku alikosa nafasi ya wazi kabla ya nahodha wa kikosi hicho Lorik Cana kupewa kadi ya manjano kwa kuunawa mpira.
Hatahivyo kushindwa kwa Switzerland kuongeza mabao kulifanya matokeo kusalia 1-0,lakini Shkelzen Gashi karibu asawazishe kwa upande wa Albania.
Mchezaji huo wa ziada alipata pasi nzuri huku ikiwa imesalia dakika tatu lakini Kipa Yann Sommer akaupangua mkwaju wake .
MANJI ASHINDA UENYEKITI WA YANGA KWA KISHINDO
WANACHAMA wa klabu ya Yanga, juzi walimchagua tena Yusuph Manji kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo baada ya kupata kura 1,468 kati ya 1,470.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Clement Sanga alichaguliwa tena kuwa makamu mwenyekiti baada ya kupata kura 1,428 kati ya 1,508.
Dalili za Manji kushinda uchaguzi huo zilionekana mapema kutokana na idadi kubwa ya wanachama kumuunga mkono. Hakukuwa na kura ya kumkataa wakati kura mbili ziliharibika. Manji hakuwa na mpinzani.
Nafasi ya makamu mwenyekiti ilikuwa na wagombea wawili, Sanmga na Titus Osoro, ambaye aliwahi kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji kabla ya kuondolewa. Katika nafasi hiyo, Osoro aliambulia kura 80.
Waliochaguliwa kuwa wajumbe wa kamati ya utendaji, idadi ya kura zikiwa kwenye mabano ni Siza Augustino Lymo (1027), Omary Said Amir (1069), Tobias Lingalangala (889), Salim Mkemi (894), Ayoub Nyenzi (889), Samuel Lucumay (818), Hashim Abdallah (727),Hussein Nyika (770).
Wajumbe 12 ambao kura zao hazikutosha katika kuwania nafasi hiyo ni David Luhago (582), Godfrey Mheluka (430), Ramadhani Kampira (182), Edgar Chibura (72), Mchafu Chakoma (69), George Manyama (249), Bakari Malima 'Jembe Ulaya' (577), Lameck Nyambaya (655), Beda Tindwa (452), Athumani Kihamia (558), Pascal Lizer (178)
na Silvester Haule (197).
Saturday, June 11, 2016
UFARANSA YAANZA VIZURI KOMBE LA ULAYA
Timu ya taifa ya soka nchini Ufaransa imeshinda mechi ya ufunguzi wa dimba la kombe la bara Ulaya baada ya kuinyuka Romania, mabao 2-1, katika uwanja wa Stade de France mjini Paris.
Dimitri Payet wa Ufaransa ambaye anaichezea klabu ya West Ham nchini Uingereza alifunga bao la ushindi katika muda wa lala salama.
Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud alifunga bao la kwanza kwa kichwa muda mfupi tu baada ya kipindi cha pili kung'oa nanga, na baadaye Romania wakazawazisha kwa mkwaju wa penalti kutoka kwa Bogdan Stancu.
Usalama umeimarishwa mjini Paris na haswa karibu na uwanja wa Stade de France, ambapo shambulizi baya la kigaidi lilitekelezwa mwaka ulopita.
IBADA YA MAZISHI YA MUHAMMAD ALI YAJAWA NA MIHEMKO
RAIS wa zamani wa Marekani, Bill Clinton akizungumza wakati wa ibada hiyo |
BAADHI ya mbondia wa zamani wa ngumi za kulipwa wakiwa na mwanamuziki Willy Smith wakati wa ibada hiyo |
MKE wa Muhammad Ali, Ronnie wakati wa ibada hiyo |
UMATI wa watu ukiwa umefurika wakati wa ibada hiyo |
MSAFARA wa gari lililobeba jeneza la Ali |
Ibada ya ukumbusho iliojawa na mihemko ya aina yake kwa bondia Mohammed Ali imefanyika katika mji alikozaliwa wa Louisville, Kentucky.
Umati watu 14000 ulisikiliza kwa makini watu wa tabaka na dini tofauti wakimuomboleza mohammed ali kutokana na umahiri wake katika ulingo wa michezo na pia alivyoitunza jamii, huku wakisifu mchango wake katika kuimarisha amani duniani na haki za binadam.
Mkewe Ali, Lonnie Ali, anasema mumewe alikabiliwa na masaibu si haba, bila kuonyesha hasira, na kuwataka watu kufuata mfano wake.
Katika taarifa, rais wa Marekani Barrack Obama, alimtaja Ali kama mtu shupavu, aliyeng'aa na aliyekuwa na ushawishi mkubwa kuliko mtu yeyote wa kizazi chake.
Rais wa zamani Bill Clinton, alikumbuka utanashati, ucheshi na utu aliooonyesha marehemu Ali, wakati akikabiliana na machungu ya ugonjwa uliomdhoofisha.
Friday, June 10, 2016
HASHIM THABEET AMTEMBELEA MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN
Mchezaji wa kikapu wa kulipwa nchini Marekani, Mtanzania Hashim Thabeet akisaini moja ya mpira mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan |
Wednesday, June 8, 2016
TFF YAANZA KUTOA FOMU ZA LESENI KWA KLABU
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeanza kutoa fomu za Leseni za Klabu (Club Licensing) za Ligi ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na zile za Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes.
Klabu hizo zitatumiwa fomu hizo na kutakiwa kuzijaza na kuzirejesha kabla ya Juni 19, mwaka huu ikiwa ni siku 10 mara baada ya Bodi ya Ligi ya TFF (TPLB) kuwatuamia fomu hizo. Klabu itakayojaza fomu hizo kwa wakati ndiyo ambayo maombi yake ya leseni yatashughulikiwa mapema.
Tayari TFF imeteua Kamati ya Leseni ya Klabu (Club Licensing Committee) ambayo ndiyo yenye jukumu la kupitia maombi ya leseni kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza na kutoa uamuzi wa kuzikubali au kuzikataa kwa kuzingatia Kanuni ya Leseni ya Klabu.
Wajumbe walioteuliwa kwenye Kamati hiyo inayoundwa kwa mara ya kwanza ni Wakili Lloyd Nchunga (Mwenyekiti), Wakili Emmanuel Matondo (Makamu Mwenyekiti), David Kivembele, Hamisi Kissiwa na Prof. Mshindo Msolla.
Klabu zinatakiwa kuchukua fomu za maombi TFF ambapo baada ya kuzirejesha zitafanyiwa kazi ambapo zile zitakazokuwa zimekidhi matakwa ya Kanuni husika zitapatiwa leseni husika ili zishiriki michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes kwa msimu wa 2016/2017.
Kwa klabu ambazo zitashindwa kukidhi matakwa ya leseni yanayolenga kuhakikisha mpira wa miguu unaendeshwa kwa weledi na kupiga vita upangaji matokeo katika maeneo matano ya wachezaji (sporting), viwanja (infrastructure), utawala (administrative and personnel), umiliki wa klabu (ownership) na fedha (financial), hazitapa leseni hivyo kutokuwa na sifa ya kushiriki ligi.
Klabu ambazo zitanyimwa leseni na kutoridhika na uamuzi huo, zitakuwa na fursa ya kukata rufani kwenye Kamati ya Rufani ya Nidhamu ya TFF. Kwa mujibu wa Ibara ya 5(3) ya Kanuni ya Leseni ya Klabu ya TFF, Kamati hiyo ndiyo itakayosikiliza rufani zinazopinga uamuzi wa Kamati ya Leseni ya TFF.
SERENGETI BOYS KUIENDEA KAMBINI SHELISHELI
Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) inataingia kambini Juni 13, 2016 kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli utakaofanyika Juni 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2, 2016 huko Shelisheli.
Katika kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
Kadhalika Serengeti Boys ilicheza mfululizo michezo saba ya kimataifa bila kufungwa dhidi ya Misri (2), India, Korea Kusini, Malaysia na Marekani (USA). Kabla ya hapo timu hiyo ilicheza michezo kadhaa ya ndani na timu za chini ya umri wa miaka 20 bila kupoteza hata mchezo mmoja.
