KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, August 2, 2012

MWAMUZI MSTAAFU MSAFIRI MKEREMI AFARIKI DUNIA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mwamuzi wa zamani wa kimataifa Msafiri Mkeremi kilichotokea leo alfajiri (Agosti 2 mwaka huu) kwenye Hospitali ya Wilaya ya Urambo mkoani Tabora.
Licha ya kuwa mwamuzi, Mkeremi aliwahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) sasa TFF kwa vipindi viwili tofauti. Pia aliwahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT).
Vilevile aliwahi kuwa mkufunzi wa waamuzi, mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) Mkoa wa Pwani.
Kwa upande wa vyama vya mpira wa miguu aliwahi kuwa kiongozi katika mikoa ya Tabora, Pwani na wilayani Mpanda katika Mkoa wa Rukwa.
Msiba wa Mkeremi uko nyumbani kwake Urambo, na kwa mujibu wa mtoto wake Masoud Mkeremi, atazikwa Jumamosi kwenye makaburi ya Msafa yaliyoko wilayani Urambo.
TFF inatoa pole kwa familia na kuitaka kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. Pia TFF itatoa ubani wa sh. 200,000 kwa familia ya marehemu kama rambirambi zake.
Marehemu aliyekuwa akisumbuliwa na presha na ugonjwa wa kisukari ameacha wajane wawili na watoto 12. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Amina

LISA JENSEN AFANYA VIZURI MISS WORLD 2012

MWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Miss World, Lisa Jensen ameanza kufanya kweli katika michuano hiyo baada ya kufanikiwa kuingia kumi bora ya shindano la Top Model, hivyo kumuongezea pointi zaidi kabla ya fainali za kinyang’anyiro hicho.
Habari zilizopatikana kutopka Mongolia ambako shindano la Miss World litafanyika, zimepasha kuwa Lisa alikuwa mwiba mchungu kwa washiriki wengine kutokana na uwezo wake mkubwa, huku akionesha kipaji cha aina yake katika shindano hilo lililofanyika juzi usiku nchini humo. Akithibitisha habari hizi, Afisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania, Haidan Ricco alisema Lisa ni mmoja kati ya wawakilishi watatu kutoka Bara la Afrika ambao wamefanikiwa kupenya na kuingia katika nafasi hiyo muhimu.
Waafrika wengine waliofanikiwa kupenya katika kumi bora ya shindano hilo kabla ya siku ya fainali ya Miss World ni mrembo wa Afrika Kusini na Shelisheli. Lisa amefanikiwa kufanya kweli na kuwatoa kimasomaso Watanzania ambao kwa sasa wanajikuta katika hali mbaya kutokana na wanamichezo wake waliopo katika Michuano ya Olimpiki wakifanya vibaya.
Kutokana na kuingia kumi bora, Lisa bado ana kazi kubwa ya kuhakikisha anapambana ndani ya wiki hii wakati mshindi wa Top Model atakaposakwa rasmi. “Kwetu sisi ni faraja kubwa mno, kwani tunaamini Lisa ataiwakilisha vema Tanzania na huu ni mwanzo mzuri kwake,” alisema Ricco, huku akitaka Watanzania wamuombee kabla ya kufanyika shindano la Miss World hapo Agosti 18, ili aweze kufanya kweli.
Shindano la Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s, ambacho kinazalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania.

AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU SHULE YA SEKONDARI KISAWASAWA KIROMBERO, MOROGORO

Kisawasawa Secondary School Headmaster in Morogoro, Menasi Msigwareceiving books donation from Dangio Kaniki Airtel Public relationsand Event Officer second while from left looking on is Airtel Publicrelations and Event Officer Dangio Kaniki.

Airtel Public relations and Event officer Dangio Kaniki leftchallenging one of the students in Kisawasawa Secondary School duringthe book handover ceremony held at Kisawasawa Secondary school inMorogoro, behind left is Corporate Social and Responsibility ManagerHawa Bayuni, second left is Headmaster of Kisawasawa Secondary SchoolMenasi Msigwa followed by Airtel Sales Officer Mohammed Mbamba.

Airtel Public Relations and Event Officer Dangio Kaniki (left) makinga point during the book handover ceremony in Kisawasawa SecondarySchool in Morogoro, left is the Corporate Social and ResponsibilityManager Hawa Bayuni and right is the Headmaster of Kisawasawa PrimarySchool Menasi Msigwa.


