KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, March 2, 2016

SERIKALI YAWAPA MOTISHA WACHEZAJI TWIGA STARS


Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa motisha kwa wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu wanawake(Twiga Stars) ikishinda katika mchezo wake dhidi ya Zimbabwe unatarajiwa kuchezwa siku ya Ijumaa tarehe 4 Machi katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.

Haya yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia James Wambula alipotembelea kambi ya Timu hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wachezaji wa Twiga Stars, Wambura amesema
kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa michezo wamekusanya shilingi milioni 15 ambazo zitatumika kama
motisha kwa wachezaji hao.

Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa iwapo timu hiyo itaibuka na
ushindi katika mechi yake dhidi ya Zimbabwe kila mchezaji
atapata gawio la sh. Laki tatu kama mptisha na kuongeza kuwa
itafanyika hivyo hivyo katika mchezo wa marudiano
utakaochezwa nchini Zimbabwe.

Aidha alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau wa michezo kuzidi
kujitokeza na kuisaidi timu hiyo ikiwa ni pamoja na kuhudhuria
kwa wingi katika mechi ya tarehe 4 machi dhidi ya Zimbabwe
itakayochezwa katika uwanja wa Taifa.

Aliongeza kuwa msaada zaidi unahitajika ili kuiwezesha timu hiyo
kukidhi mahitaji yake muhimu,hivyo alitoa wito kwa wadau
mbalimbali kutoa michango yao kupitia Twiga Specila Fund,
Akaunti na: 20110001677 iliyoko NMB tawi la Bank House jijjini
Dar es Salaam.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesiga
ameipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuhakikisha Twiga
Stars inapata huduma muhimu ikiwemo motisha kwa wachezaji
na benchi la ufundi.

Mwesiga pia amewapongeza wadau wote waliojitolea kusaidi timu
hiyo ambapo amesema kujitokeza kwa wadau hao kunaongeza
morali ya wachezaji.

Msaada huo wa shilingi milioni 15 umetolewa na wadau watatu
ambapo mmoja aliyechangia sh. Milioni 3 aliomba jina lake
lihifadhiwe, wengine ni Kampuni ya ASAS sh. Milioni 2 na
Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) sh. Milioni
10.

No comments:

Post a Comment