KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, July 21, 2011

Five Stars mpya yakamilika



MIEZI michache baada ya wasanii wake 13 kufariki katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Mikumi mkoani Morogoro, uongozi wa kundi la muziki wa taarab la Jahazi upo kwenye hatua za mwisho za kuliunda upya.
Rais wa kundi hilo, Ally J alilieleza gazeti la Burudani juzi kuwa, uzinduzi wa kundi hilo jipya unatarajiwa kufanyika Julai 29 mwaka huu kwenye ukumbi wa hoteli ya Travertine, Magomeni, Dar es Salaam.
Ally alisema tayari wameshawapata wasanii wa kutosha wa muziki wa taarab na wameshaanza mazoezi kwa ajili ya kulifufua upya kundi hilo.
Alimtaja mmoja wa wasanii hao wapya kuwa ni mwimbaji, Mussa Ally ‘Kijoti’, ambaye ni kaka wa marehemu, Issa Kijoti, aliyefariki katika ajali hiyo.
Kwa mujibu wa Ally, waimbaji wengine wapya watakaounda kundi hilo ni pamoja na mshindi wa shindano la Bongo Star Search (BSS) mwaka jana, Mariam Mohamed na Isha Mzee.
Alisema katika uzinduzi huo, Mussa atakabidhiwa rasmi mikoba ya marehemu kaka yake, Issa na ataimba nyimbo zote zilizoachwa na ndugu yake huyo.
Ally alisema uzinduzi huo utasindikizwa na wasanii mbalimbali nyota wa muziki, akiwemo mwimbaji mkongwe, Mwanahawa Ally na makundi mengine ya taarab.
Amewataka mashabiki wa muziki huo, kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo, ambao aliuelezea kuwa, utakuwa wa aina yake.

No comments:

Post a Comment