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kupitia mpango wake wa 'Airtel shule yetu' imetoa vitabu vya ziada na kiada kwa shule ya sekondari Kisawasawa ya mkoani Morogoro lengo likiwa ni kusaidiamaendeleo ya elimu mkoani hapo na kutoa huduma kwa jamii.
Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika shule ya sekondariKisawasawa na kuhudhuriwa na wawakilishi wa shule, wanafunzi,waandishi wa habari na wafanyakazi wa Airtel ambapo vitabu vyenyethamani ya shilingi milioni mbili vilikabidhiwa kwa shule hiyo.
Akiongea wakati wa halfa ya makabidhiano ya vitabu hivyo, AfisaUhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki alisema, " Airtelinatambua kuwepo kwa uhaba wa vitabu na vifaa vya kufundishia katikashule zetu na katika kutatua changamoto hizo tunaongeza nguvu nakushirikiana na Serikali chini ya wizara ya elimu kuweza kuinua sektaya elimu.
"Tunafahamu umuhimu wa elimu katika kujikwamua na umaskini, hali ngumu ya maisha na kupata nguvu kazi ya kesho, kwa kutoa kipaumbele kwakusaidia na kuhakikisha nyenzo muhimu za kufandishia zinapatikanamashuleni ili kuweza kufikia dhamira yetu ya kusaidia jamii kwa ujumlaAirtel inatoa fulsa sawa kwa shule zote nchini na leo tumewafikiawanafunzi wa Kisawasawa Kilombero Morogoro. Tunaamini elimu ndioufunguo wa maisha hivyo tunayo malengo ya dhati kabisa katika kusaidiakuinua kiwango cha elimu.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari ya Kisawasawa bw,Menasi Msigwa ameishukuru Airtel kwa kuwawezesha kupata vitendeakazi na kuongeza kuwa shule hiyo bado inakabiliwa na changamotonyingi katika elimu hivyo kuiomba kampuni hiyo kuendelea kuisaidiakatika mambo mengine.
Aidha alichukua fulsa hiyo kuwaasa wanafunzi kutumia na kuvitunzavitabu hivyo ili viweze kusomwa na wanafunzi wengi zaidi na kuongezakiwango cha kufaulu katika shule hiyo. Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, wiki iliyopita Airtel ilitoa msaada wa Vitabu kwa shule ya Mtipwa iliyopo mkoa wa Singida.
Tangu Airtel ilipoanza mpango wa kusaidia vitabu kwa shule mbali mbaliza sekondari hapa nchini, takribani miaka saba iliyopita,imeshazifikia zaidi ya shule za sekondari tofauti zipatazo 1,000nchini Hii ikiwa nikatika kurudisha faida inayoipata na kuchangiakatika huduma kwa jamii.

AZAM YAMLIPUA NGASA, YAMWAMBIA AENDE SIMBA AMA ASUGUE BENCHI MWAKA MZIMA

Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa ya ufafanuzi juu ya sakata la mchezaji Mrisho Ngasa ambalo linaonekana kupotoshwa

1. Azam FC ilitangaza kuwa biashara ya mchezaji Mrisho Ngasa ingefungwa siku ya Jumatano 1/08/2012 saa saba mchana na ilivitaka vilabu vyenye interest na mchezaji huyo kufika makao makuu ya Azam FC ofisi ndogo zilizopo kwenye kiwanda cha unga cha Azam-Mzizima zikiwa na pesa taslimu. Bei ya mauzo iliyopangwa ilikuwa ni Dola 50,000. Lakini katika mawasiliano ya email kwa makatibu wakuu wa Simba na Yanga, Azam FC iliweka bayana kuwa ilikuwa tayari kushusha bei ya mauzo na ingemuuza Ngasa kwa timu ambayo dau lake lingekuwa kubwa zaidi ya mwenzake. Kwa maana hiyo biashara ya mchezaji mrisho ngasa ilifanyika kwa uwazi. Lengo la Azam FC lilikuwa ni kutoa haki kwa kila klabu yenye uwezo wa kifedha kuweza kupata huduma ya Ngasa. Pia tunaomba ifahamike bayana kuwa mchezaji Mrisho Ngasa alipewa taarifa kuwa anauzwa na aliombwa asaidie kushawishi klabu anayoitaka ifike kwetu na ofa yake. Ngasa alitamka bayana kuwa yupo tayari kwenda klabu yoyote ambayo Azam FC itaona imekidhi mahitaji yake kwa masharti kuwa maslahi yake ya kimkataba kati yake na Azam FC yazingatiwe.

2. Hadi kufikia siku ya Jumatano 01/08/2012 saa saba mchana. Ni klabu ya Simba pekee iliyojibu kwa maandishi na kuonesha nia ya kumchukua Ngasa. Yanga wao hawakuwahi kujibu email, ingawa kwa majibu ya simu Mjumbe wao wa Kamati ya usajili Bw Sefu Magari alitangaza kuwa Ngasa hana thamani ya zaidi ya milioni 20. Na Yanga haikuwa tayari kuboresha ofa yake.

