KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, March 13, 2016

SIMBA YAZIDI KUZITIMULIA VUMBI YANGA NA AZAM


SIMBA leo imeendelea kujidhatiti kileleni mwa ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Prisons bao 1-0 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo umeiwezesha Simba kuendelea kuongoza ligi hiyo, ikitofautiana na Yanga kwa pointi sita na Azam kwa pointi tisa.

Hata hivyo, Yanga na Azam, ambazo zimecheza mechi pugufu, zinaweza kupunguza tofauti hiyo ya pointi iwapo zitashinda mechi zake za vipo. Yanga inavyo viporo viwili wakati Azam inavyo viporo vitatu.

Bao pekee  na la ushindi la Simba lilifungwa na kiungo Awadh Juma, zikiwa zimesalia dakika tatu kabla ya mchezo huo kumalizika.

Simba itabidi kujiulaumu kwa kushindwa kutoka uwanjani na ushindi mkubwa wa mabao, kwani ilipata nafasi nyingi nzuri za kufunga mabao, lakini ilizipoteza


No comments:

Post a Comment