'
Wednesday, December 23, 2015
SERIKALI YAUPATIA UFUMBUZI MGOGORO WA TIMU YA SOKA YA STAND UNITED
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hatua zilizofikia katika kutatiua mgogoro baina ya Timu ya Stand Unite ya mjini Shinyanga na kamati ya uendeshaji ya timu hiyo iliyopo chini ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo jijini Dar es Salaam.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,WHUSM.
Na: Frank Shija, WHUSM
Serikali imeagiza kumalizika kwa mgogoro uliopo baina ya Timu ya mpira wa miguu ya Stand United na Kamati ya uendeshaji wa timu hiyo iliyopo chini ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Agizo hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye mara baada ya kumaliza kikao na uongozi wa Stand United.
Nape amesema kuwa imefika wakati vilabu vikapewa uhuru wa kujiendesha kwa kutumia katiba zao badala ya kingiliwa na chombo kingine chenye maslahi binafsi.
“Wizara itasaidia kuona mgogoro huu unaisha kwa Stand United kupewa uhuru wa kujiendesha yenyewe na uongozi uliokuwapo kupewa mamlaka yake ya kusimamia na kuendesha shughuli za Timu yao kwa mujibu wa Katiba”
Aidha aliongeza kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kusimamia uendeshaji wa mchezo wa mpira wa miguu kwa kuzingatia sheria ,kanuni na taratibu za mchezo huo ili kuepuka migogoro isiyokuwa na tija.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Timu ya Stand United Bw. Aman Vicent ameishukuru Serikali kupitia Wizara yenye dhamana na masuala ya michezo kwa kuona umuhi wa kushughulikia na kumaliza mgogoro wao.
Aman amesema kuwa kutokana na makubaliano waliyofikia katika kikao hicho imani yao ni kuwa suala hili litamalizika mapema kwa kuwa Waziri mwenye dhamana ameonyesha nia na utayari wa kuhakikisha suala hili linaisha kwa wakati ili Timu iweze kusonga mbele katika kujiletea maendeleo.
Kikao baina ya Waziri na uongozi wa Timu hiyo kimefanyika ikiwa ni matokeo ya juhudi za uongozi wa Timu ya Stand Uinted kuinusuru timu yao baada ya kujikuta katika mgogoro usiokuwa na tija zaidi ya maslahi binafsi kutoka na udhamini walionao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment