KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, August 8, 2011

Yanga yachapwa 3-1 na El-Hilal



Timu ya Yanga ya Jangwani ambayo iliondoka Jumamosi kuelekea nchini Sudan kwa mwaliko wa michezo ya kirafiki na timu ya Al- Hilal ya huko, jana ilibanjuliwa mabao 3-1.


Aliyepatia Yanga bao la kufutia machozi ni mganda, Hamis Kiiza. Timu hiyo itashuka dimbani tena kesho kumenyana na timu ya El- Mereikh ya huko na baada ya hapo, itarejea nyumbani kwa ajili ya mchezo wao wa kuwania ngao ya Hisani dhidi ya watani wao wa jadi Simba.


El-Mereikh ilishiriki katika Kombe la Kagame Castle mwezi uliopita nchini Tanzania na kushika nafasi ya tatu huku Yanga wakichukua ubingwa huo. Katika mchezo wa makundi wa michuano hiyo, timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.

No comments:

Post a Comment