'
Tuesday, October 24, 2017
YANGA YATOA DOZI YA 4G KWA STAND UNITED
YANGA SC wameonyesha wapo tayari kutetea ubingwa, baada ya leo kuwafumua mabao 4-0 wenyeji Stand United kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Shujaa wa Yanga alikuwa mshambuliaji mpya, Ibrahim Hajib Migomba aliyefunga mabao mawili na kuseti moja, lililofunga na Obrey Chirwa wakati bao lingine la wana Jangwani hao limefungwa na kiungo Pius Buswita.
Kwa matokeo hayo, Yanga inafikisha pointi 15 baada ya kucheza mechi saba na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakizidiwa kwa wastani wa mabao tu ya kufunga na kufungwa na Simba SC wenye pointi 15 pia sawa na Mtibwa Sugar walio nafasi ya tatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment