'
Wednesday, August 9, 2017
KAMPENI UCHAGUZI TFF ZAENDELEA, WALIOKATWA WAREJESHWA
Kampeni za wagombea mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika shirikisho, zinaendelea.
Kwa mujibu wa kanuni 11.10 ya uchagizi wa TFF, kampeni hizo za wiki moja hadi Ijumaa wiki hii ambako Uchaguzi Mkuu utafanyika Agosti 12, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Hosteli ya Mtakatifu Gasper mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa kamati hiyo iliyokutana Jumamosi Agosti 5 2017, wagombea ambao wanawania urais ni pamoja na Wallace Karia, Imani Madega, Fredrick Mwakalebela, Ally Mayay, Shija Richard na Emmanuel Kimbe.
Katika nafasi ya Makamu wa Rais wanaowania ni Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa.
Kanda namba 1 ya Mikoa ya Kagera na Geita: waliopitishwa ni Saloum Chama, Leopold Mukebezi na Kaliro Samson wakati Kanda namba 2 inayounganisha mikoa ya Mara na Mwanza wamo Aaron Nyanda, Vedastus Lufano, Samwel Daniel na Ephraim Majinge.
Kanda namba 3 (Mikoa ya Shinyanga na Simiyu) wanaowania nafasi hiyo ni Stanslaus Nyongo, Bannista Rogora na Mbasha Matutu ilihali Kanda namba 4 (Mikoa ya Arusha na Manyara) waliopitishwa ni Omar Walii, Sarah Chao na Peter Temu.
Katika Kanda namba 5 inayounganisha mikoa ya Kigoma na Tabora waliopitishwa ni John Kadutu, Issa Bukuku, Abubakar Zebo na Francis Michael wakati Kenneth Pesambili na Baraka Mazengo – wote wamepitishwa kuwania ujumbe kupitia Kanda namba 6 yenye mikoa ya Katavi na Rukwa.
Kanda namba 7 inayounganisha mikoa ya Mbeya na Iringa waliopitishwa ni Elias Mwanjala, Cyprian Kuyava na Erick Ambakisye huku Kanda namba 8 yenye mikoa ya Njombe na Ruvuma waliopitishwa ni James Mhagama, Golden Sanga, Vicent Majili na Yono Kevela.
Kanda namba 9 Lindi na Mtwara Athumani Kambi na Dunstan Mkundi (wamepitishwa) wakati Kanda namba 10 Dodoma na Singida waliopitishwa ni Hussein Mwamba, Steward Masima, Ally Suru na George Komba.
Kanda namba 11, mikoa ya Pwani na Morogoro waliopitishwa ni Charles Mwakambaya, Gabriel Mkwawe na Francis Ndulane wakati Kanda namba 12 Kilimanjaro na Tanga waliopitishwa ni Khalid Mohamed na Godluck Moshi.
Kanda namba 13 Dar es Salaam: waliopitishwa ni Emmanuel Kazimoto, Abdul Sauko, Ayoub Nyenzi, Shaffi Dauda, Peter Mhinzi, Lameck Nyambaya, Mussa Kissoky, Said Tully, Ally Kamtande, Aziz Khalfan, Ramadhani Nassib na Saad Kawemba.
Hii sasa ni orodha ya mwisho baada ya baadhi ya wagombea kufanikiwa kushinda rufaa zao katika Kamati ya Rufaa za Uchaguzi wakipinga kuondolewa na Kamati ya Uchaguzi.
Kamati ya Uchaguzi ilipokea taarifa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kueleza kuwa iliwakamata viongozi wa soka kutoka mikoa mbalimbali katika mazingira ya kuvunja sheria za nchi na kanuni za uchaguzi.
Kamati iliamua kuwaondoa wagombea hao ambao ni Shafii Dauda wa Dar es Salaam; Banista Rugora wa Shinyanga; Ephraim Majinge wa Mara na Elias Mwanjala wa Mbeya katika kuwania nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji katika uchaguzi ujao wa TFF unatarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu kwa ukikwaji wa Kanuni ya 14 (3) inayozungumzia kampeni kabla ya wakati.
MAJIBU KAMATI YA RUFAA ZA UCHAGUZI
Kamati ya Rufaa za Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania pia imetoa matokeo ya rufaa nne ilizosikiliza Jumamosi Agosti 5, 2017 zilizokatwa dhidi ya Kamati ya Uchaguzi katika mchakato wa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya TFF.
Waliokata Rufaa ni Fredrick Masolwa ambaye awali hakupitishwa kuwania nafasi ya urais kwa kukosa uzoefu kwa mujibu wa kanuni ya 9 (3) ya kanuni za uchaguzi za TFF. Kamati ya Rufaa ilitupilia mbali hoja hiyo kwa sababu ya rufaa kukosa kigezo cha kutolipia kwa mujibu wa katiba ya TFF.
Mwingine ni Mgombea Ujumbe wa Kamati ya Utendaji Kanda namba 7 (Mikoa ya Mbeya na Iringa), Abdusuphyan Sillah awali hakupitishwa kwa kukosa uzoefu kwa mujibu wa kanuni ya 9 (3) ya kanuni za uchaguzi za TFF.
Rufaa yake ilikuwa na vigezo, lakini ilikosa hoja za uadilifu kwa mujibu wa Kanuni ya 9 (7) kwani mrufani alikosa uadilifu kwa kutoa taarifa za uongo mbele ya kamati.
Kanda namba 11 (Mikoa ya Pwani na Morogoro), Hassan Othuman awali hajapitishwa kwa kukosa uadilifu jambo ambalo alilikatia rufaa Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF. Hata hivyo, alituma ujumbe mbele ya Kamati ya Rufaa akitangaza kujitoa.
Kanda namba 13 Dar es Salaam: Saleh Abdallah awali hakupitishwa kwa kukosa uzoefu kwa mujibu wa kanuni ya 9 (3) ya kanuni za uchaguzi za TFF. Kamati ilitupilia mbali rufaa yake kwa sababu kwanza hakulipia hivyo kukosa vigezo pia hata mrufani mwenyewe hakutokea kutetea rufaa yake.
Monday, August 7, 2017
NIYONZIMA AANZA RASMI MAZOEZI SIMBA
SINGIDA UNITED YAIBOMOA KAIZER CHIEF,YAMTWA MSHAMBULIAJI HATARI TOKA ZIMBABWE
Matajiri kutoka mkoani Singida klabu ya Singida United wamefanya mabadiliko kidogo katika safu ya ushambuliaji katika usajili baada ya kufungwa na Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga cha magoli 3-2 kwenye Mchezo wa Kirafiki uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu, imemchukua mshambuliaji Michelle Katsavairo kutoka klabu ya Keizer Chiefs ya Afrika Kusini kwa mkopo na kumuacha Mzimbabwe mwenzake, Wisdom Mtasa.
