KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, December 26, 2016

YANGA YABANWA MBAVU NA AFRICAN LYON



MABINGWA watetezi Yanga jana walilazimishwa kutoka sare ya bao 1-1 na African Lyon katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Sare hiyo imeifanya Yanga iendelee kukamata nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo, ikiwa na pointi 37 baada ya kucheza mechi 17, sawa na Simba inayoongoza kwa kuwa na pointi 38.

Matokeo hayo yalipokelewa kwa hasira na mashabiki wa Yanga, kufuatia wachezaji wa timu hiyo kugomea mazoezi kwa siku mbili mfululizo, wakishinikiza kulipwa mshahara wa mwezi Novemba.

Timu ya timu zote mbili kushambuliana kwa zamu katika kipindi cha kwanza, hadi kilipomalizika hakuna iliyoweza kupata bao.

Lyon ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 67, lililofungwa na Ludovic Venance baada ya kupokea pasi kutoka kwa Abdalla Mguhi.

Bao hilo halikudumu kwa muda mrefu, kwani Yanga ilifanikiwa kusawazisha dakika ya 74, kupitia kwa Amisi Tambwe, aliyemalizia krosi ya Juma Abdul.

No comments:

Post a Comment