3. Muda wa kufungwa kwa biashara ya kumuuza Ngasa ulipofika, ni simba pekee kupitia kwa makamu Mwenyekiti wake Bw Geofrey Ngange na Mhasibu wake ndiyo waliofika wakiwa na pesa taslimu shilingi milioni 25. Yanga hawakuonekana na hawakutaka kupokea hata simu walizokuwa wakipigiwa kuulizwa kama wana interest.

4. Kikao cha dharura cha Azam FC kilikaa na kuamua kuwa biashara ya kumuuza Ngasa ilishindikana kutokana na kutokupatikana kwa mnunuzi mwenye dola 50,000. Kwa maana hiyo Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopo kwenye klabu iliyofika na kuonesha nia ya kumhitaji (Simba)

5. Simba walipewa sharti la kuhakikisha wanamlipa Ngasa mshahara wake kamili (TZsh 2,000,000) pamoja na stahiki zake nyingine zote za kimkataba

6. Sababu za kumpeleka Ngasa kwa mkopo ni kumuepusha na adhabu ambayo klabu ya Azam FC ingetoa kwa Ngasa kama angebaki.

7. Azam FC inapenda kuweka wazi kuwa haijamlazimisha Ngasa kwenda Simba kama inavyopotoshwa. Kama Ngasa anataka kuvunja mkataba wake au kama Yanga bado wanamhitaji basi waje na dola 50,000 na Azam FC itawauzia kwani licha ya kwamba amepelekwa kwa mkopo simba lakini Ngasa bado ni mali ya Azam FC

8. Tunaomba kuweka msimamo wetu kuwa hatupo tayari kumlipa Ngasa na kuvunja mkataba wake na hatuna sababu ya kufanya hivyo. Kama Ngasa hataki kwenda tunakompeleka Azam FC inamruhusu kubakia klabuni na kutumikia adhabu.

9. Lakini Ngasa na washauri wake waelewe kuwa akiamua kubaki Azam FC atakaa nje ya uwanja kwa muda wote uliosalia kwenye mkataba wake, kwani Azam FC haipo tayari kumvisha jezi mchezaji anayefanya vitendo vya utovu wa nidhamu.

10. Kwa kuwa Sakata hili limeanza kuhusishwa na sakata la Mchezaji ramadhani Chombo. Naomba nitoe ufafanuzi kama ifuatavyo. Redondo alipewa option tatu za kuchagua baada ya kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu timu ilipokuwa safarini Mwanza.a. Kupelekwa kwa mkopo Moro United?b. Kupatikana kwa mnunuzi mwenye shilingi milioni 40c. Kukubali adhabu ya kufungiwa kwa miezi mitatu na kulipwa nusu mshahara wahati akitumikia adhabu.Redondo alithibitisha kuipenda Azam FC kwa kukataa kuuzwa au kupelekwa kwa mkopo. Alikubali kutumikia adhabu yake na ilipoisha alirudi na kuomba msamaha na sasa ni mmoja kati ya wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu sana.

Azam FC inajivunia kuwa na mchezaji kama Redondo na bila kupepesa macho wala kung’ata maneno. Azam FC inamchukulia Redondo kama mtu spesho na mwenye mapenzi ya dhati na klabu yake na inamtaka aendelee kuwa na moyo huo.

Imetolewa na utawala.

Azam FC

EBSS YAFUNIKA DAR












Hivi ndivyo hali ilivyokuwa jana baada ya usaili kwa ajili ya shindano la Epiq Bongo Star Search ulipobisha hodi katika Jiji la Dar es Salaam.

Wednesday, August 1, 2012

NGASA AIKANA AZAM KUMUUZA SIMBA

Muda mchache uliopita tumefanikiwa kufanya mazungumzo na mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Ngassa ambaye klabu yake Azam leo imethibitisha kwamba ameuzwa kwenda klabu ya Simba.
Katika mazungumzo hayo Mrisho Ngassa amesema kwamba yeye binafsi hajapata taarifa rasmi kutoka kwa klabu yake ya Azam juu ya kuuzwa kwenda Simba.

