KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, September 11, 2014

PHIRI KUIPIMA SIMBA KWA URA YA UGANDA KESHO


SIMBA kesho inatarajiwa kushuka tena dimbani kumenyana na URA ya Uganda katika mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Mechi hiyo itakuwa ya pili ya kimataifa kwa Simba baada ya wiki iliyopita kuvaana na Gor Mahia ya Kenya na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri, anatarajiwa kuutumia mchezo huo kufanya tathmini ya mwisho kwenye kikosi chake kabla ya kuanza kwa michuano ya Ligi Kuu Septemba 20 mwaka huu.

Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu', alisema jana kuwa maandalizi ya mchezo huo yanakwenda vizuri na wapinzani wao walitarajiwa kuwasili Dar es Salaam leo.

Kaburu amewaomba manazi wote wa Simba kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuishangilia timu yao kwa lengo la kuwapa nguvu wachezaji.

No comments:

Post a Comment