KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, April 9, 2016

YANGA YALAZIMISHWA SARE NA AL AHLY


WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya soka ya klabu bingwa Afrika, Yanga wamejiweka kwenye mazingira magumu ya kusonga mbele baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Al Ahly ya Misri.

Katika mechi hiyo iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, timu zote mbili zilipata mabao hayo kipindi cha kwanza.

Ahly ilikuwa ya kwanza kuzitikisa nyavu za Yanga dakika ya 11 kwa bao lililofunga na Amr Gamal baada ya mabeki wa vijana hao wa Jangwani kuzembea kuokoa mpira wa adhabu.

Bao la kusawazisha la Yanga lilipatikana dakika ya 18 baada ya beki mmoja wa Al Ahly kujifunga wakati alipokuwa akijaribu kuokoa shuti la winga wa Yanga, Issoufou Boubacar.

Kwa matokeo hayo, ambayo yamefurahiwa na wachezaji wa Al Ahly, Yanga sasa italazimika kushinda mechi ya marudiano, itakayochezwa Aprili 19 mwaka huu mjini Alexandria.

No comments:

Post a Comment