"Kiukweli hizo taarifa mie nazisikia na kusoma kwenye mitandao tofauti lakini muajiri wangu bado hajanipa taarifa rasmi juu ya hili suala. Pia huu utaratibu sidhani kama ni sahihi, wanawezaje kuniuza timu nyingine bila kunihusisha, vipi kuhusu maslahi yangu katika hiyo timu nyingine nani ameyasimamia? Kwa maana hii bado nashindwa kuamini kama Azam watakuwa wamefanya hivyo. Ilipaswa wanipe taarifa kwamba Ngassa tunakuuza kwenda timu fulani na nina haki ya kuchagua kukubali au kukataa.
Ngassa akaendelea alivyoondoka Yanga, "Mimi sitaki kuondoka Azam huku kukiwa kuna hali ya kutokuelewana kati yangu na wao pamoja na wapenzi na mshabiki wa klabu hiyo ambao wamekuwa wakinisapoti kwenye kipindi chote nilichokaa pale. Unaweza ukajiuliza kwanini mimi mpaka leo kwanini mashabiki wa Yanga wanaonyesha mapenzi kwangu au ninakuwa na ukaribu nao, ni kwa sababu wakati naondoka Yanga nilipewa baraka zote na klabu yangu, yaani niliondoka vizuri.

Azam walikuja wakaongea na Yanga wakakubaliana na ada ya uhamisho then na mie nikapewa taarifa nikakaa chini na Azam tukakubalina mahitaji yangu binafsi sasa iweje leo wao wameshindwa kufuata utaratibu ule ule ambao waliufuata wakati wa kuninunua kutoka Yanga. Ilipaswa wao kabla ya kukubaliana na Simba ingebidi na mie nipewe taarifa ili kuweza kukubaliana mahitaji yangu binafsi na Simba then ndio niuzwe. lakini sivyo walivyofanya."
Alipoulizwa kama Simba wakimpa vile anavyovitaka atakuwa tayari kuichezea klabu hiyo, Ngassa alijibu, "Mpira ni kazi yangu, ninafanya hii kazi ili kuweza kujikimu kimaisha maisha. Kama klabu yoyote ikikubali kunipa mahitaji yangu niyatakayo na nikapendezewa nayo nitajiunga nayo. Taratibu lazima zifuatwe na kuniuza kama kiroba cha mchele, kwa hali ilivyo mpaka sasa sitoweza kujiunga na Simba"
By Aidan Charlie

NGASA AUZWA SIMBA KWA MIL 25

Hatimaye klabu ya Azam FC ya Tanzania imemuuza mshambuliaji wake Mrisho Khalfan Ngassa kwenda klabu ya Simba SC.
Azam, ambao walimsaini Ngassa kwa ada iliyovunja rekodi ya uhamisho kwa wachezaji wanaocheza Bongo, Million 55, wamemuuza Ngassa kwa ada ya millioni 25 iliyolipwa cash na mabingwa wa Tanzania, Simba.
Akizungumza na mtandao huu,Meneja wa Azam, Patrick Kahemele amesema kamati ya ufundi ya klabu pamoja na uongozi walikubalina kumuweka sokoni Mrisho Ngassa mara tu baada ya kumalizika kwa michuano ya Kagame Cup ambayo iliisha kwa Azam kushika nafasi ya pili nyuma ya Yanga.
"Klabu iliamua kumweka sokoni Ngassa mara tu baada ya michuano ya Kagame kumalizika, kwa kuwa mwenyewe alionesha nia ya kujiunga na klabu yake ya zamani Yanga, sisi tuliwapa kipaumbele Yanga, lakini pia Simba nayo ilionesha nia ya kumtaka. Tukafungua bid na kutangaza tunahitaji $50,000. Yanga baada ya kuwajulisha juu ya hili wakatuma ofa ya millioni 20, Simba nao wakatuma millioni 25. Ofa zote zilikuwa chini ya kiasi tulichohitaji lakini baada ya majadiliano ya viongozi wote wa Azam tukaona bora tumuuze tu, kwa bei ya millioni 25.
"Kwa kuwa Simba walikuwa wameshafikia viwango na sisi lengo letu lilikuwa ni kumuuza Yanga, asubuhi ya leo tukawatumia email Yanga tukiwaambia waboreshe ofa yao na tukawaambia bid ya Ngassa itafungwa saa saba mchana, lakini hadi muda huo unafika Yanga hawakuwa wametujibu chochote, kitendo ambacho tulikitafsiri hawana nia ya dhati ya kumsaini mchezaji huyo, kwa upande mwingine Simba walikuwa tayari wamefikia dau tulilolitaka hivyo tukafunga bid na kumuuza mchezaji huyo kwa Simba," alimaliza Patrick.
Tunaendelea kumtafuta Mrisho Ngassa na pale tutakapompata tutawaletea taarifa rasmi kuhusu alivyopokea taarifa za kuuzwa Simba.
By Aidan Charlie

