KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, April 28, 2011

Kado azitosa Simba na Yanga



KIPA wa timu ya taifa ya vijana, Shaabani Kado amesema hajafanya mawasiliano yoyote na viongozi wa klabu za Simba na Yanga kwa ajili ya kumsajili msimu ujao.
Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Kado alisema bado yeye ni mchezaji halali wa Mtibwa Sugar na ataendelea kuichezea msimu ujao.
Kado alisema amekuwa akisikia taarifa hizo kupitia kwenye vyombo vya habari, lakini binafsi hana mpango huo.
"Mimi sijawahi kukutana na viongozi wa klabu hizo kuzungumzia mpango wa kujiunga na timu zao, nitaendelea kuwepo Mtibwa Sugar msimu ujao,"alisema mlinda mlango huyo.
Wakati kipa huyo anatoa tamko hilo, klabu ya Simba ndiyo iliyoonyesha nia kubwa ya kutaka kumnasa Kado kutokana na kuwepo habari kwamba wana mpango wa kumtema Juma Kaseja.
Kutemwa kwa Kaseja na mshambuliaji Mussa Hassan ‘Mgosi’, kumeigawa klabu hiyo, ambapo kamati yake ya utendaji iliyokutana wiki iliyopita ilishindwa kutoa uamuzi.
Alipoulizwa jana, Mratibu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser alisema hana taarifa za kutakiwa kipa huyo na klabu hizo mbili, ingawa ameeleza kuwa amesoma habari hizo kupitia magazetini.

No comments:

Post a Comment