KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, August 9, 2016

SIMBA YAWAPA RAHA MASHABIKI WAKE



TIMU ya soka ya Simba jana iliwapa raha mashabiki wake baada ya kuichapa AFC Leopards ya Kenya mabao 4-0 katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi hiyo iliyohudhuriwa na mashabiki lukuki, ilikuwa maalumu kwa ajili ya kupamba tamasha la maadhimisho ya miaka 80 ya klabu ya Simba.

Simba pia ilitumia mechi hiyo kuwatambulisha nyota wake kadhaa wapya, waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao wa ligi, akiwemo Shiza Kichuya, Pauk Kiongera na Laudit Mavugo.

Bao la kwanza la Simba lilifungwa na Ibrahim Ajib dakika ya 38 kwa shuti kali lililomshinda kipa wa AFC Leopards. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

Dakika 11 baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, Ajib aliiongezea Simba bao la pili kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Kichuya.

Bao la tatu lilifungwa na Kichuya dakika ya 66, akiunganisha wavuni pasi kutoka kwa Blagnen kabla ya Mavugo kuongeza la nne dakika ya 81.

No comments:

Post a Comment