KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, July 20, 2016

SIMBA, YANGA KUVAANA OKTOBA MOSI, 2016


MIAMBA ya soka nchini Yanga na Simba, inatarajiwa kuteremka dimbani Oktoba Mosi, mwaka huu.

Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa mahasimu hao kukukata katika msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao ni mechi namba 49 katika raundi ya 10.

Yanga na Simba, zitavaana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara unatarajiwa kuanza Agosti 20, mwaka huu katika viwanja mbalimbali.

Kufuatia ratiba iliyotolewa jana na Shirikisho la Soka Tanzania TFF, mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utazikutanisha Yanga na Azam utachezwa Agosti 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Baada ya kufanyika kwa mchezo huo, Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu mpya utakuwa umefunguliwa rasmi.

Baada ya mchezo huo Yanga watafungua dimba na JKT Ruvu Agosti 31, katika mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofi sa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema kwa ujumla Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2016/ 2017 itaanza Agosti 20, Simba wakifungua dimba na Ndanda Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku Azam wakiikaribisha African Lyon Uwanja wa Chamazi.

Lucas alisema kuwa ratiba hiyo imekamilika na imeangalia mambombalimbali ikiwemo mechi za kimataifa ili kuepukana na viporo kama ilivyokuwa msimu uliopita.

“Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao imeshakamilika na tumezingatia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mechi za kimataifa ili kuhakikisha tunaepuka viporo,” alisema Lucas.

Mechi zingine za ufunguzi zitakuwa kati ya Kagera Sugar na Mbeya City Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, TotoAfricans na Mwadui Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Stand United na Mbao FC zitakazomenyana kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Mechi zingine zitazikutanisha timu za Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro na Majimaji na Prisons Uwanja wa Majimaji Songea.

No comments:

Post a Comment