Katika mashindano ya AIFF, timu hiyo pekee kutoka Afrika na ambayo ilikua kipenzi cha mashabiki katika jiji la Goha ilicheza na timu ambazo ziko juu katika hatua za juu katika mtoano wa kuwania kushiriki Kombe la Dunia kupitia mabara yao yaani CONCACAF (USA) na AFC (India, Korea na Malaysia).
Haishangazi nchi nyingi za Ulaya, Asia na Marekani zimeulizia uwezekano wa timu hii kutembelea nchi zao kwa michezo ya kirafiki.
Awali timu ya Serengeti Boys ilipewa nafasi ndogo ya kufanya vizuri kwa sababu ya rekodi zilizokuwa zinaiweka Tanzania katika viwango vya chini katika umri huo kwa nchi za Afrika Magharibi na Kaskazini zilikuwa juu zaidi na vilevile ukweli wa kwamba timu kama USA, Korea, Malasyia na India zilikuwa na bajeti kubwa iliyogharamiwa na Serikali zao na walikuwa na vifaa vya kila namna kiasi cha kuomba magari kwa ajili ya vifaa vya mazoezi na mechi.
Serengeti Boys ilimaliza Mashindano ya AIFF katika nafasi ya tatu kwa kuifunga Malaysia mabao 3-0. Serengeti Boys na Bingwa Korea hawakupoteza mchezo hata mmoja na awali walipokutana walitoka sare ya 2-2.
MALINZI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA KESHI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa Kocha Mkuu wa zamani wa Nigeria, Stephen Okechukwu Keshi (54) kilichotokea ghafla leo Juni 08, 2016 kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa.
Kutokana na kifo hicho, Rais Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Shirikisho la Soka Nigeria (NFF), Amaju Pinnick, familia ya marehemu Keshi pamoja na ndugu, jamaa, marafiki walioguswa na msiba huo wa gwiji huyo aliyepata kuwa nahodha wa kikosi cha Taifa Nigeria ‘Super Eagles’.
Katika rambirambi ambazo zimefika pia katika Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA), Rais Malinzi amesema kuwa japokuwa Keshi ametangulia mbele za haki, mchango wake kwenye mpira wa miguu hautasahaulika kwani atabaki kuwa alama ya maendeleo ya mchezo wa soka.
SAMATTA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA TTB KUITANGAZA TANZANIA
Na Geofrey Tengeneza
Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Ally Samatta (23) anayecheza kandanda la kulipwa katika klabu ya Genk nchini Ubelgiji amekubali ombi la Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuwa Balozi wa Hiari wa Tanzania na kusaidia kuitangaza Tanzania kama eneo la Utalii nchini Ubelgiji na Ulaya kwa ujumla.
Samatta ametoa ahadi hiyo leo alipotembelea ofisi za Bodi ya Utalii jijini Dar es salaam na kuwa na mazungumzo na Menejimenti ya Bodi hiyo kuhusu kumtumia katika kutangaza vivutio vya utalii na Tanzania kimataifa.
“ Kama mtanzania ninawiwa kwa nchi yangu hivyo nina furaha na niko tayari kitangaza nchi yangu kama eneo la utalii popote nitakapokuwa” alisema.
Aliongeza kwamba nchi nyingi duniani hutumia watu wao maarufu ikiwa ni pamoja na wachezaji wa kimataifa kuzitangaza nchi zao.
Ameipongeza Bodi TTB kwa mkakati wa kuwatumia watanzania mbalimbali maarufu katika kuitangaza Tanzania akaahidi kufanya kila litakalowezekana ikiwemo kutumia mitandao yake ya kijamii kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya utalii.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota mdachi amedokeza kuwa TTB itatazama namna nzuri kabisa ya kumtumia Mbwana Samatta kutangaza utalii wa Tanzania na Tanzania kwa ujumla kama eneo zuri kwa utalii.
Mbwana Samatta amesaini mkataba wa kuichezea klabu ya Genk ya Ubelgiji utakaomalizika mwaka 2020. Sammata ambaye ni Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa star, alitwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika.
Mbwana Samatta (katikati) katika picha ya pamoja na wajumbe wa Menejimenti ya TTB wakiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi hiyo Bi Devota Mdachi.
Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Ally Samatta (23) anayecheza kandanda la kulipwa katika klabu ya Genk nchini Ubelgiji amekubali ombi la Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuwa Balozi wa Hiari wa Tanzania na kusaidia kuitangaza Tanzania kama eneo la Utalii nchini Ubelgiji na Ulaya kwa ujumla.
Samatta ametoa ahadi hiyo leo alipotembelea ofisi za Bodi ya Utalii jijini Dar es salaam na kuwa na mazungumzo na Menejimenti ya Bodi hiyo kuhusu kumtumia katika kutangaza vivutio vya utalii na Tanzania kimataifa.
“ Kama mtanzania ninawiwa kwa nchi yangu hivyo nina furaha na niko tayari kitangaza nchi yangu kama eneo la utalii popote nitakapokuwa” alisema.
Aliongeza kwamba nchi nyingi duniani hutumia watu wao maarufu ikiwa ni pamoja na wachezaji wa kimataifa kuzitangaza nchi zao.
Ameipongeza Bodi TTB kwa mkakati wa kuwatumia watanzania mbalimbali maarufu katika kuitangaza Tanzania akaahidi kufanya kila litakalowezekana ikiwemo kutumia mitandao yake ya kijamii kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya utalii.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota mdachi amedokeza kuwa TTB itatazama namna nzuri kabisa ya kumtumia Mbwana Samatta kutangaza utalii wa Tanzania na Tanzania kwa ujumla kama eneo zuri kwa utalii.
Mbwana Samatta amesaini mkataba wa kuichezea klabu ya Genk ya Ubelgiji utakaomalizika mwaka 2020. Sammata ambaye ni Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa star, alitwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika.
Mbwana Samatta (katikati) katika picha ya pamoja na wajumbe wa Menejimenti ya TTB wakiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi hiyo Bi Devota Mdachi.
NYOTA WA ZAMANI NIGERIA, STEPHEN KESHI AFARIKI
Mmoja wa wachezaji maarufu wa soka barani Afrika Stephen Keshi amefariki akiwa na umri wa miaka 54, shirikisho la Nigeria limethibitisha.
Nahodha huyo wa zamani wa kikosi cha Nigeria, Keshi,alikuwa mmoja wa watu wawili pekee kushinda michuano ya kombe la bara Afrika akiwa mchezaji na kocha.
Pia alifunza Togo na Mali,na aliwahi kuichezea timu ya Anderlecht ya Ubelgiji.
Anadaiwa kuugua mshtuko wa moyo,kulingana na vyombo vya habari vya taifa hilo.
Akiwa mchezaji ,keshi alikuwa katika kikosi cha Super Eagles kilichoshinda kombe la bara Afrika mnamo mwaka 1994 na kushindwa kushirki katika mechi za robo fainali za kombe la dunia mwaka huohuo.
Alikuwa mkufunzi wa kikosi cha Nigeria kwa vipindi vitatu ,na kuisaidia Nigeria kufuzu katika michuano ya bara Afrika 2013 nchini Afrika Kusini pamoja na kombe la dunia mwaka 2014 huko Brazil.
OBAMA KUTOHUDHURIA MAZISHI YA MUHAMMAD ALI KESHOKUTWA
Rais wa Marekani Barrack Obama hatohudhuria mazishi ya marehemu Muhammad Ali siku ya Ijumaa,kulingana na Ikulu ya rais.
Ali alifariki Ijumaa iliopita akiwa na umri wa miaka 74 katika hospitali moja huko Phoenix, Arizona.
Viongozi duniani watakuwa miongoni mwa maelfu watakaohudhuria mazishi hayo yatakayofanyika katika eneo la Louisville,Kentucky ambapo Ali alizaliwa.
Ikulu ya White House imesema bw Obama na mkewe Ali, Lonnie walizungumza kwa njia ya simu.
Miongoni mwa wale watakaohudhuria ni rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na mfalme Abdullah wa Jordan.
Aliyekuwa bingwa wa ndondi katika uzani mzito duniani Lennox Lewis na muigizaji Will Smith ambaye aliigiza kama Ali ni miongoni mwa wale watakaobeba jeneza lake.
Subscribe to:
Posts (Atom)