KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, March 3, 2016

TWIGA STARS WAPO TAYARI KUWAVAA WAZIMBABWE KESHO


Kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars), leo kimefanya mazoezi ya mwisho tayari kwa kuwakabili timu ya Taifa ya Wanawake kutoka Zimbabwe (Mighty Warriors) katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika kesho Ijumaa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Twiga Stars inayonolewa na kocha mzawa mwanamke, Nasra Juma imekamilisha ratiba yake leo asubuhi kwa kufanya mazoezi mepesi katika uwanja wa Karume ofisi za TFF, huku kocha wake Nasra akisema vijana wake wote wapo katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo huo.

Akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa TFF uliopo Karume, Nasra amesema ana waheshimu Zimbabwe wana timu nzuri, ndani ya miaka minne wameshacheza nao zaidi ya mara nne, mapungu yaliyojitokeza katika michezo iliyopita wamefanyi kazi na hivyo kesho ana imani watafanya vizuri.

Aidha kocha Nasra, amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kesho Ijumaa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi kuwapa sapoti Twiga Stars katika mchezo huo utakaonza majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Naye nahodha wa kikosi hicho Sophia Mwasikili, amesema wachezaji wote wapo katika hali nzuri, wana ana ari na morali ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo wa kesho, na kuwaomba watanzania kuwapa sapoti kwa kujitokeza kwa wingi kuja kuwashangilia uwanjani watakapokuwa wakipeperusha bendera ya Tanzania.

Wapinzani wa Twiga Stars, timu ya taifa ya Zimbabwe wanawasili leo jioni tayari kwa mchezo huo, huku waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Ethiopia wakiwa tayari wameshawasili leo mchana kwa shirika la ndege la Kenya (KQ).

No comments:

Post a Comment