Hayo yamethibitishwa na Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo amesema kwamba baada ya kusajiliwa kwa Katsavairo kutoka Kaizer, Mtasa anapalekwa kwa mkopo wa Stand United ya Shinyanga.
Aidha Mkurugenzi huyu amesema kuwa wamefanya hivyo ili kuweza kusajili mchezaji mwingine wa kigeni japo kuwa walikuwa wamefikia idada ya wachezaji saba wa kigeni hivyo imewapelekea kumtoa mchezaji m0ja kwa mkopo.
Singida United mpaka sasa wameshacheza michezo mitano ya kirafiki wakishinda mechi mbili dhidi ya Pamba 5-0 na Alliance 2-0 huku wakitoka sare na wanajeshi wa Pwani Ruvu Shooting ya kufungana goli 1-1 na kupoteza michezo miwili dhidi ya Lipuli FC kwa kufungwa 1-0 na kufungwa 3-2 na Yanga.
Licha ya kufungwa na Yanga ,vijana wa Hans Van Der Pluijm walicheza kandanda safi na la kuvutia na kutawala kwa kila kitu na kuwapoteza kabisa viungo wa Yanga tatizo ambalo lilitakiwa kufanyiwa marekebisho ni la golikipa na tayari timu hiyo imemsajili mlinda mlango kinda toka kwa Wekundu wa Msimbazi Simba Manyika Peter ambaye amesaini miaka miwili.
Singida United itatumia uwanja wake wa nyumbani wa Jamhuri Dodoma kutokana na uwanja wa Namfua bado upo katika matengenezo makubwa na utakapokamilika timu hiyo itaweza kurejea katika makazi yake na inatazamiwa kuleta changamoto kubwa kwa timu kubwa kutokana na kufanya usajili mkubwa huku ikiwa ndio kinara kwa kuwa na wadhamini wengi kuliko timu yoyote ile Tanzania tangu lingi ianzishwe.
AZAM FC YATUA UGANDA KWA AJILI YA KUIPASHIA VPL
KIKOSI cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, tayari kimetua nchini Uganda kwa kambi ya siku 10 ya maandalizi ya msimu ujao utakaoanza Agosti 26 mwaka huu.
Kambi hiyo ni maalumu kabisa kwa ajili ya kucheza mechi nne kali za ushindani, dhidi ya KCCA, URA, SC Villa na Vipers, zitakazotumika kuwajenga wachezaji wa timu hiyo kabla ya mikikimikiki ya ligi kuanza.
Msafara wa Azam FC ulioongozwa na Meneja Phillip Alando, unaundwa wachezaji 26 na makipa Mwadini Ally, Razak Abalora, Benedict Haule, Mabeki ni Nahodha Msaidizi Aggrey Morris, David Mwantika, Yakubu Mohammed, Daniel Amoah, Abdallah Kheri, Swaleh Abdallah, Bruce Kangwa, Hamimu Abdul.
Viungo ni Nahodha Himid Mao ‘Ninja’, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo ‘Chumvi’, Stephan Kingue, Salmin Hoza, Bryson Raphael, Masoud Abdallah ‘Cabaye’, mawinga Joseph Mahundi, Enock Atta, Idd Kipagwile, Joseph Kimwaga na washambuliaji Yahaya Mohammed, Mbaraka Yusuph, Wazir Junior, Yahya Zayd.
Kikosi hicho kimefikia kwenye Hoteli ya Top Five, iliyopo Ntinda, jijini Kampala, Uganda, ambapo muda si mrefu benchi la ufundi linatarajia kutoa programu kamili hadi mwisho wa ziara hiyo itakayomalizika Agosti 15 mwaka huu.
Kambi hiyo ni maalumu kabisa kwa ajili ya kucheza mechi nne kali za ushindani, dhidi ya KCCA, URA, SC Villa na Vipers, zitakazotumika kuwajenga wachezaji wa timu hiyo kabla ya mikikimikiki ya ligi kuanza.
Msafara wa Azam FC ulioongozwa na Meneja Phillip Alando, unaundwa wachezaji 26 na makipa Mwadini Ally, Razak Abalora, Benedict Haule, Mabeki ni Nahodha Msaidizi Aggrey Morris, David Mwantika, Yakubu Mohammed, Daniel Amoah, Abdallah Kheri, Swaleh Abdallah, Bruce Kangwa, Hamimu Abdul.
Viungo ni Nahodha Himid Mao ‘Ninja’, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo ‘Chumvi’, Stephan Kingue, Salmin Hoza, Bryson Raphael, Masoud Abdallah ‘Cabaye’, mawinga Joseph Mahundi, Enock Atta, Idd Kipagwile, Joseph Kimwaga na washambuliaji Yahaya Mohammed, Mbaraka Yusuph, Wazir Junior, Yahya Zayd.
Kikosi hicho kimefikia kwenye Hoteli ya Top Five, iliyopo Ntinda, jijini Kampala, Uganda, ambapo muda si mrefu benchi la ufundi linatarajia kutoa programu kamili hadi mwisho wa ziara hiyo itakayomalizika Agosti 15 mwaka huu.
Sunday, August 6, 2017
MR. NICE: SINA NINACHOKIJUTIA KATIKA MAISHA YANGU
HUWEZI kuamini, lakini ndivyo ilivyotokea. Ni kama vile anajutia maisha aliyopitia au kuna mipango inayofanywa na baadhi ya wasanii wenzake kwa lengo la kumwinua tena kimuziki, baada ya kuporomoka kwa kasi ya ajabu na kupoteza umaarufu na utajiri aliokuwa nao miaka kadhaa ya nyuma.
Huyo si mwingine bali ni mkali wa zamani wa miondoko ya Takeu, Lucas Mkenda, maarufu kwa jina la Mr. Nice, ambaye nyota yake ni kama imewashwa upya, kupitia msanii anayetumia lebo ya WCB, Rajabu Abdul 'Harmonize', kwa kumtumia katika somo la kupanda na kushuka kwa maisha ya kila siku ya binadamu.
Harmonize, katika ujio wa wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Sina’, amemtumia Mr. Nice katika video ya wimbo huo kama muigizaji mkuu wa simulizi ya kisa kinachoelezea kushuka kimaisha na kupoteza marafiki pindi mtu anapoishiwa.
Baadhi ya walioishuhudia video hiyo na kuuona ushirikiano huo, wameanza kuamini kuwa, ni kweli mmiliki wa lebo ya WCB, Abdul Naseeb 'Diamond', amedhamiria kwa dhati kumwinua Mr. Nice, ambaye enzi zake alikuwa hashikiki wala kukamatika.
Kuhusika kwa Mr. Nice katika video hiyo na maudhui ya wimbo huo wa Harmonize, ni dhahiri kwamba hayo ni maandalizi ya ujio mpya wa msanii huyo, ambaye kwa miaka mingi sasa amekuwa akiishi na kufanya shughuli za muziki katika nchi jirani ya Kenya.
