KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, April 8, 2016

YANGA, AL AHLY KUONYESHWA LIVE NA AZAM TV KESHO

YANGA imeiuzia Azam TV haki za kurusha mechi ya kwanza ya hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Maana yake kesho Watanzania wote wataushuhudia mchezo huo kupitia Televisheni nchini.
Azam TV wamefanikiwa kupata haki hizo baada ya kuwapiku Al Ahly ambao pia walikuwa wanataka haki za kurusha mechi hiyo.
Mapema jana Yanga iliwagoma Al Ahly kurusha matangazo ya mechi hiyo.
Yanga watakuwa wenyeji wa Ahly kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika na Ahly walitaka wachukue matangazo kwa ajili ya kurusha Misri tu.
Hata hivyo, leo uongozi wa Ahly umethibitisha rasmi kwamba umenyimwa haki hiyo na utaonyesha mechi hiyo kupitia mitandao tu.
Wakati huo huo, uongozi wa Yanga umegoma kuwauzia wapinzani wao, Al Ahly ya Misri haki za kurusha matangazo ya mechi baina yao kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga watakuwa wenyeji wa Ahly kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika na Ahly walitaka wachukue matangazo kwa ajili ya kurusha Misri tu.
Hata hivyo, leo uongozi wa Ahly umethibitisha rasmi kwamba umenyimwa haki hiyo na utaonyesha mechi hiyo kupitia mitandao tu.

IMETOLEWA KUTOKA BLOGU YA BINZUBEIRY

No comments:

Post a Comment