'
Sunday, December 20, 2015
NAPE KUMWAKILISHA SAMIA TAMASHA LA PASAKA
Na Mwandishi Wetu
WAZIRIwa Habari,Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye anatarajia kumwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama, Makamu huyo wa rais alitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo lakini kutokana na majukumu mengine ya kikazi, hivyo tunaendelea na maandalizi ya tamasha hilo.
Msama alisema wanamshukuru Nape kukubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo lina mlengo wa kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25.
“Ni nafasi yetu kama Kampuni na Watanzania kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya kipindi ambacho kilikuwa kigumu katika maendeleo ya Tanzania, alisema Msama.
Aidha Msama alitoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo kwa sababu ya kufikisha shukrani kwa Mungu baada ya uchaguzi Mkuu.
Alitaja viingilio kwa VIP ni shilingi 50,000, viti maalum shilingi 10,000, viti vya kawaida shilingi 5000 na watoto shilingi 2000.
Msama aliwataja waimbaji watakaopanda jukwaani siku hiyo ni pamoja na Rebecca Malope (Afrika Kusini), Solomon Mukubwa, Sarah K, Faustin Munishi (Kenya), Rose Muhando, Upendo Nkone, Jesca BM, Joshua Mlelwa, Kwaya ya Wakorintho Wapili na KKKT Yombo.
“Maandalizi yamefanyika kwa kiasi kikubwa yamefanyika, hivyo nawaomba Watanzania tujitokeze kwa wingi siku hiyo ili kufanikisha asante kwa Mungu,” alisema Msama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment