KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, April 28, 2011

Kaseja, Nsajigwa kuwania tuzo mwanamichezo bora


Kaseja Nsajigwa


WACHEZAJI Juma Kaseja wa Simba, Shadrack Nsajigwa wa Yanga na Mrisho Ngasa wa Azam ni miongoni mwa watakaowania tuzo za mwanamichezo bora wa mwaka 2010 zitakazotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
Sherehe za utoaji wa tuzo hizo zimepangwa kufanyika Mei 6 mwaka huu kwenye hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam.
Akitangaza majina hayo jana, Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando alisema jumla ya tuzo 18 zitatolewa kwa wanamichezo wa michezo tofauti.
Mhando alisema wanamichezo hao kwa upande wa wanaume na wanawake, watapigiwa kura na jopo maalumu la waandishi wa habari kwa ajili ya kuteua mchezaji bora wa mwaka.
Aliwataja wanamichezo hao kwa upande wa soka ya wanaume kuwa ni Kaseja,Nsajigwa, Ngasa na Khamis Mcha (Zanzibar Ocean View). Kwa wanawake ni Asha Rashid, Mwanahamisi Omary na Fatuma Omary.
Riadha wanaume ni Samson Ramadhan, Marco Joseph na John Bazil wakati wanawake ni Zakia Mrisho, Mary Naali na Magdalena Mushi. Wachezaji wa mpira wa wavu wanaume ni Kevin Peter (Magereza), Mbwana Ally (Mzinga Morogoro) na Ibrahim Christopher ( Nyuki Zanzibar) na wanawake ni Hellen Richard Mwegoha (Magereza), Yasinta Remmy na Zainabu Thabit (Jeshi Stars). Kwa upande wa netiboli ni Lilian Sylidion (Filbert Bayi), Mwanaid Hassan na Sekela Dominick (JKT Mbweni) wakati katika mchezo wa karate wanaume ni Sempai Steven Bella na Semapai Ayub Seleman.
Walioteuliwa kuwania tuzo kwa mchezo wa kikapu wanaume ni George Otto Tarimo (Savio-Dsm), Lusajo Samwel Mwakipunda na Gilbert Batungi (Oilers-DSM) na kwa wanawake ni Faraja Malaki- (Jeshi Stars-DSM), Zakhia Kondo (Lady Lioness-DSM) na Doritha Mbunda (JKT Stars).
Katika mchezo wa ngumi za kulipwa ni Karama Nyilawila, Mbwana Matumla na Francis Cheka wakati ngumi za ridhaa ni Revocatus Shomari, Selemani Kidunda na Said Dume.
Mchezo wa gofu kwa wanawake ni Hawa Wanyeche, Madina Iddi na Vailet Peter wakati wanaume ni Frank Roman, Adam Abbas na Isaac Anania. Kwa upande wa baiskeli wanaume ni Hamis Clement, Richard Laizer na Said Jumanne na wanawake ni Sophia Anderson, Martha Anthony na Ndashimba Kulia.
Kriketi wanaume ni Kassim Nassor, Seif Khalifa na Benson Mwita na kwa wanawake ni Hawa Salum, Mariam Said na Sophia Hemed. Mpira wa mikono wanaume ni Kazadi Monga (Magereza), Hemed Saleh na Abineri Kusena (JKT) na wanawake ni Happiness Mahinya (JKT), Teresia Kifukwe (Magereza), Zena Mohammed (JKT).
Tuzo nyingine ni ya wanamichezo wa Tanzania wanaocheza nje, ambayo itawaniwa na Hasheem Thabeet (kikapu),Henry Joseph na Nizar Khalfan (soka) na Rogers Mtagwa (ngumi) wakati wachezaji wa nje wanaocheza Tanzania ni Emmanuel Okwi (Simba), Yaw Berko (Yanga) na Kanda Kabongo (kickboxing).
Wanaowania tuzo ya mwanamichezo chipukizi kwa upande wa riadha ni John Bazil na Magdalena Cristian, Lilian Sylidion (netiboli), Vailet Peter (gofu) na mchezo wa judo ni Khamis Azan Hussein, Abeid Omar Dola na Masoud Amour Kombo wote kutoka Zanzibar

No comments:

Post a Comment