KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, August 16, 2016

MALINZI AUKWAA TENA UENYEKITI WA SOKA KAGERA


Na Mwandishi Wetu, Bukoba

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, juzi, alichaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Kagera (KRFA), baada ya kupata kura 21 kati ya 22.

Katika uchaguzi huo uliofanyika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Optima, Bananzi, wilayani Misenyi, Salum Chama alitetea nafasi yake ya Katibu Mkuu KRFA kwa kupata kura zote 22.

Naye Pelegrinius Rutahyugwa alitetea nafasi yake ya ujumbe Mkutano Mkuu waTFF kwa kupata kura zote 22

Didas Zimbihile alitetea nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu klabu wa TFF kwa kukusanya kura zote 22.

Malinzi amekuwa Mwenyekiti wa KRFA tangu Machi 17, mwaka 2012 na katika kipindi chake cha kuwa madarakani, amesaidia kwa kiasi kikubwa kurejesha hamasa ya soka kimkoa.

Aidha, Malinzi amesaidia ukarabati wa Uwanja wa Kaitaba, ambao sasa una mwonekano mzuri, ukiwa unapambwa na nyasi bandia.

No comments:

Post a Comment