AZAM YAMTIMUA STEWART HALL

Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa kuwa mkataba wake na kocha Stewart John Hall kutoka nchini uingereza ulisitishwa rasmi jana Tarehe 31/07/2012 kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Klabu ya Azam FC inajivunia mafanikio ya kocha Stewart Hall, na inampongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya katika muda wote aliofanya kazi kama kocha mkuu na mkurugenzi wa ufundi.
Chini ya Stewart Hall, Azam FC ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mapinduzi Cup, Kushika nafasi ya pili katika ligi kuu, Mashindano ya Urafiki na Kombe la kagame. Haya ni mafaniko ambayo hayajawahi kufikiwa na makocha wote waliotangulia na ni mafaniko ya kihistoria katika klabu ya Azam FC.
Azam FC inamtakia kocha Stewart Hall kila la heri, na inatarajia kuwa ipo siku katika siku za usoni kocha Stewart atarudi tena kufanya kazi na Azam FC.
Stewart Hall anaacha changamoto kubwa sana kwa mrithi wake ambaye atatangazwa hapo baadaye lakini kizuri ni kuwa, mrithi wa Stewart Hall atakuwa ni mwalimu anayefuata mfumo ule ule wa uchezaji ulioachwa na Stewart Hall kwani hiyo ndiyo (Playing Philosophy ya Azam FC) Kwa sasa timu itakuwa chini ya Vivek Nagul na Kally Ongala
Azam metolewa na Utawala

TFF YARIDHIA LIGI KUU KUENDESHWA NA KAMPUNI

KWA mara ya kwanza Ligi Kuu Bara itaandika historia msimu ujao, ambapo sasa itasimamiwa na kuendeshwa na kampuni, 'Tanzania Premium League' (TPL). Hatua ya kupitisha mabadiliko hayo, ilifikiwa katika kikao cha siku mbili cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Akizungumza jana, mwenyekiti wa kamati ya kuendesha mchakato wa kampuni, Wallace Karia alisema TFF imepitisha kampuni kuwa chombo huru cha kuendesha ligi hiyo itakayoanza rasmi Septemba Mosi mwaka huu.
"Tulichokuwa tunatofautiana na TFF juu ya ligi kuendeshwa na chombo huru, lakini sasa kamati ya utendaji imetoa baraka," alisema Karia."Kuna mambo madogo ya kufanyiwa mabadiliko, hata hivyo hali hiyo siyo kikwazo cha ligi kusimamiwa na chombo huru," aliongeza Kiria.
Karia alisema baadhi ya maeneo ya kufanyiwa marekebisho ni suala la muundo wa kisheria wa uendeshaji ligi na kasoro ndogo walizozibaini awali.
Kimuundo kutakuwa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa TPL, kiongozi wa juu wa klabu iliyoshinda Ligi Kuu msimu uliotangulia.
Pia kutakuwa na Makamu Wenyeviti wa Bodi watatu, ambao ni viongozi wa juu wa timu mbili zilizoshika nafasi ya pili na tatu na Makamu wa pili wa Rais wa TFF anayewakilisha klabu.
"Pia bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Ligi Kuu inahusisha wenyeviti au wakurugenzi au kiongozi wa juu wa klabu zote 14 (16) zinazocheza Ligi Kuu, ambapo kila klabu itatoa mjumbe mmoja na TFF pia itakuwa na hisa kwenye kampuni.
Wajumbe wengine wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya ligi ambao hawatapiga kura ni mjumbe mmoja kutoka Chama cha Wanasoka wa Kulipwa, Chama cha Waamuzi (FRAT), Chama cha Makocha (TAFCA0 na Wadhamini wa Ligi Kuu.
"Kutakuwa na kamati huru ya nidhamu na rufaa ambayo itateuliwa na Bodi ya wakurugenzi ya TPL kila mwaka. Maamuzi ya kamati hii yatapaswa kutekelezwa na klabu zote zinazoshiriki Ligi Kuu lakini yanaweza kupigwa kwenye Kamati ya Nidhamu na Rufaa ya TFF," aliongeza Kiria.
Uhusiano kati ya TPL na TFF utaruhusu Makamu wa pili wa Rais TFF kuwa makamu wenyeviti wa bodi ya wakurugenzi wa TPL.
Aidha, uchaguzi wa makamu wa rais wa TFF utafanywa na Bodi ya Wakurugenzi wa TPL au UTAFOC na kiongozi huyo atapaswa kuwa ama kiongozi wa juu wa klabu ya Ligi Kuu au Ligi Daraja la Kwanza au mmoja wa wanahisa wa Klabu inayoshiriki Ligi Kuu au Daraja la Kwanza.
Kuhusiana na mapato ya milango ambayo kwa sasa TFF inachukua asilimia 10, TPL itapaswa kutoa asilimia ya hisa za TFF kutoka pato lake na klabu zitapaswa kutoa asilimia tano (5%) pato la milangoni.
Kuhusu kumiliki hisa za kampuni, klabu zote zinazocheza Ligi Kuu zitakuwa na hisa sawa kwenye kampuni, ambazo zitapatikana kutokana na klabu kuwa mwananchama, na iwapo iwapo itashuka daraja, hisa zake zitahamia kwa klabu iliyopanda daraja.
Wakati huohuo, klabu zote 14 zinazoshiriki Ligi Kuu zinatarajia kufanya kikao leo kwenye ukumbi wa JB Delmont, ambapo moja ya ajenda ni kujadili kwa kina suala la kampuni hiyo.Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Yanga, Mwesigwa Celestine alikiri kuwapo kwa mkutano huo leo.
Msemaji wa Shirikisho la soka nchini, TFF, Boniface Wambura hakukataa wala kukubali taarifa hizo zaidi ya kusema wakati kikao cha Kamati ya Utendaji kinakutana, yeye hakuwepo ofisini.
Source: Mwananchi

