KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, March 6, 2016

YANGA, AZAM HAKUNA MBABE


Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC imeendelea kukamata usukani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya sare ya 2-2 na Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Timu zote zinafikisha pointi 47 baada ya kucheza mechi 20, lakini Yanga inabaki kileleni mwa wastani wake mzuri wa mabao.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Kennedy Mapunda, aliyesaidiwa na Frank Komba na Soud Lilla, wote wa Dar es Salaam, hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-1
Azam FC ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 10, baada ya beki wa Yanga, Juma Abdul Jaffar kujifunga katika jitihada za kuokoaa shuti la mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche.
Hata hivyo, beki wa kulia, Juma Abdul akaisawazisha makosa yake dakika ya 28 baada ya kufunga kwa shuti la umbali wa mita 20 bada ya kukutana na mpira ulioridishwa na beki wa Axam FC, Serge Wawa kufuatia shuti la Amissi Tambwe.
Mshambuliaji wa Burundi, Tambwe alipokea pasi ya Mzimbabwe, Donald Ngoma ambaye alianzishwia mpira wa kurusha na Mwinyi Hajji Mgwali.
Zikiwa zimesalia dakika tatu mchezo kuwa mapumziko, mshambuliaji wa Zimbabwe, Donald Ngoma akaifungia Yanga bao la pili kwa kichwa akimalizia pasi ya juu ya Tambwe.
Kabla ya kumpasia Ngoma, Tambwe alijaribu kufunga mwenyewe baada ya kupokea pasi ya Deus Kaseke, lakini shuti lake liliokolewa na kipa Aishi Manula na kumrudia tena Mrundi huyo, ambaye alimuinulia Donald aliyewainua vitini mashabiki wa Yanga dakika ya 42.
Kipa Aishi Manula a,ijitahidi kwenda kuokoa mpira huo ukiwa umekwishangia nyavuni, lakiji haujagusa chini – hata hivyo refa Mapunda akawapa Yanga haki yao.
Kipindi cha pili, Azam FC walirudi kwa bidii kutaka kusawazisha bao, lakini mchezo ukawa wa mashambulizi ya pande zote mbili.
Hata hivyo, mabadiliko ya kocha Muingereza wa Azam FC, Stewart John Hall kuwaingiza wachezaji wa zamani wa Yanga kiungo Frank Domayo na mshambuliaji Didier Kavumbangu yaliisaidia timu yake kuongeza kasi ya mchezo.
Na hatimaye Nahodha John Rapahael Bocco akaisawazishia timu yake dakika ya 70 kwa shuti kali akiwa ndani ya boksi, baada ya kupokea pasi ya Kipre Tchetche.
Kidogo Yanga wakaonekana ‘kupooza’ baada ya bao hilo huku Azam FC wakiendelea kusaka bao la ushindi.
Kuona hivyom kocha Mholanzi akaamua kuiwekea udhibiti pointi moja, baada ya kumuingiza beki Pato Ngonyani kwenda kuchukua nafasi ya Tambwe dakika ya 82.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva/Godfrey Mwashiuya dk68, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe/Pato Ngonyani dk82, Donald Ngoma na Deus Kaseke.
Azam FC; Aishi Manula, Shomary Kapombe, David Mwantika, Said Mourad, Serge Wawa, Farid Mussa/Didier Kavumbangu dk59, Jean Baptiste Mugiraneza, Himid Mao/Frank Domayo dk68, Ramadhani Singano ‘Messi’/Mudathir Yahya dk85, John Bocco na Kipre Tchetche.
IMETOLEWA KUTOKA BLOGU YA BINZUIBERY

No comments:

Post a Comment