KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, December 30, 2015

AZAM YAREJEA KILELENI LIGI KUU


Goli pekee la team captain John Bocco JB ‘Adebayor’ limeipa Azam FC nafasi ya kuongoza ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kwa kuiondoa Yanga kwenye nafasi hiyo baada ya kufikisha jumla ya pointi 35 wakiwa wamecheza mechi 13 sawa na Yanga yenye pointi 33 baada ya kucheza mechi 13 pia.

Azam wamekwea kileleni mwa VPL baada ya kuifunga Mtibwa Sugar kwa goli 1-0 kwenye mchezo wao wa kipolo uliopgwa leo kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.



Mchezo wa leo ulikuwa mgumu kwa upande wa Azam kutokana na kubanwa na Mtibwa Sugar kila sehemu kwa dakika zote za mchezo huo. Mtibwa walimiliki mchezo kwa dakika zote lakini walishindwa kupachika mabao kutokana na nafasi ambazo walitengeneza.

Wakati kila mtu akiamini mchezo huo utamalizika kwa sare ya bila kufungana (0-0), ndipo nahodha huyo na mkongwe wa Azam FC akaifungia goli timu yake na kuipaisha hadi kileleni mwa msimamo wa ligi. Bocco alifunga goli hilo kwa mpira wa adhabu ndogo baada ya yeye mwenyewe kuchezewa ndivyo sivyo nje kidogo ya eneo la hatari.

Bocco alipiga shuti kali ambalo lilijaa wavuni moja kwa moja na kumwacha golikipa wa Mtibwa Sugar Said Mohamed akiwa hana la kufanya.


Winga wa Azam FC Farid Musa akijaribu kumtoka mchezaji wa Azam FC Winga wa Azam FC Farid Musa akijaribu kumtoka mchezaji wa Azam FC

Matokeo hayo ya ushindi kwa Azam ni habari mbaya kwa Yanga kutokana na kushushwa kwenye nafasi ya kwanza hadi ya pili hasa katika kipindi hiki ambacho ligi ya Vodacom Tanzania bara itasimama kwa muda tena kupisha mashindano ya Mapinduzi Cup yanayotarajia kuanza January 3, 2016 visiwani Zanzibar ambapo timu tatu kutoka Tanzania bara zitashiriki mashindano hayo.

CHANZO CHA HABARI. BLOGU YA SHAFFIE DAUDA

No comments:

Post a Comment