KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, August 31, 2014

SIMBA YAIPIGA KMKM 5-0


TIMU kongwe ya soka nchini, Simba jana usiku iliibugiza KMKM mabao 5-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.


Katika mechi hiyo, Kocha Patrick Phiri wa Simba aliendelea kukitumia kikosi kile kile, ambacho kimecheza mechi tatu za kirafiki mjini hapa.

Kipigo hicho ni cha pili mfululizo kwa KMKM. Jumatano ya wiki iliyopita, KMKM ilipigwa mabao 2-0 na Yanga kwenye uwanja huo.

Mshambuliaji Hamisi Tambwe aliendelea kudhihirisha kuwa ni tishio katika kuzifumania nyavu baada ya kuifungia Simba mabao mawili kati ya matano. Mabao mengine yalifungwa na Amri Kiemba, Ramadhani Singano na Elius Maguri.

Kocha Phiri alilazimika kubadili kikosi chake chote cha kwanza na kuingiza wachezaji wengine katika kipindi cha pili.

Katika mechi hiyo, Emmanuel Okwi, ambaye usajili wake umezua utata, alijikuta akisugua benchi kama ilivyokuwa kwa beki Donald Musoti, ambaye amechwa kwa vile ana mipangoa ya kwenda Arabuni.

Viongozi kadhaa wa Simba, wakiwemo wanaounda kundi la Marafiki wa Simba, walikuwepo uwanjani kushuhudia mechi hiyo.

YANGA SC YAUNDA KAMATI ZA SHERIA, MAADILI, NIDHAMU NA UCHAGUZI




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MWANASHERIA Sam Mapande, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya YANGA –(Utawala Bora)
anapenda kutoa taarifa kupitia vyombo vya habari kwa wana YANGA, ameunda Kamati ndogo chini ya
Kamati ya Utendaji wa YANGA zifuatazo:

1) KAMATI YA MAADILI
Wajumbe:
1) Fimbo, Mgongo Prof. (Advocate)
2) Kabudi, Mpalamaganda Prof. (Advocate)
3) Njaa, Salehe Ramadhani (Advocate)
4) Rashidi, Tausi Abdallah (Advocate)
5) Tenga, Cathbert (Advocate)

2) KAMATI YA NIDHAMU
Wajumbe:
1) Karua, Tedy
2) Lamlembe, Roger
3) Kihanga, Pascal
4) Mahenge, Burton Yesaya
5) Mudhihir, Mudhihir (Advocate)

3) KAMATI YA SHERIA NA KATIBA
Wajumbe:
1) Fimbo, Mgongo Prof. (Advocate)
2) Gikas, Farija (Advocate)
3) Kabisa, Jessica (Advocate)
4) Kabudi, Mpalamaganda Prof. (Advocate)
5) Kambamwene, January (Advocate)
6) Lupogo, Herman (Advocate)
7) Madibi, Richard (Advocate)
8) Mahenge, Burton Yesaya
9) Mgongolwa, Alex (Advocate)
10) Mkucha, Elisha (Advocate)
11) Mudhihir, Mudhihir (Advocate)
12) Njaa, Salehe Ramadhani (Advocate)
13) Rashidi, Tausi Abdallah (Advocate)
14) Tenga, Cathbert (Advocate)
15) Tenga, Ringo Dr. (Advocate)
16) Vedasto, Audax (Advocate

4) KAMATI YA UCHAGUZI
Wajumbe:
1) Kajole, Mustafa
2) Lundenga, Hashim Ibrahim
3) Makele, Bakili
4) Mlelwa, Daniel
5) Ngongolwa, Alex (Advocate)

Ifahamike kwamba, kutakuwa na nyongeza ya uteuzi wa Wajumbe wengine wa Kamati za YANGA
zilizotajwa hapo juu.

Mwanasheria Sam Mapande, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya YANGA – (Utawala Bora) atakuwa
Mwenyekiti wa Kamati zilizotajwa hapo juu.

Kamati ya Utendaji ya YANGA, ina karibisha Wajumbe waliotajwa katika Kamati zilizotajwa hapo juu
kwa dhamira njema kuwa watasaidia kujenga YANGA bora, na wanaomba ushirikiano kutoka kwa
wanaYanga wote ili Wajumbe walioteuliwa waweze kutenda kazi zao vyema kwa manufaa ya YANGA.

(YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO)
(BENO NJOVU)
KATIBU MKUU WA YANGA.

Tuesday, August 26, 2014

JK AMPA ZAWADI LUIS FIGO


 
RAIS Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi ya kinyago mchezaji veterani wa timu ya Real Madrid ya Hispania, Luis Figo wakati wa hafla ya chakula cha jioni aliyowaandalia wachezaji wa timu hiyo na timu ya maveterani ya Taifa Stars Ikulu jijini Dar es Salaam juzi usiku baada ya mechi ya kirafiki ambapo Real Madrid illifungaTaifa Stars 3-1 katika Uwanja wa Taifa.  (Picha na Freddy Maro).

26 WAITWA TAIFA STARS, KUIVAA MOROCCO SEPTEMBE 5


KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Taifa, Mart Nooirj ametangaza kikosi cha wachezaji 26 kitakachocheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Morocco.

Mechi hiyo, ambayo imo kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA), imepangwa kuchezwa Septemba 5 mwaka huu nchini Morocco.


Wachezaji wapya waliomo kwenye kikosi hicho ni kiungo Said Ndemla wa Simba SC na washambuliaji Mwagane Yeya wa Mbeya City na Juma Luizio wa ZESCO United ya Zambia.

Kikosi kamili ni makipa; Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni Said Morad (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Shomari Kapombe (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Azam), Aggrey Morris (Azam), Joram Mgeveke (Simba) na Charles Edward (Yanga).

Viungo; Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba), Said Juma (Yanga) na Haruna Chanongo (Simba).

Washambuliaji; John Bocco (Azam), Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City) na Juma Liuzio ZESCO, Zambia).

Kikosi hicho kinatarajiwa kuingia kambini Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) mchana katika hoteli ya Accomondia mjini Dar es Salaam na kitakuwa kikifanya mazoezi Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

WATAKAOPANGA MATOKEO KUFUNGIWA MAISHA, BONIFACE WAMBURA AULA TFF



KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeamua kuanzia sasa adhabu kwa watu

wanaotoa rushwa au kupanga matokeo katika mchezo huo itakuwa ni kufungiwa maisha kujishughulisha
na mchezo huo.

Taarifa katika tovuti ya TFF imesema kwamba hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo juzi.

Kwa muda sasa, kumekuwa na tuhuma nyingi za wachezaji na marefa kuhongwa ili kupanga matokeo-
lakini hakukuwa na sheria madhubuti ya kupambana na hali hiyo- lakini kwa hatua hii mpya ya TFF
dhahiri itasaidia kupunguza mchezo huo mchafu.

Aidha, baada ya Libya kujitoa kuwa mwenyeji wa Fainali za Afrika (AFCON) za 2017, Shirikisho la
Soka Afrika (CAF) limealika nchi wanachama kuomba uenyeji wa fainali hizo.

Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Agosti 24, mwaka huu imeamua Tanzania kuomba uenyeji wa
fainali hizo.

“Tunatambua kuwa moja ya masharti ya kuandaa fainali hizo ni pamoja na nchi kuwa imeandaa moja ya
mashindano ya vijana. Lakini kwa kuwa suala hili liko katika mazingira maalumu (exceptional
circumstances) tunaamini CAF watafikiria ombi letu kwa msingi huo,”.

Awali Libya ilipewa uenyeji wa fainali hizo 2015, lakini zikahamishiwa Afrika Kusini kutokana na sababu za kiusalama. Hivyo, Libya ikapewa fainali za 2017 ambapo sasa imejitoa yenyewe kuandaa fainali hizo.

Wakati huo huo: Kamati ya Utendaji ya TFF imemteua Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi mpya wa Mashindano kuanzia Septemba 1 mwaka huu.

Kabla ya uteuzi huo, Wambura alikuwa Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF kuanzia Januari 1, 2011.
Nafasi hiyo sasa iko wazi na itajazwa baadaye na Kamati ya Utendaji.