Ikumbukwe kuwa, Diamond alishaweka wazi kuhusu uwezekano wa kumsaidia Mr. Nice ili kurejesha makali aliyokuwa nayo miaka kadhaa iliyopita na kumfanya awe na jeuri ya matumizi makubwa ya pesa kila mahali alikokwenda kustarehe.
ENZI ZAKE
Enzi zake, Mr Nice alikuwa hakamatiki. Mtindo wake wa muziki alioubuni na kuupa jina la Takeu, ulimfanya awe maarufu katika ukanda wa Afrika Mashariki. Fedha alizozipata zilimfanya awe na kiburi. Matumizi yake yalikuwa hayaelezeki. Alikuwa msanii jeuri.
Muziki wake ulikuwa ukiuza sio mchezo. Maonyesho yake yalikuwa hayana mfano. Katika baadhi ya nchi alizotembelea, alipokewa kama mfalme huku vijana wakiandamana barabarani kumsindikiza.
Kuna wakati alipokwenda Burundi, alipokelewa uwanja wa ndege wa Bujumbura na waziri mmoja wa nchi hiyo huku akitandikiwa zuria jekundu na msafara wake ukisindikizwa na magari ya polisi. Ni msanii pekee wa Tanzania aliyewahi kupata heshima hiyo.
Mr Nice pia alibahatika kutembelea nchi nyingi za Ulaya kwa ajili ya kufanya maonyesho ya muziki. Marekani, Uingereza, Ujerumani, Sweden, Uholanzi, Dubai, Afrika Kusini kote huko alikuwa akijulikana.
Waswahili wanasema fedha fedheha na pia ivumayo haidumu. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Mr Nice. Haikuchukua muda mrefu umaarufu wake kimuziki na utajiri wake vikatoweka ghafla. Hadi leo hajui nini kilichotokea, lakini anaamini hiyo ni mipango ya Mungu, hakuna mkono wa mtu.
Mr Nice aliwahi kukiri kwamba, alikuwa na fedha lukuki, zote zikiwa kwenye akaunti mbalimbali hapa nchini, lakini zote zilitoweka ghafla bila yeye kujua zimetumikaje. Kila anapoyakumbuka yote hayo, machozi huwa yakimtoka.
Ni kutokana na kuporomoka kwake kimuziki na pengine kukimbia aibu iliyoanza kumpata, Mr Nice akaamua kuhamisha makazi yake kutoka Tanzania kwenda Kenya, akiamini kuwa huenda huko mambo yangemnyookea na angeweza kurejesha hadhi yake kimuziki. Lakini sivyo ilivyokuwa.
MIKASA
Alijikuta akikumbwa na masaibu mengi zaidi. Kuna wakati aliwahi kupata ajali ya gari, wenzake wote aliokuwa nao kwenye gari walilokuwa wakisafiria, walifariki, isipokuwa yeye pekee. Ama kweli kama siku yako haijafika, huwezi kufa.
Pia, aliwahi kuzushiwa kifo mara kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuvumishwa kwamba alikuwa na ukimwi, baada ya kulazwa kwenye hospitali moja ya mjini Nairobi kwa zaidi ya mwezi mmoja. Alipoibuka na kueleza ukweli kuhusu afya yake, watu wakabaki vinywa wazi. Hadi leo anadunda akiwa na afya njema kabisa.
Mr. Nice pia aliwahi kupigwa mara kadhaa kwenye kumbi za burudani, kama ilivyokuwa enzi zile alipokuwa na ugomvi usiokwisha kati yake na msanii Dudu Baya. Kuna wakati iliwahi kubainika kuwa, waliompiga walikuwa wakitaka kuharibu sura yake, kisa kikiwa ni kuhusishwa na mke wa mtu.
Alipochoka sana kimaisha, ikavumishwa kwamba, aliamua kuwa dereva wa bodaboda. Pia ilikuwa ikidaiwa alikuwa akilala na kukesha kwenye baa kwa vile hakuwa na sehemu ya kulala.
Hiyo ndiyo historia fupi ya maisha na mikasa iliyowahi kumkuta msanii huyu, ambaye ni mwenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro, aliyezaliwa na kukulia maeneo ya Kinondoni, Dar es Salaam.
HANA ANACHOJUTIA
Licha ya kukutwa na mikasa yote hiyo kimaisha, Mr. Nice anasema hakuna chochote anachokijutia. Anasema kwake kitu majuto hakipo kwa sababu hakuna kitu chochote ambacho hajawahi kukifanya.
"Hata unifanye nini, mimi ni huyu huyu, hakuna kitu kitakachobadilika. Hakuna ninachoweza kujutia," amesema Mr. Nice, alipohojiwa na kituo kimoja cha televisheni hivi karibuni.
Msanii huyo alisema hawezi kueleza bayana ni kiasi gani cha fedha alichowahi kumiliki wakati alipokuwa maarufu kimuziki kwa sababu hiyo ni siri ya maisha yake, hawezi kuitoa mahali popote wala kwa mtu yeyote.
"Hiyo ni siri yangu. Hakuna aliye na ushahidi ni kiasi gani cha fedha nilikuwa nacho,"amesema Mr. Nice.
Aliongeza kuwa, kuweka fedha kwenye buti la gari kama alivyokuwa akifanya wakati akiwa na hali nzuri kimaisha ni jambo la kawaida, lakini akasisitiza kuwa siyo kila anayefanya hivyo, fedha hizo ni zake, wengine hutafuta ujiko.
Mr. Nice anasema watu wengi wanaamini kuwa, alitumia vibaya fedha alizokuwa akizipata, lakini amesisitiza kuwa, 'hajachoka' kama wengine wanavyofikiria.
"Bado ninazo fedha zilezile. Watu hawajui vitu ninavyovimiliki. Pesa niliyonayo ni ileile niliyokuwa nayo wakati ule kwa sababu kuna vitu niliwekeza, lakini watu hawajui,"alisema na kuongeza:
"Ninayo makoloni mengi. Nikishindwa hapa, nafanya kitu kingine. Msanii unapaswa kuwekeza katika mambo mengine, badala ya kutegemea muziki peke yake. Wapo wasanii wamewekeza kwenye vioski na biashara mbalimbali."
Mr Nice anasema msanii anapokuwa juu, anapaswa kutambua kuwa kuna siku ataporomoka, hivyo ni lazima ajiandae kwa hali hiyo.
WITO KWA WASANII
"Wasanii wengi wakishaporomoka, wanachanganyikiwa. Wengine hukimbilia kutumia dawa za kulevya na kujiharibu kabisa. Wanapaswa kujua kuwa, kama kuna kupanda, pia kuna kushuka," amesisitiza.