21 WATEULIWA TAIFA STARS, CHUJI AREJESHWA, BAHANUZI MPYA

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Agosti 1 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kwa ajili ya mechi ya kirafiki itakayochezwa ugenini Agosti 15 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti kambi kwenye hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam, Agosti 8 mwaka huu saa 1 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza siku inayofuata.
Makipa walioitwa kwenye kikosi hicho ni Deogratias Munishi (Azam), nahodha Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni nahodha msaidizi Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Moshi (Simba), Mrisho Ngassa (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Ramadhan Chombo (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Wachezaji wanaounda safu ya ushambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Said Bahanuzi (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).

Tuesday, July 31, 2012

AUNTY EZEKIEL KUFUNGA NDOA OKTOBA

ILE kasumba kwamba hakuna msanii wa bongo muvi anayeweza kuolewa na kudumu ndani ya ndoa, inatarajia kufutwa na msanii Aunty Ezekiel, ambaye anatarajia kufunga ndoa mwezi October mwaka huu, na mpenzi wake anayeishi Dubai ambako ndiko atakoenda kuishi baada ya kufunga ndoa.
Mtandao , ulifanya mazungumzo mafupi na msanii huyo juu ya maisha yake na filamu kwa ujumla ambapo, alisema kuwa ameamua kuchukua maamuzi hayo ya kutaka kufunga ndoa kwani anahitaji kuishi na mtu ambaye wataweza kupanga naye maisha.
Alidai kuwa mpenzi wake huyo ni Mtanzania ingawa anaishi nje, ambapo anaamini baada ya kufunga ndoa na yeye anataweza kwenda kufanya kazi huko.
“Nilikuwa kimya juu ishu hii lakini nachotaka kusema ni kwamba mambo yangu sasa yameanza na nimeamua kufunga ndoa, hivyo mashabiki wangu nahitaji nao waweze kujua kuwa sasa nimeamua kuchukua maamuzi hayo,” alisema.
Ezekiel alisema kuwa vikao vya harusi na kupanga itakavyokuwa wameshaaza kukaa, kwani wameanza Jumapili.
Aliongeza kuwa mbali na mchakato huo mkubwa pia mwaka huu wa 2012 kampuni yake inatarajia kufunga mwaka kwa kutoa filamu mbili ambazo anaamini zitakuwa moto wa kuotea mbali.
CHANZO CHA HABARI;ODAMA1.BLOGSPOT