Sunday, August 24, 2014

TANZANIA ELEVEN ILIPOMENYANA NA WAKONGWE WA REAL MADRID


Beki wa Tanzania Eleven, Salum Sued akijaribu kumdhibiti mshambuliaji wa wachezaji wakongwe wa Real Madrid ya Hispania, De La Red
 Manahodha wa Tanzania Eleven, Mohamed Mwameja na wa Real Madrid, Andress Sabido wakipiga kura kabla ya kuanza mchezo huo
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akitambulishwa kwa mmoja wa wachezaji wa Tanzania Eleven.
Rais Jakaya Kikwete akipunga mkono kwa mashabiki waliofika kushuhudia pambano kati ya Tanzania Eleven na wachezaji wakongwe wa Real Madrid.
 Kikosi cha wachezaji wakongwe wa klabu ya Real Madrid ya Hispania

Kikosi cha wachezaji wa zamani wa timu ya Tanzania Eleven
Nahodha wa Tanzania Eleven, Mohamed Mwameja akisalimiana na mwenzake wa Real Madrid, Andress Sabido. Katika mechi hiyo, Real Madrid ilishinda mabao 3-1.

SITTI MTEMVU NDIYE MISS TEMEKE 2014

Redd's Miss Temeke 2014, Sitti Mtemvu akipunga mkono huku akiwa na mshindi wa Pili, Salma Saleh (kushoto) na watatu, Neema Mollel, baada ya kutangazwa kuwa washindi wa shindano hilo.

Thursday, August 21, 2014

SIMBA, YANGA KUVAANA OKTOBA 12 LIGI KUU


Add caption


MIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga inatarajiwa kushuka dimbani Oktoba 12 mwaka huu katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara.

Ratiba ya ligi hiyo iliyotolewa jana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), inaonyesha kuwa mechi hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ratiba, miamba hiyo ya soka inatarajiwa kurudiana Februani 2015 katika mechi ya mzunguko wa pili itakayochezwa kwenye uwanja huo.

Michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara imepangwa kuanza Septemba 20 mwaka huu, ikitanguliwa na mechi ya kuwania Ngao ya Jamii kati ya mabingwa watetezi, Azam na Yanga zitakazomenyana Septemba 12 mwaka huu.

Katika mechi za ufunguzi wa ligi hiyo, Azam itamenyana na Polisi Moro kwenye Uwanja wa Azam Complex, Mtibwa Sugar itaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Stand United itavaana na Ndanda FC mjini Shinyanga, Mgambo JKT na Kagera Sugar mjini Tanga, Ruvu Shooting na Prisons mjini Pwani, Mbeya City na JKT Ruvu mjini Mbeya, Simba na Coastal Union mjini Dar es Salaam.

Tuesday, August 19, 2014

MTIBWA, POLISI MORO KUCHEZA MECHI YA TIKETI ZA ELEKTRONIKI



Timu za Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro zinazojiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zitacheza Jumamosi (Agosti 23 mwaka huu) mechi ya majaribio ya mfumo wa tiketi za elektroniki.

Mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuanzia saa 10 jioni wakati kiingilio kitakuwa sh. 1,000.

Tiketi za mechi hiyo zitaanza kuuzwa kesho (Agosti 20 mwaka huu) kupitia mtandao wa M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka 30 ya Fahari Huduma yaliyopo katika wilaya zote za Mkoa wa Morogoro, wengi wao wakiwa Morogoro Mjini.

Washabiki 100 wa kwanza kuingia uwanjani wapata jezi za timu za Mtibwa Sugar na Polisi.

Tayari mechi ya majaribio ya tiketi za elektroniki imeshafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ambapo timu za Tanzania Prisons na Mbeya City zilipambana na kutoka sare.

Mechi nyingine za majaribio ya tiketi za elektroniki zitachezwa Agosti 30 mwaka huu. Uwanja wa Mkwakwani jijini utakuwa na mechi kati ya Coastal Union na Mgambo Shooting wakati katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ni Kagera Sugar dhidi ya mabingwa wa Mkoa wa Kagera, Eleven Stars.

Septemba 6 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa kutakuwa na mechi kati ya Simba na Mtibwa Sugar. Mechi nyingine ni ya Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga itakayofanyika Septemba 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

WAAMUZI KUFANYA MTIHANI WA UTIMAMU WA MWILI
Waamuzi wanaotarajia kuchezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu huu watafanya mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) mwezi ujao.

Mtihani huo utahusisha waamuzi wa daraja la kwanza (class one) wakiwemo pia wale wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Mbali ya mtihani huo unaotarajiwa kufanyika kabla ya Septemba 10 mwaka huu, pia kutakuwa na semina kwa makamishna ambao watasimamia mechi za VPL na FDL.

Hivyo waamuzi wote wanatakiwa kutumia muda uliobaki kufanya maandalizi kwa ajili ya mtihani huo.

MAKOCHA COPA COCA-COLA KUNOLEWA DAR
Makocha wa kombaini za mikoa zitakazoshiriki Copa Coca-Cola mwaka 2014 pamoja na waamuzi vijana wa michuano hiyo watashiriki kozi ya ukocha na uamuzi itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 25 hadi 29 mwaka huu.

Kozi hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 25 hadi 29 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi michuano ya Copa Coca-Cola ngazi ya Taifa itakayochezwa Septemba mwaka huu.

Makocha watakaoshiriki kozi hiyo na mikoa yao kwenye mabano ni Ahmed Simba (Mwanza), Ally Kagire (Kagera), Aloyce Mayombo (Pwani), Andrew Zoma (Tabora), Anthony Mwamlima (Mbeya), Athuman Kairo (Morogoro), Bakari Ali (Kaskazini Pemba) na Charles Mayaya (Shinyanga).

Fidelis Kalinga (Iringa), Gabriel Gunda (Singida), Hafidh Muhidin Mcha (Kusini Pemba), Hamis Mabo (Kigoma), John William (Geita), Joseph Assey (Shinyanga), Joseph Haley (Manyara), Jumanne Ntambi (Kilimanjaro), Leonard Jima (Ruvuma), Madenge Omari (Mara), Mohamed Muya (Dodoma), Nicholas Kiondo (Ilala) na Nurdin Gogola (Temeke).

Osuri Kosuli (Simiyu), Peter Amas (Arusha), Ramadhan Abdulrahman Ramadhan (Mjini Magharibi), Renatus Mayunga (Kinondoni), Samwel Moja (Lindi), Seif Bakari (Katavi), Shaweji Nawanda (Mtwara), Sheha Khamis Rashid (Kaskazini Unguja), Tigana Lukinjo (Njombe), Yusuf Ramadhan Hamis (Kusini Unguja), Zahoro Mohamed (Tanga) na Zakaria Mgambwa (Rukwa).

Waamuzi vijana watakaoshiriki kozi hiyo chini ya Mkufunzi wa FIFA, Felix Tangawarima wa Zimbabwe ni 33. Kwa upande wa ukocha Mkufunzi ni Ulric Mathiott kutoka Shelisheli.

KOZI YA UKOCHA LESENI A KUFANYIKA SEPTEMBA 4
Kozi ya ukocha wa Leseni A inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itafanyika mara ya kwanza nchini, jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 4 mwaka huu.

Mkufunzi wa kozi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume atatoka CAF, na itamalizika Septemba 8 mwaka huu wakati ada ya ushiriki ni sh. 300,000.

Washiriki wa kozi hiyo ni wale wenye leseni B ya ukocha ya CAF. Fomu kwa ajili ya ushiriki wa kozi hiyo zinapatikana kwenye ofisi za TFF na tovuti ya TFF

OKWI BYE BYE YANGA, KIKOSI CHATUA PEMBA



KLABU ya Yanga imeondoka mjini Dar es Salaam jana kwenda Pemba kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa kwa michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Yanga imekwenda Pemba bila ya mshambuliaji wake nyota, Emmanuel Okwi kutoka Uganda, ambaye ameshindwa kuripoti kambini kwa wakati uliopangwa.

Katibu Mkuu wa Yanga, Benno Njovu alisema jana kuwa, kikosi hicho kimekwenda Pemba kikiwa na msafara wa watu 35.

Njovu alisema kwa sasa wameamua kuachana na Okwi na kwamba hawatakuwa na muda tena wa kumjadili mshambuliaji huyo.

Kiongozi huyo wa Yanga alisema, klabu yake imeamua kuelekeza nguvu zaidi katika ligi kuu, inayotarajiwa kuanza Septemba 20 mwaka huu.

Alisema benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Marcio Maximo, litaendelea kutoa mafunzo kwa wachezaji waliokwenda Pemba.

"Kwa sasa hatuwezi kuzungumzia suala la Okwi, muda ukifika, tutaweka bayana, tumeamua kujikita zaidi kwenye mazoezi,"alisema Njovu.

Awali, Maximo alikaririwa akisema kuwa, atatoa kipaumbele kwa wachezaji waliofanya mazoezi ya pamoja kwa takriban miezi miwili na kwamba mchezaji, ambaye hayupo, hatakuwa na chake.

Okwi ndiye mchezaji pekee,ambaye hajaripoti kambini hadi sasa tangu alipokwenda kuichezea Uganda katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Yanga inatakiwa kukata jina la mchezaji mmoja wa kigeni kati ya sita ilionao kama sheria za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zinavyotaka.

Wachezaji wa kimataifa waliopo Yanga ni Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima (Rwanda), Hamisi Kiiza (Uganda), Genilson Santos 'Jaja' na Andrey Coutinho (Brazil).

Kwa mujibu wa Njovu, Yanga inatarajia kucheza mechi mbili za kirafiki, moja dhidi ya Chipukizi ya Pemba na nyingine dhidi ya timu kutoka nje ya nchi.

Njovu alisema kikosi cha Yanga kitakuwa kikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gombani ulioko Pemba, ambao umewekewa nyasi za bandia.

Yanga inatarajia kukata utepe wa ligi kuu kwa kumenyana na mabingwa watetezi, Azam katika mechi ya kuwania Ngao ya Jamii, itakayopigwa Septemba 13 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Monday, August 18, 2014

FIFA KUBORESHA MAKAO MAKUU YA TFF




Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani (FIFA) limeahidi kuboresha makao makuu ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) yaliyoko kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Ilala ili yawe katika kiwango cha kisasa ikiwa ni
pamoja na kuwa na vitendea kazi na miundombinu ikiwa ni pamoja na upanuzi
wa ofisi.

Hatua hiyo itaiwezesha TFF kuwa na mazingira bora ya
kufanya shughuli zake kwa ufanisi.

Vilevile kupitia programu zake mbalimbali ikiwemo ile ya Goal, FIFA imeahidi
kushirikiana na TFF katika kuendeleza mradi wa kiuchumi kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume.

Mwanzoni mwa mwaka huu, TFF ilihamishia makao yake makuu katikati ya
jiji ili kupisha maendeleo ya kuiwezesha Karume kuwa kituo cha kisasa kwa
michezo na vitega uchumi.

Akiongea mwishoni mwa ziara ya kikazi nchini, Meneja Miradi wa FIFA
anayeshughulikia Programu za Afrika, Zelkifli Ngoufonja amesema
FIFA inaunga mkono wazo la kuboresha makao makuu ya Karume na itasaidia
kwa awamu uboreshaji huo.

Katika kuhakikisha usimamizi na utekelezaji
barabara wa mradi huo, ujumbe huo wa FIFA ulikubaliana na Kamati ya
Utendaji ya TFF kuboresha ofisi za Karume ili jengo la utawala lianze
kutumika huku mradi ukitekelezwa kwa awamu.

Pamoja na kuongelea mradi huo muhimu kimichezo na kibiashara, ujumbe huo
uliokuwa nchini kwa juma moja kufuatia mwaliko wa TFF ulikuwa na nafasi ya
kujadiliana na TFF kuhusu maboresho katika masuala mbalimbali yakiwemo ya
Utawala, Fedha, Masoko, Ufundi, Mashindano na timu za taifa.

Akiongea kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya TFF, Rais wa TFF Jamal Malinzi
aliushukuru ujumbe huo wa FIFA kwa msaada mkubwa katika historia ya
mahusiano kati ya FIFA na TFF.

Ujio huo unafuatia maombi ya TFF kuwa sehemu ya mradi wa Performance wa
FIFA. Mradi wa Performance unaoshirikisha nchi
mashirikisho 163 kati ya wanachama 209 wa FIFA, unalenga kuongeza ufanisi
katika uendeshaji na uongozi wa nchi wanachama wa FIFA.

TFF KUREJESHA OFISI ZAKE KARUME



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeamua kurejesha ofisi zake Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kwa vile mipango ya uendelezaji wa eneo hilo bado haijakwenda kama ilivyopangwa awali.

Uendelezaji wa eneo utafanyika wakati ofisi zikiwa hapo hapo, na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) litasaidia katika uendelezaji huo utakaofanyika kwa awamu.

Vilevile FIFA imeahidi kusaidia uboreshaji wa ofisi za Uwanja wa Karume ili ziwe katika mazingira bora zaidi ya kufanyika kazi.

Uamuzi huo ni moja ya maazimio yaliyofikiwa kati ya Kamati ya Utendaji ya TFF na ujumbe wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) uliokuwepo nchini kwa wiki nzima kwa ajili ya kufanya mapitio (review) ya uendeshaji wa TFF.

Akizungumza Dar es Salaam leo (Agosti 17 mwaka huu), kiongozi wa ujumbe huo wa FIFA uliokuwa na maofisa sita, Zelkifli Ngoufonja amesema wamepitia maeneo mbalimbali ya uendeshaji wa TFF na mpira wa miguu kwa ujumla na kukubaliana kufanya uboreshaji kwa lengo la kuongeza ufanisi.

Ngoufonja ambaye ni Meneja Mwandamizi wa FIFA anayeshughulikia Programu za Maendeleo Afrika amesema kabla walikutana na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali kwa lengo la kuangalia jinsi watakavyochangia katika uendelezaji mpira wa miguu nchini.

Amesema wamekubaliana na TFF katika mpango wa utekelezaji (Action Plan) na maazimio waliyokubaliana ikiwemo na muda wa utekelezaji wake, hivyo FIFA watafuatilia na kutoa msaada ili kuhakikisha utekelezaji unafanyika kama ilivyopangwa.

Maeneo yaliyofanyiwa kazi ni utawala bora (Governance), Maendeleo ya Ufundi (Technical Development), timu za Taifa (National teams), Mashindano na Vitendea Kazi (Competitions and Facilities), na Utawala na Uongozi (Administration and Management).

Maofisa wengine wa FIFA waliofuatana na Ngoufonja ambaye ni raia wa Cameroon ni Meneja wa Programu za Ustawi (Performance), Marco Schuepp, Ofisa Maendeleo, Ashford Mamelodi, Ofisa Maendeleo wa Ufundi, Govinden Thondoo, Mkufunzi wa Makocha, John Peacock na Mshauri wa Programu za Ustawi, Ian Riley.

MUDA WA USAJILI WASOGEZWA MBELE KWA SIKU MOJA



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeongeza kwa siku kumi muda wa kumalizika usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutokana na kuchelewa kwa link ya mfumo mpya wa usajili (system) kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Kwa mujibu wa CAF, link hiyo itakuwa tayari kwa matumizi ndani ya siku tatu zijazo kutokana sasa. Hivyo, mameneja wa usajili wa timu hizo kwa sasa wanatakiwa kukamilisha nyaraka zote zinazotakiwa ili link hiyo itakapokuwa tayari waweze kuingiza usajili wao mara moja.

Kuanzia msimu wa 2014/2015 mfumo unaotumika kwa usajili kwa klabu hizo ni wa elektroniki badala ya ule wa zamani wa kutumia fomu za kawaida. Mfumo huo wa kisasa ambao pia unatumiwa na CAF unaondoa upungufu uliokuwepo katika mfumo wa zamani.

Kutokana na mabadiliko hayo, usajili sasa utamalizika Agosti 27 mwaka huu badala ya leo (Agosti 17 mwaka huu). Kipindi cha pingamizi ni kuanzia Agosti 28 mwaka huu hadi Septemba 3 mwaka huu.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itakutana kati ya Septemba 6 na 8 mwaka huu kwa ajili ya kupitia pingamizi na kuthibitisha usajili.