Ametoa mwito kwa wasanii nchini wasife moyo kwa sababu muziki una kupanda na kushuka na kwamba, pale msanii anapojiona kuwa yuko juu, ajue pia kuwa wakati wowote mambo yanaweza kuharibika akashuka chini. Anasema hali hiyo iko kwa wasanii kote duniani.
Aidha, amewataka wasanii kuwa na upendo na kuacha majungu na unafiki. Amesisitiza kuwa, kile kidogo wanachokipata kutokana na muziki, wanapaswa kuwekeza kwa sababu kuna leo na kesho.
Mr Nice anasema kwa sasa bado yuko katika Jiji la Nairobi nchini Kenya, ambako ndiko ameamua kuendesha maisha yake, isipokuwa amekuja Dar es Salaam, kwa ajili ya kazi maalumu, ambayo hakuwa tayari kuitaja.
"Bado nipo Nairobi naendelea na mambo yangu. Ukijipanga na usipojali, hata kama mambo yamekwenda mrama, unasema mimi ni mimi. Naendelea na muziki na nitakuwa mwanamuziki hadi siku nitakapokufa,"anasema msanii huyo.
Mr. Nice amesema kwa kuwa muziki ni biashara, anaangalia wapi upepo unakokwenda vizuri na hiyo ndiyo sababu iliyomfanya ahamishie makazi yake mjini Nairobi.
"Wengi anajiuliza kwa nini Mr. Nice amehama nchini na kwenda kuishi Kenya. Ninachopenda kuwaambia ni kwamba, upepo wangu upo kule,"amesema.
Hata hivyo, amesema kuna mipango anayoifanya kwa kushirikiana na baadhi ya watu maarufu nchini, lakini amesisitiza kuwa ni mapema kuitaja.
Lakini baadhi ya wadadisi wanaamini kuwa, ujio wake na kushirikishwa kwake kwenye kibao cha Harmonize, ni utekelezaji wa ahadi ya Diamond, kumrejesha tena msanii huyo kwenye chati ya juu kimuziki.
NYIMBO MPYA
Mr. Nice anasema anazo nyimbo nyingi mpya, ambazo ameshamaliza kuzirekodi, lakini bado hajazisambaza kwenye vituo vya redio na televisheni.
"Ninashirikiana na watu fulani, sitaki kuwataja. Tutafanya mambo makubwa, mashabiki wangu wanivumilie, mambo mazuri yanakuja,"amesema Mr. Nice.
FAMILIA
Msanii huyo ana watoto wawili, wa kike na kiume, lakini hapendi maisha yake ya kimuziki yafanane na yale ya kawaida, ndio sababu hapendi kumpangia mtoto wake yeyote kufuata nyayo zake.
"Siwezi kujua kama wanapenda muziki au la, lakini siwezi kuwalazimisha au kuwatembeza kwenye vyombo vya habari ili wajulikane. Sipendi wawe na maisha yanayofanana na ya kwangu,"amesema.
ACHENI KUNIZUSHIA KIFO ILI MUUZE MAGAZETI-MAJUTO
MUIGIZAJI nyota na mkongwe wa filamu nchini, Amri Athumani, maarufu King Majuto, amevitaka vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuacha tabia ya kumzushia kifo kwa lengo la kuuza magazeti.
Amesema amekuwa akichukizwa na tabia hiyo kwa kuwa imekuwa ikiwashtua ndugu, jamaa na marafiki zake kwa kuamini kuwa ni kweli amekufa, hivyo kukusanyika kwa wingi nyumbani kwake kwa lengo la kuhudhuria mazishi.
Majuto, ambaye alianza uigizaji tangu miaka ya 1970, amesema ameshazushiwa kifo zaidi ya mara tano, hivyo kuwataka waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari, kuacha kuchapisha taarifa, ambazo hawana uhakika nazo.
"Kusema kweli haipendezi. Kuweni na taarifa za uhakika, sio hujaipata sawa sawa, lakini kwa sababu unataka kuuza gazeti, unaitoa haraka haraka,"amesema Majuto, alipohojiwa na kituo kimoja cha televisheni hivi karibuni.
"Ninao ndugu zangu wengi nje ya nchi, taarifa hizi ziliwashtua. Kuweni wastaarabu,"amesisitiza msanii huyo, ambaye pia ni mahiri kwa filamu za vichekesho.
Majuto amesema taarifa za hivi karibuni kwamba amekufa, zilitokana na mwandishi mmoja wa habari kusambaza picha zake kwenye mitandao, zikumuonyesha alipokuwa amelazwa kwenye hospitali moja mjini Tanga.
"Wiki moja kabla ya kusambazwa kwa picha hizo, kuna gazeti moja liliandika kwamba nipo hoi, naumwa ngiri wakati sikuwa naumwa. Huyu mwandishi aliyeandika habari hizi ni kama vile alikuwa mchawi wangu kwani haikuchukua hata siku 10, wakati natoka Kenya kufanya maonyesho, nikaanza kuumwa,"amesema King Majuto.
"Wakati nipo hospitali, kuna mtu alinipiga picha, akairusha kwenye gazeti. Wakaweka picha yangu nikiwa mzima nimevaa suti, wakaweka nyingine nikiwa nimelazwa na nyingine ya jeneza na kaburi.
"Nilipoichunguza ile picha ya mazishi na jeneza, nikagundua kwamba zilikuwa picha za mazishi ya marehemu Sharo Milionea. Picha hizi zilitapakaa hadi nje ya nchi. Hapa nyumbani palijaa watu kuja kuzika. Nikaona huu sasa ni mkosi,"amesema msanii huyo, ambaye ameigiza zaidi ya filamu 500.
Majuto amesema kuna wakati aliwahi kuzushiwa kifo alipokwenda kuhiji Makka miaka mitatu iliyopita, jambo ambalo halikuwa la kweli.
"Uzushi ulionikera zaidi ni ule nilipokwenda kuhiji Makka. Nilipofika tu Dubai, nikazushiwa nimefia njiani. Nilipofika Makka, ulitokea upepo mkali, nikazushiwa nimekufa. Tulipokuwa tukijiandaa kutoka Makka kwenda Madina, nikazushiwa tena nimekufa. Wakati wa kurusha mawe kwa shetani, Watanzania 50 walipoteza maisha, nikazushiwa nami nilikufa, wakati sio kweli,"amesema msanii huyo.
Akizungumzia afya yake kwa sasa, Majuto amesema anamshukuru Mungu kwamba anaendelea vizuri na anaweza kurejea katika shughuli zake za kawaida baada ya muda si mrefu.
"Kuishi ukiwa mzima ama ukiwa mgonjwa ni mipango ya Mungu. Nabii Ayubu aliishi karne nyingi akiwa mgonjwa hadi akawa anatoka funza mwilini, lakini akaja kupona,"amesisitiza nguli huyo wa filamu nchini.
