KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, July 16, 2016

TFF SASA YAUTAMBUA UONGOZI MPYA WA STAND UNITED



Katika kikao chake cha 13 Julai, 2016, Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imetoa msimamo kuhusu suala la Stand United kama ifuatavyo:-

Kamati imepitia vielelezo vyote na kujadiliana na wadau wa Stand United na kubaini bayana kwamba Stand United Football Club, ndiyo jina sahihi na halali lililosajiliwa kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo.

Uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kwenye Klabu ya Stand United una sifa zote za kuitwa uchaguzi huru na wa haki kwa vile mchakato ulihusisha wanachama halali klabu hiyo.

Wanachama wa Stand United ambao hawakushiriki uchaguzi ikiwa ni pamoja na wale waliokwenda kundi la kampuni wana uhalali wa kuendelea kuwa wanachama wa Stand United.

Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi wa Stand United FC ni halali na ni ruksa kwao kuendesha ofisi na shughuli za Stand United kwa ujumla.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania linatambua daftari la Wanachama wa Stand United lililoboreshwa kwa maelekezo ya TFF.


IMETOLEWA NA DOMINA MADELI –

MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI TFF

No comments:

Post a Comment