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoshirikisha timu 14 itaanza Septemba 20 mwaka huu wakati ratiba inatarajia kutoka mwezi mmoja kabla ya kuanza ligi hiyo. Ligi Daraja la Kwanza inatarajia kuanza wiki ya kwanza ya Oktoba.

Mwisho wa kuombewa Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wanatoka nje ya Tanzania ni Septemba 6 mwaka huu.

Sunday, August 17, 2014

SHILLA NDIYE MISS KINONDONI 2014


Redd's Miss Kinondoni 2014, Maria Shila akipunga mkono baada ya kutawazwa kuwa malkia wa Kanda ya Kinondoni katika shindano lililoshirikisha wanyange 16 waliokuwa wakiwania tiketi ya kushiriki shindano la Miss Tanzania 2014. Shindano hilo lilifanyika Dar es Salaam usiku wa kuamia leo.

Shila ameungana na warembo wengine Camila Cindy John aliyeshika nafasi ya pili na Queenlatifa Hashim aliyeshika nafasi ya tatu ambao kwa pamoja wamepata tiketi ya kuiwakilisha Kanda ya Kinondoni katika mashindano ya taifa ya Miss Tanzania 2014 yanayotaraji kufanyika mapema mwezi Oktoba.


Redd's Miss Kinondoni 2014, Maria Shila (katikati) akipunga mkono baada ya kutangazwa kuwa ndie mshindi wa taji hilo na kuwaongoza warembo wengine 15 waliokuwa wakiwania taji hilo. Wengine mshindi wa pili Camila Cindy John (kulia) na mshindi wa tatu Queenlatifa Hasim. Shindano hilo lilifanyika Dar es Salaam usiku wa kuamia leo.

MANYAMA AMWAGA WINO YANGA MIAKA MIWILI



Mlinzi wa kushoto wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Andrew Charles Manyama kutoka timu ya JKT Ruvu Stars leo amesaini mkataba wa miaka miwili (2) tayari kwa kuitumikia timu ya Young Africans SC kuanzia msimu huu wa 2014/2015.

Andrew Charles Manyama beki wa kushoto wa timu ya Taifa Tanzania amekamilisha taratibu zote kutoka katika timu yake ya JKT Ruvu leo mchana na sasa kuanzia kesho ataonekana katika mazoezi ya kikosi cha kocha mkuu Marcio Maximo tayari kwa mikikimikiki ya VPL msimu huu.

Usajili wa Manyama unafanya idadi ya wachezaji wapya msimu huu kufikia watano (5) wakiwemo washambuliaji wabrazil Andrey Coutinho, Geilson Santos "Jaja", Kiungo mkabaji Said Juma "Makapu" na mlinzi wa kati Pato Ngonyani.

Friday, August 15, 2014

MWAMEJA, NSAJIGWA, PAWASA, LUNYAMILA KUUNDA KIKOSI CHA TANZANIA ALL STARS KITAKACHOMENYANA NA REAL MADRID






 NYOTA kadhaa maarufu wa zamani wa soka nchini, wameitwa kwenye kikosi cha Tanzania All Stars Veterans, kitakachomenyana na wanasoka wa zamani wa klabu ya Real Madrid ya Hispania.

Pambano hilo la aina yake na linalosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini, limepangwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Miongoni mwa nyota hao ni makipa Mwameja Mohamed na Manyika Peter na mebeki Nsajigwa Shadrack, Mecky Mexime, Boniface Pawasa, John Mwansasu, Abubakar Kombo, George Masatu na Habib Kondo.

Viungo ni Suleiman Matola, Shaaban Ramadhani, Salvatory Edward, Sabri Ramadhani ‘China’, Yussuf Macho, Abdul Mashine, Abdul Maneno, Mao Mkami, Steven Nyenge, Madaraka Suleiman, Akida Makunda na Mtwa Kihwelo.

Washambuliaji ni Monja Liseki, Iddi Moshi, Dua Said, Emmanuel Gabriel, Said Maulid, Thomas Kipese, Nasor Mwinyi ‘Bwanga’, Edibilly Lunyamila, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Clement Kahabuka, Madaraka Suleiman na Akida Makunda.

Kikosi hicho kitakuwa chini ya makocha Charles Boniface Mkwasa na wasaidizi wake ni Freddy Felix Minziro na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’. Daktari wa timu hiyo atakuwa Mwanandi Mwankemwa na viongozi ni Mtemi Ramadhani, Hassan Mnyenye, Omar Gumbo na Hamisi Kisiwa.

Kikosi cha Real Madrid kilichosheheni nyota mbalimbali waliowahi kung'ara katika ligi kuu ya Hispania, kinatarajiwa kutua nchini Agosti 22 mwaka huu, kikiwa na kina Luis Figo, Zinedine Zidane, Claude Makelele na wengine.

Mbali na kucheza mechi hiyo ya kirafiki, kikosi hicho kinatarajiwa kufanya ziara ya kiutalii katika vivutio mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupanda Mlima Kilimanjaro.

Real Madrid inakuja nchini kwa mwaliko wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini ya Mkurugenzi wake Mkuu, Farough Baghozah.

PHIRI AMWAGA WINO SIMBA MWAKA MMOJA, KIKOSI CHAPELEKWA MAFICHONI ZANZIBAR


KOCHA Mkuu mpya wa Simba, Patrick Phiri kutoka Zambia (kulia) akibadilishana hati za mkataba wake na Rais wa Simba, Evance Aveva katika hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Regency mjini Dar es Salaam jana. Phiri ametia saini mkataba wa kuifundisha Simba kwa mwaka mmoja. (Picha kwa hisani ya Blogu ya BINZUBEIRY)

KIKOSI cha Simba kinaondoka mjini Dar es Salaam leo kwenda Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara.

Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa, kikosi hicho kitakwenda Zanzibar kikiwa chini ya kocha wake mpya, Patrick Phiri na kitarejea Dar es Salaam siku chache kabla ya kuanza kwa ligi.

Ratiba ya ligi kuu inaonyesha kuwa, michuano hiyo imepangwa kuanza Septemba 20 mwaka huu, ikitanguliwa na mechi ya kuwania Ngao ya Jamii kati ya mabingwa Azam na washindi wa pili, Yanga.

Mmoja wa viongozi wa kamati ya utendaji ya Simba, alisema jana kuwa tayari klabu hiyo imeshakamilisha usajili wa wachezaji wake, wakiwemo watano kutoka nje ya nchi.

Phiri amerejea nchini kurithi mikoba ya kocha wa zamani wa timu hiyo, Zdravko Logarusic, ambaye mkataba wake ulivunjwa wiki iliyopita kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.

Hadi sasa mkataba wa Phiri umefanywa kuwa siri, lakini kuna habari kuwa kocha huyo atakuwa akilipwa zaidi ya dola 5,000 za Marekani kwa mwezi, kiwango ambacho alikuwa akilipwa kwa mara ya mwisho alipokuwa akiifundisha timu hiyo miaka minne iliyopita.

Phiri aliwahi kufanyakazi kwa awamu tatu tofauti kuanzia 2004 hadi 2010, ikiwa ni pamoja na kuiwezesha kutwaa mataji mawili ya ligi kuu na Kombe la Tusker. Kocha huyo ndiye aliyeiwezesha Simba kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu wa 2009/2010 bila kupoteza mechi.

Thursday, August 14, 2014

TFF YAKIRI BASI LAKE KUKAMATWA NA MADALALI KWA DENI LA MIL. 140/-


Basi la Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekamatwa na madalali kwa amri ya mahakama kutokana na deni la sh milioni 140 ambalo tunadaiwa hadi litakapolipwa.

Amri hiyo imetokana na deni hilo la kampuni ya Punchline ya Kenya iliyokuwa ikichapa tiketi za kuingilia uwanjani kuanzia mwaka 2007. Hadi sasa tumeshalipa sh. milioni 70 katika deni hilo.

Jitihada zinafanyika ili kumaliza deni hilo. Pia tunachunguza mwenendo mzima uliosababisha kuwepo deni hilo.