"Nikiumwa najua ni sunna, lazima niumwe. Na nikifa ni faradhi, lazima nife. Baba yangu na mama yangu hawapo, hata Rais wangu niliyekuwa nikimpenda, Mwalimu Nyerere hayupo, lazima nife," ameongeza.
Majuto amekiri kuwa, sanaa ya filamu na maigizo ya jukwaani imemwezesha kuwa na maisha mazuri, ikiwa ni pamoja na kumiliki magari, mashamba na kuwasomesha watoto wake katika shule za kulipia.
Amesema hakuna mtoto wake aliyesoma shule ya sekondari ya serikali na kwamba, waliofika chuo kikuu wamemaliza, wanaofanyakazi wanafanya na kusisitiza kuwa, hakuna mtoto wake, ambaye hakuna kitu kichwani.
King Majuto anasema awali, alikuwa akimiliki magari zaidi ya saba, lakini sasa ameyapunguza na kubaki matatu baada ya kuona biashara ya daladala haiendi vizuri.
"Niliamua kuachana na biashara ya daladala kwa sababu mara dereva kaleta hesabu, mara hakuna, nikaona nisije nikapata kichaa,"amesema.
Aidha, King Majuto ameanzisha kampuni yake ya kutengeneza filamu, inayojulikana kwa jina la Kings Movied Ltd na kusisitiza kuwa, hana wasiwasi wa ugali wa watoto kwa kuwa fedha alizonazo, zitaiwezesha familia yake kuishi vizuri hadi atakapoitwa na Mungu.
Akizungumzia maendeleo ya fani ya filamu nchini, amesema wapo wasanii wengi wazuri chipukizi na wenye vipaji vya fani hiyo, lakini hawajiamini. Amewataka kuacha woga na kujituma kwa bidii.
Kabla ya kuwa mwigizaji, King Majuto alikuwa mwajiriwa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na baadaye kujihusisha na kazi ya ulinzi katika kiwanda cha mablanketi na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) miaka ya 1960.
Alianza kupata umaarufu baada ya kujiunga na kikundi cha DDC Kibisa, ambako ndiko alikobatizwa jina la King Majuto, kutokana na kutunga maigizo mengi yanayotia simanzi.
Baadhi ya filamu alizocheza na kupata umaarufu ni Ndoa ya Utata, Daladala Nimekuchoka,Mbegu, Zebra, Shikamoo Mzee, Tabia, Utani, Tikisa, Trouble Maker, Gundu, Kizungunguzu, Shoe Shine, Street Girl, Faithful, Mtego wa Panya, Boss, Back with Tears, Sikukuu ya wajinga, Nyumba nne, Chips kuku,
Kitu bomba, Ndoto ya tamaa, Lakuchumpa na ATM.
Nyingine ni Bishoo, Tupo wangapi, Moto bati, Varangati, Out side, Pusi na Paku, Juu kwa Juu, Swagger, Oh Mama, Jazba, Mke wa mtu sumu, Mbugila, Kidumu, Mkali Mo, Mpela Mpela, Utanibeba, Babatan, Mjomba, Msela wa Manzese, Karaha, Mpango sio matumizi, Mume bwege, Shuga Mammy,
Embe Dodo, Nakwenda kwa mwanangu, Seaman, Naja leo naondoka leo.
MTANZANIA ASHIKA NAFASI YA TATU MBIO ZA DUNIA
MTANZANIA Alphonce Felix Simbu amefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika mbio za dunia za IAAF zinazoendelea kufanyika nchini Uingereza katika Jiji la London.
Simbu ameshika nafasi ya tatu nyuma ya Mkenya aliyeshika nafasi ya kwanza akifuatiw ana Muethiopia aliyeshika nafasi ya pili.
Akitumia masaa 2 na dakika 10 Simbu aliweza kushiuka nafasi ya tatu baada ya kumpita Mkenya mwingine aliyejua kushika nafasi ya tano.
Hii inakuwa ni kwa mara ya kwanza kwa Simbu kushika nafasi ya tatu baaada ya mwaka jana katika mbio ndefu za London Marathonaliweza kushika nafasi ya tano.
YANGA YAICHAPA SINGIDA UNITED 3-2
YANGA imetoka nyuma na kushinda mabao 3-2 dhidi ya wageni wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Singida United mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa wa Taifa Dar es salaam.
Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwa kocha George Lwandamina kukutana na aliyekuwa kipenzi cha wanayanga Mholanzi Hans Van Der Pluijm ambaye anakifundisha kikosi cha Singida United chenye maskini yake mkoani Singida.
Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Kiungo Mzimbabwe, Thabani Scara Kamusoko aliyefunga bao la kwanza kunako dakika ya tano kwa shuti la mpira wa adhabu baada ya mshambuliaji mpya, Ibrahim Hajib kuangushwa umbali wa mita 25.
Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Azam Rwanda kwa misimu yote miwili iliyopita, Dany Usengimana akaifungia Singida United bao la kusawazisha dakika ya nane akitumia vizuri makosa ya nabeki wa Yanga kuchanganyana.
Mshambuliaji Mzimbabwe, Simbarashe ‘Simba’ Nhivi Sithole akaifungia bao la pili Singida dakika ya 23 akitumia tena makosa ya safu ya ulinzi ya Yanga.
Kipindi cha pili, kocha Mzambia wa Yanga alibadilisha karibu kikosi kizima akimtoa hadi kipa Beno Kakolanya na kumuingiza Mcameroon, Yoouth Rostand.
Mabadliko hayo yaliisaidia Yanga kupata mabao mawili dakika za mwishoni, akianza Mrundi Tambwe kusawazisha kwa penalti dakika ya 83 baada ya kipa Said Lubawa kumchezea rafu kiungo chipukizi, Said Juma, kabla ya Martin kufunga la ushindi dakika ya 90
Friday, August 4, 2017
COSAFA YATOA ZAWADI TAIFA STARS, WACHEZAJI
Baraza la Mpira wa Miguu kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (Cosafa), limetoa zawadi ya dola 10,000 kwa Taifa Stars ya Tanzania baada ya kushinda na kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Castle Cosafa yaliyofanyika mwezi uliopita nchini Afrika Kusini.
Fedha hizo ni sawa na Sh. 22,000,000 ambako Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeamua fedha hizo kwa mgawanyo sawa, zitolewe kwa wachezaji wote walioshiriki fainali hizo pamoja na benchi la ufundi.
Kadhalika Cosafa limetuma fedha za zawadi kwa wachezaji wa Tanzania ambao walifanya vema kwenye mchezo mmoja baada ya mwingine katika mashindano hayo ambayo yalikuwa na mvutio wa aina yake kwa mafanikio ya timu ya Tanzania.
Wachezaji hao ni Shiza Kichuya aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Malawi; Muzamiru Yassin aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Angola; Erasto Nyoni aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Mauritius; Elius Maguri aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Afrika Kusini.
