KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, November 9, 2011

Jim Iyke atanua na magari ya kifahari


LAGOS, Nigeria
MWIGIZAJI mwenye mvuto nchini Nigeria, Jim Iyke ameendelea kudhihirisha jinsi alivyo mtu wa matanuzi baada ya kununua magari mawili ya kifahari yenye thamani ya dola 100,000 za Marekani.
Mbali na kununua magari, Jim amejenga jumba la kifahari mjini Abuja, ambalo thamani yake inakadiriwa kufika Naira milioni 90 za Nigeria.
Magari hayo mawili ni mwendelezo wa vitu kadhaa vya thamani, ambavyo mcheza filamu huyo amevinunua katika siku za hivi karibuni. Magari yaliyonunuliwa na Jim, ambayo yote mawili yapo wazi kwa juu ni aina ya Plymouth Prowler na Camero SS yaliyotengenezwa mwaka huu.
Jim amekuwa mtu wa pili kumiliki gari aina ya Prowler katika mji wa Abuja na amekuwa wa kwanza kumiliki gari aina ya Camero.
Kwa mujibu wa watu wake wa karibu, amenunua gari aina ya Prowler kwa dola 45,000 za Marekani wakati gari aina ya Camero limemgharimu dola 55,000.
Imeelezwa kuwa, jumba la Jim lina maeneo manane kwa ajili ya wanaume, wanawake, vinywaji, watoto pamoja na sehemu za kutengeneza nywele na mapambo. Uzinduzi wa jumba lake hilo umepangwa kufanyika Novemba 12 mwaka huu na unatarajiwa kuhudhuriwa na watu mbalimbali maarufu, akiwemo Gavana wa Abuja, Rochas Okorocha.

No comments:

Post a Comment