KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, August 22, 2016

SAMATTA AENDELEA KUNG'ARA UBELGIJI



MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta  amefunga mabao mawili timu yake, KRC Genk ya Ubelgiji ikishinda 3-0 dhidi ya wenyeji, Lokeren Uwanja wa Daknamstadion mjini Lokeren
katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.


Samatta alifunga mabao yote mawili ya mwanzo, la kwanza dakika ya 34 na la pili dakika ya 38, yote akisetiwa na kiungo kutoka Hispania, Alejandro Pozuelo Melero aliyemsetia pia Mjamaica Leon Bailey
kufunga la tatu dakika ya 48.

No comments:

Post a Comment