NGORONGORO, NIGERIA ZAINGIZA MIL 12/-

Mechi ya kwanza ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 kati ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Nigeria (Flying Eagles) iliyochezwa juzi (Julai 29 mwaka huu) imeingiza sh. 12,901,000.
Fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 3,377 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo lililochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Sehemu iliyoingiza watazamaji wengi ilikuwa viti vya bluu na kijani ambapo 2,697 walikata tiketi kwa kiingilio cha sh. 3,000 kila mmoja. Viingilio vingine katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B, na sh. 15,000 kwa VIP A iliyoingiza watazamaji 21.
Mgawanyo wa mapato hayo ni kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ilikuwa sh. 1,967,949.15, gharama ya kuchapa tiketi sh. 2,250,000, gharama za waamuzi na kamishna wa mechi hiyo sh. 760,000 na ulinzi na usafi kwa Uwanja wa Taifa sh. 2,350,000.
Malipo kwa Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000, asilimia 20 ya gharama za mchezo ni sh. 714,610.17, asilimia 10 ya uwanja sh. 357,305.08, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 178,652.54 na asilimia 65 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 2,322,483.05.
Mechi ya marudiano ya michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Algeria itachezwa Agosti 12 mwaka mjini Ilorin, Jimbo la Kwara, Nigeria.
PONGEZI KWA UONGOZI MPYA SIREFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida (DOREFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Julai 28 mwaka huu.
Ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa SIREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Singida.
TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya SIREFA chini ya uenyekiti wa Baltazar Kimario ambaye amechaguliwa kwa mara ya kwanza.
Uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu mkoani Singida kwa kuzingatia katiba ya SIREFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya SIREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo uliofanyika Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Singida ni Baltazar Kimario (Mwenyekiti), Hussein Mwamba (Katibu Mkuu), Gabriel Gunda (Katibu Msaidizi), Gabriel Mwanga (Mhazini), Hamisi Kitila (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Omari Salum (Mwakilishi wa Klabu TFF), Yagi Kiaratu na Dafi Dafi (wajumbe wa Kamati ya Utendaji).
Nafasi za Makamu Mwenyekiti, Mhazini Msaidizi na wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji zitajazwa katika uchaguzi mdogo utakaofanyika baadaye.
MICHELSEN AITA 22 KAMBI YA COCA-COLA
Kocha wa timu za Taifa za vijana za Tanzania, Jakob Michelsen ameita wachezaji 22 kwa ajili ya michuano ya kimataifa ya Coca-Cola itakayofanyika baadaye mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Baadaye watachujwa na kubaki 16 ambao ndiyo watakaokwenda kwenye michuano ya Afrika Kusini.

Wachezaji waliochaguliwa wametokana na michuano ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Dar es Salaam na mkoani Pwani kuanzia Juni 24- Julai 2 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni Abdulrahman Mandawanga (Dodoma), Abraham Mohamed (Mjini Magharibi), Ayoub Alfan (Dodoma), Bakari Masoud (Tanga), Daniel Justin (Dodoma), Denis Dionis (Ilala), Edward Songo (Ruvuma), Fikiri Bakari (Tanga), Hassan Kabunda (Temeke), Joseph Chidyalo (Dodoma), Mutalemwa Katunzi (Morogoro) na Mwarami Maundu (Lindi).
Wengine ni Nankoveka Mohamed (Ilala), Nelson Peter (Morogoro), Omari Saleh (Singida), Rajab Rajab (Mwanza), Said Said (Kagera), Shiza Kichuya (Morogoro), Shukuru Msuvi (Temeke), Tanganyika Suleiman (Kigoma), Tumaini Baraka (Kilimanjaro) na William John (Ruvuma).
Pia Michelsen ameongeza wachezaji saba kwenye kikosi cha Serengeti Boys ambacho Septemba mwaka huu kitacheza na Kenya kuwania tiketi ya fainali za vijana wenye umri chini ya miaka 17 za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Wachezaji walioongezwa kwenye kikosi hicho ambao pia wametoka kwenye Copa Coca-Cola ni Abdallah Baker (Mjini Magharibi), Abdallah Kheri (Mjini Magharibi), Calvin Manyika (Rukwa), Dickson Ambunda (Mwanza), Hassan Mganga (Morogoro), Miza Abdallah (Kinondoni) na Mzamiru Said (Morogoro).

JB AMGALAGAZA RAY

Msanii nyota wa filamu, Jacob Steven, maarufu kwa jina la JB

Msanii machachari wa bongo movie, Vicent Kigosi, maarufu kwa jina la Ray


Mcheza filamu nyota nchini, Jacob Steven ameibuka mshindi wa shindano la mcheza filamu bora wa kiume wa bongo lililoandaliwa na blogu ya liwazo zito.

Shindano hilo liliwashirikisha wacheza filamu wanne wa kiume wa bongo movie na washiriki walipigiwa kura na wasomaji wa blogu hii kutoka sehemu mbali mbali duniani.

Jacob, ambaye ni maarufu zaidi kwa jina la JB aliibuka mshindi baada ya kupata kura 33, ambazo ni sawa na asilimia 82 ya kura zilizopigwa.

Vicent Kigosi, maarufu kwa jina la Ray alishika nafasi ya pili baada ya kupata kura nne, ambazo ni sawa na asilimia 14,

Single Mtambalike, maarufu kwa jina la Richie alishika nafasi ya tatu baada ya kuambulia kura mbili wakati Issa Mussa, almaarufu kwa jina la Cloud aliambulia kura moja.

Msanii Awadh Mahsen, maarufu kwa jina la Dk. Cheni ndiye pekee, ambaye hakuambulia kura katika washiriki watano walioshindanishwa katika shindano hili.

Mmiliki wa blogu ya liwazo zito, Rashid Zahor amesema lengo la kuandaa shindano la aina hii ni kuwapa nafasi wasanii wa fani mbali mbali wajitambue kupitia kwa watazamaji na mashabiki wa fani wanazoshiriki.