Kipa Bora wa michuano hiyo ni Said Mohammed alyezawadiwa moja kwa moja na Cosafa. Tanzania ilishika nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa Zimbabwe na Zambia iliyoshika nafasi ya pili. Tanzania iliifunga Lesotho na kushika nafasi ya tatu.
TFF YAPANGUA MAKUNDI YA LIGI DARAJA LA KWANZA
Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefanya mabadiliko kidogo ya timu zilizo kwenye makundi ya ‘A’ na ‘B’ katika Ligi Daraja la Kwanza (FDL) Tanzania Bara iliyopangwa kuanza Septemba 16, mwaka huu.
Timu ambazo zimefanyiwa mabadiliko ni Polisi Morogoro FC ya Morogoro iliyokuwa kundi ‘A’ sasa itakuwa Kundi ‘B’ wakati Mshikamano FC ya Dar es Salaam iliyokuwa Kundi ‘B’ sasa itacheza mechi mechi zake katika Kundi ‘A’.
Kwa msingi huo, makundi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu yenye timu nane kila kund, zitakazochuana msimu huu wa 2017/18 kuwania nafasi tatu muhimu za kupanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2018/19 yatakuwa hivi:-
Kundi ‘A’ litakuwa na timu za African Lyon, Ashati United, Friends Rangers, Mshikamano za Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga na Mvuvumwa ya Kigoma.
Kundi ‘B’ zitakuwa timu za itakuwa na timu za Coastal Union ya Tanga; JKT Mlale ya Ruvuma; KMC ya Dar es Salam, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufundi United ya Iringa, Polisi Dar za Dar es Salaam na Polisi Morogoro na Mawezi Market ya Morogoro.
Kundi ‘C’ ina timu za Alliance School, Pamba na Toto African za Mwanza, Rihno Rangers ya Tabora, Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma ya Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.
DK.MWAKYEMBE ATAKA KUANZISHWA KWA MFUKO WA WASANII
Na. Neema Mathias na Thobias Robert- MAELEZO
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewahamasisha Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya nchini kuanzisha mfuko wa wasanii kwa lengo la kutatua changamoto ya udhamini inayowakabili.
Waziri Mwakyembe ametoa wito huo leo Jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na Wasanii hao kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) ambacho kilijadili changamoto mbalimbali zinazowakabili Wasanii na namna ya kukabiliana nazo.
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Mwakyembe alisema kuwa kutokana na malalamiko na changamoto mbalimbali zinazowakabili Wasanii, ambazo nyingi zinasababishwa na mikataba inayowanyonya Wasanii katika kazi zao, ni vema sasa Wasanii hao kupitia Chama chao cha Tanzania Urban Music Association (TUMA) kuanzisha mfuko ambao utakua unatoa mikopo kwa Wasanii ili kuwezesha utendaji wa kazi zao pasipo kutegemea wadhamini.
“Ninafikiri dawa tunayohitaji ni kuanzishe mfuko wa Wasanii ambapo kila Msanii atatakiwa kuchangia fedha. Jambo ambalo litawavutia wadau wengine kuchangia mfuko huo na kuwaondoa katika dhana ya utumwa, na mfuko huo utamsaidia msanii aliyejisajili kupata mkopo bila kutozwa riba yoyote,” alielezea Waziri Mwakyembe.
Waziri Mwakyembe alisema kuwa Tasnia ya Sanaa ina mchango mkubwa katika kuongeza pato taifa hivyo ametaka tasnia hiyo kurasimishwa ili kupunguza tatizo la ajira na pia kutumika kama chombo maalumu cha kuielimisha jamii kwani kupitia Sanaa wananchi hupata ujumbe kwa urahisi.
Aidha, Waziri Mwakyembe ameunda Kamati ya kushughulikia masuala yanayowakabili Wasanii ikiwemo sera na sheria ili kuboresha maslahi ya Msanii. Wasanii wanaounda Kamati hiyo ni Azma Mponda, Niki wa Pili pamoja na Witness Mwaijanga.
Katika hatua nyingine Waziri Mwakyembe amelitaka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kufanyia mabadiliko sera ya Sanaa pamoja na baadhi ya vipengele vya sheria ya Sanaa ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia.
“Tunahitaji mabadiliko ya sheria ya sanaa haraka. Katika sheria hiyo ni marufuku mmiliki wa vyombo vya habari kulipwa na Msanii ili kupiga wimbo wake, hakuna nchi katika dunia hii ambayo Msanii anatozwa fedha ili wimbo wake upigwe,” alisisitiza.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Onesmo Kayanda amesema kuwa, ili kuboresha na kukuza tasnia ya muziki nchini ni lazima kuwepo na soko la uhakika la kazi hizo pamoja na tuzo mbalimbali ambazo zitatumika kutia hamasa kwa wasanii.
Hata hivyo Bw. Kayanda ameongeza kuwa sera, sheria na miongozo ya baraza hilo ihuishwe ili kulinda kazi mbaimbali za Wasanii ikiwa ni pamoja na kuanzisha mfumo wa kielektoniki wa kujisajili ili Serikali iweze kupata mapato halisi kupitia biashara ya muziki.
Kikao hicho ni cha kwanza kufanyika tangu Waziri Mwakyembe ateuliwe katika Wizara hiyo ambapo ameeleza kuwa kikao kazi kitakuwa kikifanyika mara kwa mara na atakuwa akikutana na wasanii wa vikundi mbalimbali ili kujadili mambo yanayohusu Wasanii hao.
Thursday, August 3, 2017
SIMBA YATOKA SARE YA BAO 1-1 NA MABINGWA WA AFRIKA KUSINI
SIMBA SC imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na mabingwa wa Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini, Bidvest Wits katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Sturrock Park, Chuo Kikuu cha Afrika Kusini asubuhi ya leo.
Katika mchezo huo wa kujipima nguvu kujiandaa na msimu mpya, Simba SC walikuwa wa kwanza kupata bao, lililofungwa na beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, Erasto Edward Nyoni dakika ya 33 kabla ya wenyeji kusawazisha.
Huo ulikuwa mchezo wa pili wa kirafiki wa Simba katika kambi yake Afrika Kusini kujiandaa na msimu, baada ya Jumamosi kufungwa 1-0 Orlando Pirates.
Baada ya mchezo huo, Simba SC inatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania kwa ajili ya mchezo mwingine wa kujipima nguvu dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda Agosti 8, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
ZFA KUJADILI MFUMO MPYA WA KUPATA TIMU ZA LIGI KUU
Na Sleiman Ussi,Zanzibar
Kamati ya utendaji ya chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar (ZFA) imekutana asubuhi ya leo kujadili masuala kadhaa ikiwemo namna yakupatikana kwa mfumo utakaotumika kuendesha ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu wa 2017-2018.
