KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, April 30, 2014

DIAMOND AAHIDI MAKUBWA MTWARA KESHOKUTWA



Nyota wa muziki wa Bongo flava nchini anayepasua anga ya Afrika, Rais wa wasafi kama wengi wanavyomuita, Diamond Platnum, Dangote ameahidi makubwa kwa mashabiki wake wote wa Mkoa wa Mtwara kuhusu show ya aina yake inayotarajiwa kufanyika katika umbi wa Makonde Club mjini Mtwara siku ya ijumaa tarehe 2 mwezi huu.


Msanii huyo aliyeafanikiwa kujizolea mamilioni ya mashabiki wa muziki wa Bongo flava atasindikizwa na kipenzi chake, Malkia wa Bongo Movie nchini, Wema Sepetu - 'Beautiful Onyinye' au Madame kama mashabiki wake wanavyopenda kumwita.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, katika ofisi za Vodacom Tanzania, ambao ndio wadhamini wa tamasha hilo amesema Mashabiki wakae mkao wa kula burudani ya nguvu ya muziki kutoka kwa kipenzi chao ambaye hafikirii kukosea wala kuwaangusha mashabiki wake katika show zake zote anazozifanya.

"Mashabiki wote waliopo Mtwara watashuhudia nikiimba live nyimbo yangu mpya ya My number One remix niliyomshirikisha Davido kutoka nchini Nigeria. Kwa kawaida huwa sipendi kuwaangusha mashabiki zangu hivyo basi nawaahidi makubwa sana katika tamasha hilo na ningependa kuwaona wengi wakihudhuria show hiyo kwani kutakuwepo na mengi ambayo hawakutarajia kuyaona" Alisema Diamond.

Msanii Diamond ambaye kwa sasa ndiyo mwenye mafanikio makubwa ya kimuziki nchini amekuwa ni kivutio kikubwa kwa mashabaiki wa ndani na nje ya nchi kila mahali anapoalikwa kufanya shoo na hivyo kujizolea sifa lukuki na hata kuchaguliwa kuwania tuzo mbali mbali za muziki barani Afrika.

Kwa upande wao wadhamini wa tamasha hilo Mkuu wa kitengo cha masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa amesema mtandao wao unajivunia kudhamini tamasha kubwa kama hili kwani hakuna kitu ambacho wanakijali kama wateja wao haijalishi wapo kona gani ya Tanzania.

"Tunajivunia kuwa sehemu ya Wadhamini wa Tamasha hili kubwa, Vodacom siku zote tumekuwa tukitoa kipaumbele kwa wateja wetu, Kipindi cha Pasaka tulifanya Tamasha pale coco beach na sasa ni zamu ya watu wa Mtwara" alisema Twissa na kuongeza.

"Tutawafikia wateja wetu popote pale walipo na kuwapa burudani Vodacom imekuwepo nchini kwa zaidi ya miaka kumi sasa na kwa kipindi chote hicho watanzania wameonyesha kutuunga mkono na kutufanya tuwe mtandao unaaongoza siku zote Hivyo hatuna budi kuwafanyia yale ambayo wanaweza wakafurahi ikiwemo kuwaletea burudani kama hii".

"Ili kuwarahisishia wateja wetu na wananchi kwa ujumla, mteja anaweza kununua tiketi yake kwa njia ya M-pesa kwa kutuma pesa kwenda 0754 980 769. Na atapatiwa ufafanuzi wa jinsi ya kupata tiketi yake. Wateja watakaotumia njia hii watapata punguzo la asilimia 20 (20%). Wateja wa Vodacom na Mashabiki wote kwa ujumla wasiache kuhudhuria shoo hiyo ambayo itakuwa na kishindo kikubwa na kwa aina yake". Alisema.

Aidha, "Vodacom tunaahidi kuenedelea kuwaunga mkono wasanii wetu wa Kitanzania na kujivunia kilicho chetu, wote ni mashahidi kwa namna ambavyo tumekuwa msitari wa mbele kuwaunga mkono wasanii wetu na tutaendelea na jitihada hizo na kufikia viwango vya wasanii wengine wa kimataifa," alihitimisha Twissa.

No comments:

Post a Comment