CAF YAZUIA MECHI ZAKE KUPISHA EBOLA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limezuia mechi zake kuchezwa Guinea, Liberia na Sierra Leone kutokana na kuripotiwa kuwepo kwa wagonjwa wengi wa Ebola katika nchi hizo.

Ikiwa ni njia mojawapo ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya ugonjwa huo kupitia mkusanyiko wa watu, CAF imevitaka vyama vya mpira wa miguu vya nchi hizo kuchagua viwanja vingine huru kwa ajili ya timu zao zinazoshiriki michuano yake kwa kipindi hiki hadi katikati ya mwezi ujao.

CAF itafanya tathmini nyingine kuhusiana na ugonjwa huo kuanzia katikati ya Septemba ili kuona kama nchi hizo zinaweza kupokea timu ngeni kwa ajili ya mechi mbalimbali za michuano yake, na baadaye kufanya uamuzi wa kuruhusu au kuendelea kusimamisha.

Pia kutokana na mapendekezo ya Shirika la Afya Duniani (WHO), CAF imesema kwa nchi zenye virusi vya Ebola ni muhimu kwa vyama vyake vya mpira wa miguu kuufanyia vipimo vya afya msafara wa timu zao ili kuhakikisha wenye virusi vya ugonjwa huo hawasafiri.

ELIZABETH NDIYE MISS KANDA YA MASHARIKI 2014


Mshindi wa Taji la Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2014, Elizabeth Tarimo (18) ambaye pia ni Miss Lindi, akiwa mwenye uso wa furaha na tabasamu la ushindi sambamba na mshindi wa pili, Nidah Katunzi (19) ( kulia), ambaye ni Miss Mtwara pamoja na wa tatu, Lucy Julius Diyu (21), Miss Morogoro baada ya kutangazwa kuwa washindi kwenye nafasi hizo wakati wa kinya’ganyiro cha
kuwania taji hilo kilichofanyika juzi usiku kwenye ukumbi wa Hoteli ya Nashera ya mjini Morogoro.

Wednesday, August 13, 2014

REAL MADRID BINGWA KOMBE LA SUPER


MABAO yaliyofungwa na mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo juzi yaliiwezesha Real Madrid kutwaa Kombe la Super la Ulaya baada ya kuichapa Sevilla mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Cardiff City.

Ronaldo alifunga bao la kwanza dakika ya 30 kabla ya kuongeza la pili dakika ya 49 kutokana na pasi maridhawa kutoka kwa Gareth Bale, aliyekuwa akicheza kwenye ardhi ya nyumbani.

Wakati huo huo, Chelsea juzi iliichapa Real Sociedad ya Hispania mabao 2-0 karika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Mshambuliaji mpya wa Chelsea, Diego Costa aliibuka nyota wa Chelsea baada ya kuifungia mabao yote mawili.

ROONEY NAHODHA MPYA MAN UTD


KOCHA Mkuu wa Manchester United, Louis van Gaal, amemteua mshambuliaji nyota wa timu hiyo, Wayne Rooney kuwa nahodha mpya.

Van Gaal amemteua Rooney kushika wadhifa huo kutokana na kuvutiwa na kiwango chake cha soka tangu alipoanza kuinoa timu hiyo mwezi uliopita.

Kocha huyo raia wa Uholanzi amesema, siku zote kwake, chaguo muhimu ni nahodha wa timu na kwamba anaamini, Rooney atakuwa kiongozi mzuri wa wachezaji wenzake.

Wakati huo huo, Van Gaal ameendelea kuwapa raha mashabiki wa Manchester United, baada ya kuiongoza timu hiyo kuichapa Valencia ya Hispania mabao 2-1.

Mabao ya Manchester United yalipachikwa wavuni Darren Fletcher dakika ya 49 na Marouane Fellani aliyefunga bao l;a ushindi dakika ya 90.

Bao la Valencia lilipachikwa wavuni na Rodrigo, ikiwa ni dakika chache baada ya Rooney kukosa penalti baada ya shuti lake kuokolewa na kipa Diego Alves.

TFF HAITAMBUI MABADILIKO YA UONGOZI COASTAL UNION


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) halitambui mabadiliko ya uongozi ndani ya Coastal Union yanayodaiwa kufanywa na mkutano wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika hivi karibuni.

Uongozi wa Coastal Union uliochaguliwa na mkutano wa uchaguzi wa klabu hiyo ndiyo ambao tunautambua, na tutaendelea kufanya nao kazi, na sio uongozi mwingine wowote ule.

Tunapenda kuwakumbusha wanachama wetu (ikiwemo Coastal Union) kuheshimu katiba ya TFF pamoja na katiba zao, kwani hazitambui mapinduzi ya uongozi wala kamati za muda za utendaji. TFF inafanya kazi za kamati za utendaji zilizopatikana kwa njia ya uchaguzi tu.

Tayari tumepokea barua kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mnguto ikilalamikia kusimamishwa kwake.

Hivyo, tunafuatilia suala hilo kwa kina, na ikibainika kuwa kuna viongozi wamehusika katika mapinduzi hayo watafikishwa katika vyombo husika kwa hatua zaidi.

Tuesday, August 12, 2014

USAJILI LIGI KUU ENGLAND (LATEST),NANI KAINGIA NANI KATOKA


ARSENAL
WALIOSAJILIWA
Alexis Sanchez (Barcelona, £30m),
Calum Chambers (Southampton, £12m),
Mathieu Debuchy (Newcastle, £10m),
David Ospina (Nice, £3m)

WALIOONDOKA
Thomas Vermaelen (Barcelona, £15m),
Thomas Eisfeld (Fulham, undisclosed),
Bacary Sagna (Manchester City, free),
Lukasz Fabianski (Swansea, free),
Nicklas Bendtner (released),
Park Chu-young (released),
Chuks Aneke (released),
Daniel Boateng (released),
Wellington Silva (Almeria, loan),
Carl Jenkinson (West Ham, loan),
Benik Afobe (MK Dons, loan)

ASTON VILLA
WALIOSAJILIWA
Philippe Senderos (Fulham, free),
Joe Cole (West Ham, free),
Tom Leggett (Southampton, undisclosed),
Isaac Nehemie (Southampton, undisclosed),
Kieran Richardson (Fulham, undisclosed),
Aly Cissokho (Valencia, £2m)

WALIOONDOKA
Marc Albrighton (Leicester City, free),
Nathan Delfouneso (Blackpool, free),
Jordan Bowery (Rotherham, undisclosed),
Samir Carruthers (MK Dons, undisclosed),
Nicklas Helenius (Aalborg, loan),
Yacouba Sylla (Kayseri Erciyesspor, loan),
Jed Steer (Doncaster Rovers, loan),
Antonio Luna (Hellas Verona, loan)

BURNLEY
WALIOSAJILIWA
Lukas Jutkiewicz (Middlesbrough, £2.5m),
Michael Kightly (Stoke, undisclosed),
Marvin Sordell (Bolton, free),
Matt Gilks (Blackpool, free),
Matt Taylor (West Ham, free),
Steven Reid (West Brom, free)

WALIOONDOKA
Chris Baird (West Brom, free),
Junior Stanislas (Bournemouth, free),
David Edgar (Birmingham, free),
Keith Treacy (released),
Brian Stock (released),
Nick Liversedge (released)

CHELSEA
WALIOSAJILIWA
Cesc Fabregas (Barcelona, £30m),
Diego Costa (Atletico Mdrid, £32m),
Mario Pasalic (Hadjuk Split, undisclosed),
Filipe Luis (Atletico, £16m),
Didier Drogba (Galatasaray, free)

WALIOONDOKA
David Luiz (Paris Saint-Germain, £50m),
Romelu Lukaku (Everton, £28million),
Samuel Eto'o (released),
Frank Lampard (New York City, free),
Sam Hutchinson (Sheffield Wednesday, free),
Mark Schwarzer (released),
Henrique Hilario (released),
Wallace (Vitesse Arnhem, loan),
Bertrand Traore (Vitesse Arnhem, loan)
Thorgan Hazard (Borussia Monchengladbach, loan),
Ashley Cole (Roma, £1.5m),
Demba Ba (Besiktas, £8m),
Mario Pasalic (Elche, loan)
Patrick van Aanholt (Sunderland, undisclosed),
Ryan Bertrand (Southampton, loan),
Gael Kakuta (Rayo Vallecano, loan),
John Swift (Rotherham, loan),
Oriol Romeu (Valencia, loan)

CRYSTAL PALACE
WALIOSAJILIWA
Chris Kettings (Blackpool, free)
Fraizer Campbell (Cardiff, £800,000),
Brede Hangeland (Fulham, free)

WALIOONDOKA
Jonathan Parr (Ipswich, free),
Dean Moxey (Bolton, free),
Aaron Wilbraham (Bristol City, free),
Kagisho Dikgacoi (Cardiff, free),
Danny Gabbidon (released),
Neil Alexander (released),
Ibra Sekajja (released),
Alex Wynter (Portsmouth, loan),
Kwesi Appiah (Cambridge, loan),
Jose Campana (Sampdoria, undisclosed),
Jack Hunt (Nottingham Forest, loan),
Stephen Dobbie (Fleetwood, loan)

EVERTON
WALIOSAJILIWA
Romelu Lukaku (Chelsea, £28m),
Gareth Barry (Manchester City, free),
Muhamed Besic (Ferencvaros, £4m),
Brendan Galloway (MK Dons, Undisclosed)

WALIOONDOKA
Apostolos Vellios, (Lierse, free)
Mason Springthorpe (released)
Magaye Gueye (Millwall, free)

HULL
WALIOSAJILIWA
Robert Snodgrass (Norwich, £8m),
Jake Livermore (Tottenham, £6m),
Tom Ince (Blackpool, free),
Harry Maguire (Sheffield United, £2.5m),
Andrew Robertson (Dundee United, £2.85m)

WALIOONDOKA
Matty Fryatt (Nottingham Forest, free),
Cameron Stewart (Ipswich, free),
Nick Proschwitz (Brentford, free),
Robert Koren (released),
Abdoulaye Faye (released),
Conor Henderson (Crawley, free),
Dougie Wilson (released),
Conor Townsend (Dundee United, loan),
Joe Dudgeon (Barnsley, loan)

LEICESTER CITY
WALIOSAJILIWA
Matthew Upson (Brighton, free),
Marc Albrighton (Aston Villa, free),
Leonardo Ulloa (Brighton, £7m),
Ben Hamer (Charlton, free),
Jack Barmby (Manchester United, free),
Louis Rowley (Manchester United, free)

WALIOONDOKA
Lloyd Dyer (Watford, free),
Neil Danns (Bolton, free),
Sean St Ledger (released),
Zak Whitbread (Derby, free),
Paul Gallagher (Preston, loan),
Marko Futacs (released),
George Taft (Burton Albion, free)

LIVERPOOL
WALIOSAJILIWA
Adam Lallana (Southampton, £23m),
Lazar Markovic (Benfica, £20m),
Emre Can (Bayer Leverkusen, £9.8m),
Rickie Lambert (Southampton, £4m),
Dejan Lovren (Southampton, £20m),
Divock Origi (Lille, £10m),
Javier Manquillo (Atletico Madrid, loan)

WALIOONDOKA
Luis Suarez (Barcelona, £75m),
Pepe Reina (Bayern Munich £2m),
Conor Coady (Huddersfield, £500,000),
Luis Alberto (Malaga, loan),
Iago Aspas (Sevilla, loan),
Andre Wisdom (West Brom, loan),
Divock Origi (Lille, loan),
Brad Smith (Swindon, loan)

MANCHESTER CITY
WALIOSAJILIWA
Eliaquim Mangala (Porto, £32million),
Fernando (Porto, £12m),
Willy Caballero (Malaga, £6m),
Bruno Zuculini (Racing Club, £3m),
Bacary Sagna (Arsenal, free),
Frank Lampard (New York City, loan)

WALIOONDOKA
Costel Pantilimon (Sunderland, free),
Joleon Lescott (West Brom, free)
Gareth Barry (Everton, free),
Alex Nimely (released),
Rony Lopes (Lille, loan),
Emyr Huws (Wigan, loan),
Reece Wabara (Doncaster Rovers, free),
Jack Rodwell (Sunderland, £7m)

MANCHESTER UNITED
WALIOSAJILIWA
Luke Shaw (Southampton, £31.5m),
Ander Herrera (Athletic Bilbao, £29m),
Vanja Milinkovic (FK Vojvodina, undisclosed)

WALIOONDOKA
Alexander Buttner (Dinamo Moscow, £5.6m),
Rio Ferdinand (QPR, free),
Nemanja Vidic (Inter Milan, free),
Federico Macheda (Cardiff City, free),
Jack Barmby (Leicester, free),
Louis Rowley (Leicester, free)
Ryan Giggs (retired),
Patrice Evra (Juventus, £2.5m)
Bebe (Benfica, £2.4m)

NEWCASTLE
WALIOSAJILIWA
Remy Cabella (Montpellier, £12m),
Emmanuel Riviere (Monaco, £6m),
Siem de Jong (Ajax, £6m), Daryl Janmaat (Feyenoord, £5,m),
Jamaal Lascelles and Karl Darlow (Nottingham Forest, £7million -joint fee),
Ayoze Perez (Tenerife, £1.5m),
Jack Colback (Sunderland, free),
Facundo Ferreyra (Shakhtar Donetsk, loan)

WALIOONDOKA
Mathieu Debuchy (Arsenal, £10m),
James Tavernier (Wigan, undisclosed),
Dan Gosling (Bournemouth, free),
Shola Ameobi (released),
Conor Newton (Rotherham, free),
Michael Richardson (released),
Sylvain Marveaux (Guingamp, loan),
Jamaal Lascelles (Nottingham Forest, loan),
Karl Darlow (Nottingham Forest loan),
Adam Campbell (Fleetwood, loan)

QUEENS PARK RANGERS
WALIOSAJILIWA
Rio Ferdinand (Manchester United, free),
Steven Caukler (Cardiff, £8m),
Jordon Mutch (Cardiff, £6m),
Mauricio Isla (Juventus, loan)

WALIOONDOKA
Tom Hitchcock (Mk Dons, free),
Aaron Hughes (Brighton, free)
Stephane Mbia (released),
Andrew Johnson (released),
Luke Young (released),
Hogan Ephraim (released),
Angelo Balanta (released),
Yossi Benayoun (Maccabi Haifa, undisclosed),
Esteban Granero (Real Sociedad, undisclosed)

SOUTHAMPTON
WALIOSAJILIWA
Dusan Tadic (Twente, £10.3m),
Fraser Forster (Celtic, £10m),
Graziano Pelle (Feyenoord, £8m),
Ryan Bertrand (Chelsea, loan),
Saphir Taider (Inter Milan, loan)

WALIOONDOKA
Luke Shaw (Manchester United, £31.5m),
Adam Lallana (Liverpool, £23m),
Dejan Lovren (Liverpool, £20m),
Calum Chambers (Arsenal, £12m),
Rickie Lambert (Liverpool, £4m),
Tom Leggett (Aston Villa, undisclosed),
Isaac Nehemie (Aston Villa, undisclosed),
Guly do Prado (released),
Lee Barnard (Southend, free),
Jonathan Forte (Oldham, free),
Danny Fox (Nottingham Forest, free),
Andy Robinson (Bolton, free),
Dani Osvaldo (Inter Milan, loan)

STOKE
WALIOSAJILIWA
Mame Biram Diouf (Hannover, free),
Dionatan Teixeira (Banska Bystrica, undisclosed),
Phil Bardsley (Sunderland, free),
Steve Sidwell (Fulham, free),
Bojan Krkic (Barcelona, undisclosed)

WALIOONDOKA
Michael Kightly (Burnley, undisclosed),
Matthew Etherington (released),
Juan Agudelo (released)

SUNDERLAND
WALIOSAJILIWA
Jack Rodwell (Man City, £7m),
Patrick van Aanholt (Chelsea, undisclosed),
Billy Jones (West Brom, free),
Jordi Gomez (Wigan, free),
Costel Pantilimon (Manchester City, free),
Santiago Vergini (Estudiantes, loan)