Akizungumza na wana habari baada yakukamilika kwa kikao hicho msemaji wa chama cha mpira wa miguu visiwani humo,Ali Bakar alisema katika kikao hicho ukiachia suala la usajili na uhamisho kamati imependekeza kukutana na vilabu kupanga mfumo mpya kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
Alisema kwamba ukiachia suala hilo kamati tendaji imelizungumzia suala zima la usajili na uhamisho sambamba na kuvitaka vilabu kulipia ada ya uanachama kwa ramjisi,ada ya mwaka wilayani, sambamba na ada ya mashindano huku akisisitiza kuwa timu itakayoshindwa kufanya hayo haitashiriki katika mashindano kwa msimu ujao.
Kuhusu mfumo uliopitishwa na vilabu kisiwani Pemba afisa habari huyo alisema mfumo ule ulikuja baada ya kupatiwa uanachama wa kudumu CAF lakini kutokana na taarifa zilizokuja hivi karibuni kamati hiyo imeona umuhimu wa kukutana tena na vilabu kutafuta njia mbadala ambayo itasaidia kupata mfumo.
SINGIDA UNITED YATOKA SARE NA RUVU SHOOTING
Timu ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Singida United mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Mabatini ukiwa ni mchezo wa maandalizi ya msimu mpya unaotarajia kuanza Agosti 26.
Ruvu walikuwa wa kwanza kupata bao likifungwa na Full Maganga dakika ya 20 hata hivyo goli hilo halikudumu kwani dakika ya 26 mshambuliaji wa zamani wa Jkt Ruvu Atupele Green aliweza kuisawazishia Singida hadi mapumziko timu hizo zilikwenda zikiwa zimefungana 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hata hivyo hakuna timu ambayo iliweza kupata goli hadi dakika 90 kipyenga kinamalizika timu hizo zilitoshana nguvu sawa kwa kufungana goli 1-1.
Singida United wanatarajia kesho kuwasili jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara Yanga mchezo ambao utapigwa siku ya Jumamosi na unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini kuona kocha wa zamani wa Yanga,Hans Van Der Pluijm anakutana na timu yake ya zamani ambayo ipo chini ya George Lwandamina.
MGOSI AVULIWA UMENEJA SIMBA,APEWA KAZI NYINGINE
*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*
Kikao cha kamati ya utendaji ya klabu ya Simba iliokutana hivi karibuni,imemteua Dr Cosmas Kapinga kuwa Meneja mpya wa Timu ya Simba
Dr kapinga anachukua nafasi ya Mussa Hassan Mgosi ambae amepangiwa majukumu mengine ndani ya klabu.
Kapinga ataanza kazi yake mpya,mara baada ya kikosi cha Simba kurejea nchini kutoka Afrika kusini,ambapo kwa sasa kipo katika maandalizi ya mwanzo wa msimu.
Kwa upande wa Mgosi,sasa atakuwa kocha msaidizi na Meneja wa Timu ya vijana,sambamba na Nico Nyagawa ambae nae atakuwa kocha msaidizi wa kikosi hicho,huku pia akiwa mratibu,Kikosi hicho cha vijana kitaendelea kuwa chini ya kocha mkuu Nico kiondo.
Katikati ya mwezi huu Mussa Mgosi atafanya mafunzo ya ukocha leseni C,ambayo yatampa fursa ya kuongeza ujuzi kwenye majukumu mapya ya ualimu ndani ya timu yetu.
Wakati huo huo,benchi la ufundi la Timu ya Simba,limeridhishwa na maandalizi yao huko Afrika kusini,huku pia likiridhishwa jinsi kikosi cha Simba kilivyocheza jana na Klabu ya Orlando Pirates.
Ingawa tumepoteza mchezo wetu wa jana,lakini tumeshaanza kupata mwelekeo wa kikosi,na katika siku chache zijazo,teyari tutakuwa tushapata kikosi cha kwanza”alisema Mwalimu Omog.
Hapo kesho Timu hiyo itashuka kwenye dimba la Sturrock Park liliopo ndani ya Chuo kikuu cha Wits kilichopo Braamfontein Jijini Johannesburg kucheza mechi ya mwisho ya maandalizi nchini humo,dhidi ya Bidvest.
Timu hiyo ndio mabingwa wa soka nchini Afrika kusini kwa sasa.
IMETOLEWA NA…
*HAJI MANARA*
MKUU WA HABARI SIMBA SC
*SIMBA NGUVU MOJA*
TFF YAZIONYA KLABU ZA LIGI KUU, LIGI DARAJA LA KWANZA
Wakati zimebaki siku nne (4) kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili kwa msimu wa 2017/18, tunazikumbusha klabu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL); timu 24 za Ligi Daraja la Kwanza na 24 Ligi Daraja la Pili kukamilisha usajili kwa Mfumo wa Mtandao wa TMS – Transfer Matching System.
Ikumbukwe kuwa dirisha la usajili linafungwa Agosti 6, mwaka huu na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatoa angalizo kwamba hakuna klabu itakayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kama haitapata leseni ya klabu.
Baadhi ya klabu hazijachukua hata fomu za leseni ya klabu wakati zile zilizochukua kuna baadhi hazijarejesha na pamoja kwamba kuna zile ambazo zimerejesha, lakini baadhi inaonekana hazikujazwa kwa usahihi.
Kikao cha Kamati ya Leseni za Klabu, chini ya Msomi Wakili Lloyd Nchunga kinatarajiwa kuketi Jumamosi Agosti 5, mwaka huu kwenye ofisi za TFF, Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam ambako kitapitia fomu zilizorejeshwa kabla ya kufanya uamuzi wa kutoa leseni kwa klabu zilizotimiza masharti.
Klabu ambayo haitapata leseni kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), haitakuwa na nafasi ya kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kwa msimu wa 2017/18.
Suala la leseni linakwenda pia kwa wachezaji. Kama ilivyokwisha kutangazwa, hakuna mchezaji atakayeshiriki Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili – michuano inayoendeshwa na kusimamiwa na TFF kama hakutimiza masharti ya kupata leseni ya kumruhusu kucheza.
Kuna vigezo sita (6) vya mchezaji kupata leseni ambavyo ni: –
1. Kujazwa fomu ua utimamu wa afya (Medical Form).
2. Bima ya matibabu kwa mchezaji.
3. Barua ya uhamisho (Release Letter).
4. Hati ya Uhamisho wa Kimataifa kwa wachezaji wa kigeni.
5. Mikataba ya wachezaji iliyosajiliwa kwenye mfumo wa usajili TMS
6. Ada ya wachezaji wa kigeni ambayo ni Sh 2,000,000 badala ya dola 2,000 za Marekani.
Wakati hayo yakiagizwa, maandalizi ya ujio mpya wa msimu wa mashindano yanaendelea ambako kwa kesho Alhamisi, Agosti 3, mwaka huu Kampuni ya Vodacom – inayoongoza kwa kutoa huduma za mawasiliano nchini Tanzania itatoa vifaa vya mchezo kwa timu zote 16 za Ligi Kuu ya Vodacom kwa kuwa ndiyo Mdhamini Mkuu wa michuano hiyo yenye ushindani mkali. Vodacom wanafanya hivyo kwa mujibu wa mkataba wa udhamini.
