KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, March 27, 2016

TFF YAIAGIZA KRFA KUCHUNGUZA MATOKEO LIGI YA KATAVI


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekiagiza Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Katavi (KRFA) kufanya uchunguzi juu ya matokeo ya kumpata bingwa wa ligi ya mkoa huo iliyomalizika wikiendi hii kabla ya kutangaza Bingwa wa Mkoa wa Katavi.

TFF imeagiza KRFA kuziagiza kamati zake kufanya uchunguzi juu ya matokeo ya mwisho katika mchezo kati ya Stand FC dhidi ya Kazima FC, ambapo Stand FC iliibuka na ushindi wa mabao 16 - 0.

Kabla ya mchezo huo wa mwisho, klabu ya Nyundo FC ilikua inangoza kwa kuwa na pointi 21 na magoli 24 ya kufunga, na klabu ya Stand FC ilihitajia ushindi wa mabao 13 ili kuweza kuwa bingwa wa mkoa wa Katavi, hali inayopelea kuwepo kwa dalili za kupanga matokeo kwa ushindi wa Stand FC wa mabao 16 – 0 dhidi ya Kazima FC.

KRFA haitaruhusiwa kutangaza bingwa wa mkoa hadi uchunguzi ukamilke na TFF ijiridhishe na uchunguzi huo.

No comments:

Post a Comment