KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, March 5, 2016

TWIGA STARS YAJIWEKA PAGUMU


TIMU ya soka ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, imejiweka kwenye mazingira magumu ya kufuzu kucheza raundi ya pili ya michuano ya ubingwa wa Afrika baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Zimbabwe.

Katika mechi hiyo iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Azam Complex, ulioko Chamazi, Dar es Salaam, Twiga Stars ilikwenda mapumziko ikiwa sare ya bao 1-1.

Kutokana na kipigo hicho, Twiga Stars sasa italazimika kuishinda Zimbabwe mabao 2-0 katika mechi ya marudiano itakayochezwa wiki mbili zijazo mjini Harare.

Twiga Stars ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 17 lililofungwa na Mwanahamisi Omari kabla ya Erina Jeke kuisawazishia Zimbabwe dakika ya 19.

Bao la pili na la ushindi la Zimbabwe lilifungwa na Erika katika kipindi cha pili.

No comments:

Post a Comment