Ikumbukwe kuwa dirisha la usajili linafungwa Agosti 6, mwaka huu na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatoa angalizo kwamba hakuna klabu itakayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kama haitapata leseni ya klabu.
Baadhi ya klabu hazijachukua hata fomu za leseni ya klabu wakati zile zilizochukua kuna baadhi hazijarejesha na pamoja kwamba kuna zile ambazo zimerejesha, lakini baadhi inaonekana hazikujazwa kwa usahihi.
Kikao cha Kamati ya Leseni za Klabu, chini ya Msomi Wakili Lloyd Nchunga kinatarajiwa kuketi Jumamosi Agosti 5, mwaka huu kwenye ofisi za TFF, Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam ambako kitapitia fomu zilizorejeshwa kabla ya kufanya uamuzi wa kutoa leseni kwa klabu zilizotimiza masharti.
Klabu ambayo haitapata leseni kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), haitakuwa na nafasi ya kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kwa msimu wa 2017/18.
Suala la leseni linakwenda pia kwa wachezaji. Kama ilivyokwisha kutangazwa, hakuna mchezaji atakayeshiriki Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili – michuano inayoendeshwa na kusimamiwa na TFF kama hakutimiza masharti ya kupata leseni ya kumruhusu kucheza.
Kuna vigezo sita (6) vya mchezaji kupata leseni ambavyo ni: –
1. Kujazwa fomu ua utimamu wa afya (Medical Form).
2. Bima ya matibabu kwa mchezaji.
3. Barua ya uhamisho (Release Letter).
4. Hati ya Uhamisho wa Kimataifa kwa wachezaji wa kigeni.
5. Mikataba ya wachezaji iliyosajiliwa kwenye mfumo wa usajili TMS
6. Ada ya wachezaji wa kigeni ambayo ni Sh 2,000,000 badala ya dola 2,000 za Marekani.
Wakati hayo yakiagizwa, maandalizi ya ujio mpya wa msimu wa mashindano yanaendelea ambako kwa kesho Alhamisi, Agosti 3, mwaka huu Kampuni ya Vodacom – inayoongoza kwa kutoa huduma za mawasiliano nchini Tanzania itatoa vifaa vya mchezo kwa timu zote 16 za Ligi Kuu ya Vodacom kwa kuwa ndiyo Mdhamini Mkuu wa michuano hiyo yenye ushindani mkali. Vodacom wanafanya hivyo kwa mujibu wa mkataba wa udhamini.
YANGA, SINGIDA UNITED SASA KUKIPIGA JUMAMOSI
Ile mechi ya kirafiki ya Yanga na Singida United iliyopangwa kuchezwa Agosti 6 imerudishwa siku moja ili kupisha shughuli za kiserikali.
Rasmi mchezo huo utapigwa Agosti 5 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam ikiwa ni pamoja na utambulisho wa wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu tayari kwa mikikimikiki ya Ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao.
Singida United ambao wamepanda daraja msimu huu tangu waliposhuka daraja mwaka 2002 nao watajipima na mabingwa mara tatu mfululizo wa Vpl kwenye tarehe hiyo ambayo tayari imethibitishwa
DIDA AANZA KUPIGA MZIGO AFRIKA KUSINI
Kipa wa zamani wa Yanga, Deogratius Munish ‘Dida’ amesajiliwa na klabu ya Chuo Kikuu cha Pretoria.
Timu hiyo maarufu kama Tuks FC inashiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Afrika Kusini.
Mara ya mwisho iliteremka daraja kutoka Ligi Kuu Afrika Kusini maarufu kama ABSA Premiership baada ya kushika nafasi ya 15 ilikuwa ni msimu wa 2015-16.
Timu hiyo maarufu kama Tuks FC inashiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Afrika Kusini.
Mara ya mwisho iliteremka daraja kutoka Ligi Kuu Afrika Kusini maarufu kama ABSA Premiership baada ya kushika nafasi ya 15 ilikuwa ni msimu wa 2015-16.
SIMBA YACHAPWA 1-0 NA ORLANDO PIRATES MECHI YA KIMATAIFA YA KIRAFIKI
Simba imechapwa kwa bao 1-0 katika mechi yake ya kwanza ya kirafiki baada ya maandalizi ya msimu wa 2017-18.
Simba imelala kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wake Orlando Pirates katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Orlando jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
MTIBWA SUGAR YAPATA MRITHI WA MBONDE,ASAINI MIAKA MIWILI
Timu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro baada ya kuondokewa na beki wao kisiki Salum Mbonde aliyejiunga na Simba hatimaye leo wameingia mkataba na beki wa African Lyon Hassan Suleiman Isihaka.
Timu hiyo inayomilikiwa na kiwanda cha Sukari bora nchini Mtibwa Sugar kilichopo Turiani, imefanikiwa kunasa saini ya beki huyo ambaye msimu uliopita aliichezea kwa mkopo African Lyon ya Dar es Salaam.
Hata hivyo, baada ya African Lyon kuteremka Daraja msimu uliopita, Isihaka akafikia makubaliano maalum ya kuvunja mkataba na Simba ili awe huru na hivyo kufanikiwa kujiunga na Mtibwa Sugar
Ujio wa beki huyo ni pendekezo la benchi la ufundi la Mtibwa Sugar linaloongozwa na Zuberi Katwila.
“Kiukweli usajili huu niliusubilia kwa hamu yote kubwa nadhani kila kocha anatamani kuwa na mchezaji huyu nadhani bahati imedondokea kwa Mtibwa Sugar , pia natoa shukrani za dhati kwa viongozi kwa kufanikisha usajili huu maana ulikua wa muhimu sana kwangu,” amesema Katwila.
Kwa upande wake. Isihaka amesema kwamba alikua anatamani kufanya kazi na ‘Wana Tam Tam’ kwa muda mrefu; “Nilikua natamani kufanya kazi na Mtibwa Sugar kwa muda mrefu na ninadhani nimefanikiwa kwa kuwa ni klabu kubwa na wachezaji wengi nchini wakubwa wamepita hapa,” amesem Isihaka.
Isihaka anakuwa mchezaji mpya wa saba kusajiliwa na Mtibwa Sugar dirisha hili, wengine wakiwa ni kipa Shaaban Hassan Kado, mabeki Salum Kanoni kutoka Mwadui, Hussein Idd Hante kutoka JKT Oljoro, viungo Hassan Dilunga kutoka JKT Ruvu na washambuliaji ni Riffat Khamis Msuya kutoka Ndanda FC na Salum Ramadhani Kihimbwa ‘Chuji’.
Subscribe to:
Posts (Atom)




















