KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, September 3, 2014

YANGA YAINGIA MKATABA NA CRDB


Uongozi wa klabu ya Young Africans leo umewekeana sahihi ya makubaliano na Benki ya CRDB nchini juu ya uboreshaji na utengenezaji wa kadi za uanachama, hafla hiyo imefanyika katika Makao Makuu ya Benki hiyo eneo la Posta mpya jijni Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dr Charles Kimei amesema anaushukuru uongozi wa Yanga kwa kuwaamini benki yao kuwa wanaweza kufanya kazi hiyo, na sisi tunaamini tutafanya kazi vizuri na kuweza kufikia malengo yao waliyotuwekea katika kipindi muafaka.

"Kwetu sisi kupata nafasi ya kufanya kazi na klabu ya Yanga ni jambo jema, tunatambua wana wana wapenzi zaidi ya milioni 20 nchi nzima, hivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunawifikia kila sehemu walipo na wanajiunga na uanachama wa klabu yao pendwa," alisema Dr Kimei.

Aidha Kimei amesema kwa utaratibu huo wa mfumo wa kisasa, wataanza kwa kutoa bure kadi za uanchama wa Yanga ambazo zitakua na nembo ya VISA itakayomfanya mtumiaji aweze kuitumia sehem yoyote alipo na kurahisisha zoezi la ukusanyaji wa ada za uanachama.

Gharama ya kadi itakua ni Tshs 8,000 tu kwa watakaoanza upya (bure kwa waliokua tayari wanachama) na mteja/mwanachama ataendelea kuichangia klabu yake ya Yanga kiasi cha Tsh 250/= tu kwa wiki ambapo kwa mwezi ni sawa Tsh 1,000/= na kufanya kwa mwaka ada kuwa ile ile Tshs 12,000/=.
Mjumbe wa Baraza la Wadhamini wa klabu ya Young Africans, Bi Fatma Karume amesema anaishukuru benki ya CRDB kwa kubali kufanya kazi hiyo, na kwa uwezo wao wa utendaji kazi anaamini wataifanya kazi hiyo kwa kiwango cha hali ya juu.
"Kikubwa nilichofurahi ni kuwa hawa CRDB Bank wapo mpaka kwetu Unguja, hivyo naona zoezi hilo litafanikiwa vizuri na kurahisisha upatikanaji wa kadi za wanachama kwa uharaka zaidi," alisema  Bi Fatma.
Kadi mpya za uanachama wa Yanga zitakazotolewa na CRBD Bank zitakua za aina mbili, Premieum Visa Card kwa ajili ya viongozii mashuhuri wa klabu ya Young Africans tangu kuanzishwa kwake na nyingine ni Normal Visa Card kwa ajili ya wanachama wa kawaida.
Awali klabu ya Young Africans ilikuwa na mkataba wa aina hiyo na Benki ya Posta, Uongozi wa Yanga umeshawasilisha Notice kwa benki ya Posta juu ya kusitisha mkataba nao na sasa huduma hiyo itaanza kutolea kupitia benk ya CRDB.

No comments:

Post a Comment