WALIOONDOKA
Ignacio Scocco (Newell's, £800,000),
Jack Colback (Newcastle, free),
Craig Gardner (West Brom, free),
Phil Bardsley (Stoke, free),
Billy Knott (Bradford, free)
Keiren Westwood (Sheffield Wednesday, free),
Carlos Cuellar (released),
Andrea Dossena (released),
Louis Laing (released),
Oscar Ustari (Newell's, free),
David Vaughan (Nottingham Forest, free),
John Egan (Gillingham, free),
El Hadji Ba (Bastia, loan)

SWANSEA
WALIOSAJILIWA
Marvin Emnes (Middlesbrough, £1.5m),
Bafetimbi Gomis (Lyon, free),
Lukasz Fabianski (Arsenal, free),
Stephen Kingsley (Falkirk, undisclosed),
Gylfi Sigurdsson (Tottenham, swap)
Jefferson Montero (Monarcas Morelia, £4m)

WALIOONDOKA
Leroy Lita (released),
David Ngog (released),
Daniel Alfei (Northampton, loan),
Jernade Meade (released),
Darnel Situ (released),
Michu (Napoli, loan),
Ben Davies (Tottenham, £10m),
Michel Vorm (Tottenham, £5m)
Alejandro Pozuelo (Rayo Vallecano, undisclosed),
Leroy Lita (Barnsley, free),
Chico Flores (Lekhwiya, free)

TOTTENHAM
WALIOSAJILIWA
Ben Davies (Swansea, swap), Michel Vorm (Swansea, £5m),
Eric Dier (Sporting Lisbon, £4m)

WALIOONDOKA
Jake Livermore (Hull, £6m),
Gylfi Sigurdsson (Swansea, swap),
Iago Falque (Genoa, £4m)
Heurelho Gomes (Watford, free),
Cameron Lancaster (released),
Alex Pritchard (Brentford, loan), Shaquile Coulthirst (Southend, loan)

WEST BROMWICH ALBION
WALIOSAJILIWA
Brown Ideye (Dynamo Kiev, £10m),
Jason Davidson (Heracles, undisclosed),
Cristian Gamboa (Rosenborg, undisclosed),
Craig Gardner (Sunderland, free),
Joleon Lescott (Manchester City free),
Chris Baird (Burnley, free),
Sebastien Pocognoli (Hannover 96, undisclosed),
Andre Wisdom (Liverpool, loan)

WALIOONDOKA
Liam Ridgewell (Portland Timbers, free),
Billy Jones (Sunderland, free),
Steven Reid (Burnley, free),
Cameron Gayle (Shrewsbury, free),
Diego Lugano (released),
Zoltan Gera (released),
Scott Allan (released),
Nicolas Anelka (released),
George Thorne (Derby County, undisclosed)

WEST HAM
WALIOSAJILIWA
Enner Valencia (Pachuca, £12m), Cheikhou Kouyate (Anderlecht, £7m),
Mauro Zarate (Velez Sarsfield, undisclosed),
Aaron Cresswell (Ipswich, undisclosed),
Diego Poyet (Charlton, undisclosed),
Carl Jenkinson (Arsenal, home)

WALIOONDOKA
Joe Cole (Aston Villa, free),
Matt Taylor (Burnley, free),
Stephen Henderson (Charlton, free),
Jack Collison (released),
George McCartney (released),
Callum Driver (released),
Jordan Spence (released),
George Moncur (Colchester, free

Monday, August 11, 2014

LOGA ATUPIWA VIRAGO SIMBA, AMWITA AVEVA MBABAISHAJI



SIKU moja baada ya Simba kumtimua, kocha wa zamani wa timu hiyo, Zdravko Logarusic, ameibuka na kudai kuwa viongozi wa klabu hiyo ni wababaishaji.

Logarusic, raia wa Croatia alisema Simba imemfanyia mchezo mchafu kwa kumfukuza katika mazingira ya kutatanisha.

Kauli ya 'Loga' imekuja muda mfupi baada ya Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, kutangaza juzi Dar es Salaam kumtimua kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Logarusic, alisema alifahamu Simba itamfukuza kazi muda si mrefu kwa kuwa haikuwa ikimuhitaji.

Logarusic alisema alianza kutofautiana na uongozi, baada ya kukataa kufuata baadhi ya mambo ambayo walitaka afanye kinyume na utaratibu wake wa kazi.

Kocha huyo alisema baada ya msuguano huo, aliamua kufuata walichokuwa wakitaka na hatua ilichangia kutimiza malengo.

Alisema amekuwa na msuguano wa chini kwa chini na uongozi tangu ulipoingia madarakani naalitarajia asingeweza kufanya nao kazi.

Alisema amefukuzwa kazi kihuni bila kufuata utaratibu na waliamua kumpa mkataba mbovu usiokuwa na tija kwa upande wake ili wamdhulumu haki zake.

"Mwezi mmoja uliopita walinipa mkataba uliosema yeyote atakayevunja atamlipa mwenzake mshahara wa mwezi mmoja lakini mkataba huo nilijua siwezi kuutumikia," alisema Logarusic.

Alisema licha ya kufukuzwa hana hofu kwa kuwa anaamini ni kocha bora ambaye anayejua vyema misingi ya kazi yake, hivyo atapata kibarua kingine na maisha yataendelea.

Logarusic alisema anasubiri alipwe haki yake na kupata tiketi ili aondoke nchini kwenda kutafuta kibarua sehemu nyingine.

Hata hivyo alisema huenda akarejea nchini Kenya kuinoa Gor Mahia ambayo imemuita kwa mazungumzo ya kupewa kazi. Kochwa Gor Mahia Bobby Williamson ameteuliwa kuinoa timu ya taifa 'Harambee Stars'.

Awali, Aveva alisema kocha huyo amekuwa akionywa mara kwa mara lakini amekuwa mkaidi na kushindwa kujirekebisha jambo ambalo uongozi umeshindwa kuivumilia.

Kocha huyo alitwaa mikoba ya Abdallah 'King' Kibadeni, aliyetimuliwa muda mfupi kabla ya ligi hiyo kumalizika msimu uliopita.

Sunday, August 10, 2014

ZESCO YATIBUA SHEREHE ZA SIMBA DAY, MNYAMA APIGWA 3-0








TIMU ya soka ya Zesco ya Zambia jana ilitibua sherehe za Simba Day baada ya kuwalaza mabingwa

hao wa zamani nchini mabao 3-0 katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.

Simba ilitumia mechi hiyo kuwatambulisha wachezaji wake wapya, inayotarajia kuwasajili kwa ajili ya
msimu ujao wa ligi kuu.

Hata hivyo, maelfu ya mashabiki wa Simba waliofurika kwenye uwanja huo kuanzia saa nane mchana,
walijikuta wakigeuka mabubu baada ya kuishuhudia timu yao ikicheza soka ya kiwango cha chini na
kukubali kipigo hicho kikubwa.

Baadhi ya nyota wapya wa Simba waliocheza mechi hiyo ni pamoja na Paul Kiongera kutoka Kenya na Kwizera kutoka Burundi. Wakati Kwizera alionyesha uhai kwenye safu ya kiungo, Kiongera alishindwa kuonyesha makeke yake katika ushambuliaji.

Iliwachukua Zesco dakika 14 kuhesabu bao la kwanza lililofungwa bna Jacskon Mwanza, aliyeunganisha  wavuni kwa kichwa krosi kutoka kwa Justine Zulu, aliyemlamba chenga beki Donald Musoti wa Simba kutoka pembeni ya uwanja. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

Simba ilikianza kipindi cha pili kwa kufanya mabadiliko ya wachezaji wa tano baada ya awali, Haruna
Chanongo kuchukua nafasi ya Ramadhani Singano.

Bao la pili la Zesco lilifungwa kwa njia ya penalti na Clatoos Chane dakika ya 64 baada ya kuangushwa ndani ya eneo la hatari na beki Musoti wa Simba.

Simba ilipata nafasi kadhaa nzuri za kufunga mabao katika kipindi cha kwanza, lakini zilipotezwa na
washambuliaji wake, Hamisi Tambwe, Singano na Kiongera.

