KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, March 7, 2016

SIMBA YAREJEA KILELENI LIGI KUU


SIMBA jana ilirejea kileleni mwa ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Mbeya City mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Washambuliaji Ibrahim Hajib na Daniel Lyanga ndio walioiwezesha Simba kutoka uwanjani na pointi zote tatu baada ya kuifungia mabao hayo mawili.

Kwa ushindi huo, Simba sasa imefikisha pointi  48 baada ya kucheza mechi 21 na kuziengua Yanga na Azam, zenye pointi 47 kila moja huku zikiwa na mechi moja mkononi kila moja.

Lyanga, aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Bryan Majwega, alifunga bao la kwanza dakika ya 75 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Hannington Kalyesebula.

Hajib aliiongezea Simba bao la pili dakika ya 90 baada ya kuwatoka mabeki wa Mbeya City na kufumua shuti kama krosi lililotinga moja kwa moja wavuni.

No comments:

Post a Comment