Bao la tatu la Zambia lililowavunja nguvu kabisa mashabiki wa Simba lilifungwa na Mayban Mwamba
dakika za lala salama baada ya kupokea pasi kutoka kwa Ziniselemi Moyo.

Kabla ya pambano hilo, kulikuwepo na burudani mbalimbali za muziki kutoka kwa bendi ya Twanga
Pepeta International na wasanii Barnabas na Dully Sykes.

Wednesday, August 6, 2014

YANGA YAIGEUZIA KIBAO CECAFA


UONGOZI wa klabu ya Young Africans leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu na kusema kilichofanywa na waandaji wa michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuiondoa timu isishiriki ni cha kushangaza sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.

Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema walipata barua ya mwaliko wa kushiriki mashindano tarehe 25/7/2014 na kudhibitisha kushiriki michuano hiyo kwa kuandika barua iliyokwenda TFF na kisha wao kuiwasilisha kwa CECAFA.

Katibu wa Yanga SC, Benno Njovu kushoto akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari leo. Kulia ni kocha Marcio Marcio Maximo.

"Baada ya kudhibitisha kushiriki michuano hiyo tuliambiwa na CECAFA tutume orodha ya wachezaji na viongozi ambao watasafiri kuelekea nchini Rwanda kwenye michuano hiyo ili waweze kuandaa tiketi za ndege na sehemu ya malazi kitu ambacho tulitimiza" alisema Beno.

Lakini katika hali ya kushangaza jana tulipokea barua kutoka TFF ikisema CECAFA imetuondoa kwenye mashindano hayo kwa kushindwa kukidhi vigezo na kuiteua timu ya Azam kuchukua nafasi yetu "aliongeza Beno."

Kanuni za CECAFA zipo wazi kuwa wachezaji wanaopaswa kushiriki michuano hiyo ni lazima wawe na leseni za kucheza mpira kutoka kwa chama husika, jambo ambalo ambalo orodha tuliyowapelekea wachezaji wote wataichezea Yanga msimu huu wa 2014/2015.

Kocha Marcio Maximo alianza maandalizi ya kikosi ambacho kingekwenda kushiriki michuano hiyo ambayo ilipaswa kuanza ijumaa tarehe 8/8/2014 kwa Yanga kufungua dimba la wenyeji timu ya Rayon FC .

Kikosi ambacho kocha mkuu alikichagua kwenda kwenye michuano ya Kagame kilikua na jumla ya wachezaji 20, 15 wakiwa kutoka timu ya kikosi cha wakubwa na wachezaji watano wakitoka kikosi cha pili U20 chini ya kocha Leonado Neiva ambaye amekua na wachezaji hao kwa takribani mwezi mmoja.

Lakini walichokiamua CECAFA ni kuiondoa klabu ya Yanga na kuipa nafasi timu nyingine kwa kusema kikosi kilichopelekwa hawakubaliani nacho na hata kocha mkuu Marcio Maximo haendi, hao ndo tulipojua ya kuwa wanataka majina ya watu na sio timu.

Zifuatazo ni sababu za Kiufundi ambazo Yanga ilizipelekea CECAFA kuhusu kikosi hicho kutojumuisha wachezaji wa timu za Taifa.

a) Ripoti ya kocha aliyeondoka Yanga msimu uliopita Hans ilitoa maelekezo ya kupunguza wachezaji tisa (9) na wachezaji wawili kujiunga na klabu ya Azam hivyo kufanya kikosi kupungua wachezaji 11 kutoka katika idadi ya wachezaji 30 wa msimu uliopita.

b) Wachezaji 10 wa Yanga wamekuwa na majukumu ya timu za Taifa za Tanzania (Taifa Stars), Rwanda na Uganda tangu Aprili 19, 2014 mpaka mwanzoni mwa Agosti, takribani miezi mitatu wamekuwa kambini bila kupata muda wa kupumzika.

c) Benchi la Ufundi la Yanga ni jipya kuanzia kocha mkuu Maximo na wasaidizi wake watatu Leonardo Neiva, Salavatory Edwarda na Shadrack Nsajigwa hivyo wanahitaji muda wa kuwajua wachezaji waliokuwa kwenye timu ya Taifa ndo maana hawakuwajumuisha kwenye kikosi cha kwenda Kigali Rwanda.

d) Baadhi ya wachezaji wanahitaji Vibali vya kufanyia kazi nchini, uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili waweza kushiriki michuano ya Kagame, na moja ya kanuni za CECAFA mchezaji anayeshiriki mashindano hayo ni lazima awe na leseni ya kucheza mpira kwa ligi ya ndani.

e) Katika wachezaji 20 waliochaguliwa kushiriki michuano ya Kagame, wachezaji 6 wamepandishwa moja moja katika kikosi cha wakubwa msimu huu hivyo kufanya idadi ya wachezaji wa U20 kuwa watano tu.

f) Wachezaji walikokuwa kambini Taifa Stars kwa takribani miezi mitatu bila ya kupumzika, daktari alipendekeza wapate japo siku kumi na nne (14) za kupumzika ili miili yao iweze kupoa na kuanza upya tena maandalizi ya msimu mpya.

g) Yangga tunaamini hakuna mtu yoyote zaidi ya Kocha Mkuu anayeweza kutupangia kikosi cha kwanza, sababu yeye ndio anayekaa na wachezaji mda wote na kujua ubora wa wachezaji wake.

Tuesday, August 5, 2014

YANGA YAPIGWA CHINI KOMBE LA KAGAME, AZAM YACHUKUA NAFASI


Azam FC ndiyo itakayoiwakilisha Tanzania Bara kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) iliyopangwa kuanza Agosti 8 mwaka huu jijini Kigali, Rwanda.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeiteua Azam kuiwakilisha Tanzania Bara katika michuano hiyo baada ya waandaaji wake, Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuamua kuindoa Yanga iliyokuwa icheze awali.

CECAFA imesema baada ya majadiliano na Yanga kupitia TFF, klabu hiyo ilipewa muda hadi jana (Agosti 4 mwaka huu) iwe imetekeleza matakwa ya kikanuni ili iruhusiwe kushiriki michuano hiyo lakini haikufanya hivyo.

Yanga iliwasilisha orodha ya wachezaji wengi wa kikosi cha pili kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo, jambo ambalo limekatawaliwa na CECAFA kwa vile linakwenda kinyume na kanuni za michuano hiyo.

Azam FC ambayo ilishika nafasi ya pili- nyuma ya Yanga katika ligi iliyopita msimu wa 2012/2013 imekubali kushiriki michuano hiyo na inatarajia kuondoka nchini kesho (Agosti 6 mwaka huu) kwenda Kigali.

Msafara wa Azam FC katika michuano hiyo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, James Mhagama.

RAMBIRAMBI MSIBA WA MAKAMU WA RAIS FIFA.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Shrikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Sepp Blatter kutokana na kifo cha makamu wake mwandamizi Julio Grondora.

Amesema yeye binafsi na jamii ya mpira wa miguu Tanzania kwa ujumla wanaomboleza msiba wa Grondora ambaye pia alikuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Argentina (AFA).

Ameongeza kuwa Grondora alikuwa mtumishi mwandamizi wa mpira wa miguu, kwani alijitoa katika kuutumikia mpira wa miguu, na mchango wake katika maendeleo ya mchezo huo utaendelea kukumbukwa wakati wote.

Rais Malinzi amesema familia ya mpira wa miguu nchini Argentina imepata pigo, na ametoa pole kwa familia ya marehemu, AFA na familia nzima ya FIFA na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina.

KLABU VPL, FDL ZATAKIWA KUWASILISHA MABENCHI YA UFUNDI
Klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zinatakiwa kuwasilisha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) orodha ya watendaji wa mabenchi yao ya ufundi yakiongozwa na Kocha Mkuu.

Ni wajibu wa klabu kuhakikisha zinatekeleza maagizo hayo kwani ni matakwa ya Kanuni za VPL na zile za FDL.

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara itaanza kutimua vumbi Septemba 20 mwaka huu wakati ile ya FDL inatarajia kuanza Oktoba mwaka huu.

WACHEZAJI, VIONGOZI SIMBA WATEMBELEA TBL LEO






TAMASHA LA MATUMAINI


TAMASHA LA MATUMAINI