Zahor, maarufu kwa jina la Ramoza alisema kupitia kura hizi zinazopigwa na wasomaji na watazamaji wa fani hizo, wasanii wanaweza kujitambua namna wanavyokubalika ama wasivyokubalika na mashabiki wao na nini wafanye ili waweze kupiga hatua zaidi.

Alimpongeza JB kwa kuibuka mshindi wa shindano hilo na kuwashukuru wasomaji wote wa blogu hii walioshiriki kupiga kura na wale wanaoipitia kila siku kwa ajili ya kupata taarifa mbali mbali zinazohusu michezo na burudani ndani na nje ya nchi.

AZIM DEWJI AIPONGEZA YANGA

MWANACHAMA maarufu wa klabu ya Simba, Azim Dewji ameipongeza timu yasoka
ya Yanga kwa kufanikiwa kutetea ubingwa wa michuano ya AfrikaMashariki na Kati.Yanga ilifanya hivyo mwishoni mwa wiki, baada ya kuizamisha Azam kwamabao 2-0 katika mchezo mkali wa fainali kwenye Uwanja wa Taifa, Dares Salaam.

Akizungumza jana, Dewji aliyewahi kuifadhili Simba na kuifikisha fainali za Kombe la CAF mwaka 1993, alisema pamoja na yeye kuwa `SimbaDamu’, ana kila sababu za kuimwagia sifa Yanga kwa kuwa imezika harakamatatizo yake na kugeukia kusaka maendeleo.

“Huwezi kuamini kama Yanga iliyopigwa 5-0 na kuibua tafrani nzitoJangwani, ndiyo hii ya leo. Wameikubali hali na kubadilika ndani ya muda mfupi sana. Wana amani na matunda yake yameonekana ingawa walikuwa na kipindi kifupi cha kusuka timu na kurejesha mshikamanondani ya klabu.

“Naipongeza Yanga na hasa Mwenyekiti wake, Yussuf Manji kwa sababunaamini imani ya
wanachama juu yake ndiyo iliyorekebisha hali haraka,naye kama kiongozi kuhakikisha usajili makini unafanyika, kochaanapatikana na uzalendo ndani ya Yanga unarejea,” alisema Dewji.

Aliongeza kuwa, pamoja na matunda ya haraka ya uongozi wa Manji,wana-Yanga wanapaswa kumpa ushirikiano ili kuiondoa Yanga katikautegemezi wa miaka nenda rudi, huku akisisitiza Manji hatabaki Yangamilele.

“Wana kiongozi shupavu, sasa washirikiane naye kuujenga uchumi waklabu. Haya mambo
ya kutegemea mtu kila kukicha si mazuri. Na hili sikwa Yanga tu, hata Simba na klabu nyingine
zinapaswa kujikita katikakujijenga kiuchumi ili ziwe na jeuri ya fedha bila ya kutegemea mifukoya mwanachama mmoja mmoja,” alisema.

Akisisitiza kujijenga kiuchumi, Dewji mmoja wa wafanyabiashara maarufunchini, alisema viongozi wa klabu kubwa za Simba na Yanga zianzekuutumia mtaji wa wanachama kujijenga, huku akitolea mfano kuwa, kilamoja ina zaidi ya wafuasi milioni 15, lakini klabu zinabaki kuwamasikini.

“Huu ni mtaji mkubwa sana, lakini utashangaa klabu haina hata asilimia moja (150,000) ya wanachama wa kweli. Kila siku utasikia wanachama3,000 hadi 6,000. Kiongozi wa klabu anachaguliwa na wanachamawasiofika 2,000?

“Jamani, kwa klabu inayoshabikiwa na mamilioni ya watu inashindwajekujijenga kiuchumi kwa kuwatumia mashabiki wake waliozagaa kila konaya nchi? Jiulize, kama angalau hao watu 150,000 tu wakilipa ada yamwaka ya 12,000 ambayo hata hivyo bado ni ndogo, si wanaweza kuvuna shbilioni 1.8 kwa mwaka, hizi si fedha nyingi?

“Kuna haja ya kufanya mapinduzi ya kweli, badala ya kufikiria kuifungaSimba au Yanga na kutwaa ubingwa wa Bara. Timu yenye uchumi imara,ndiyo inayokuwa na jeuri ya kuwa na kikosi imara na hivyo kufanyavizuri zaidi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Huko ndikotunakopaswa kwenda,” alisisitiza.

SIMBA YAMNASA TWITE WA APR

MAKAMU Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange Kaburu amesema wapo kwenye hatua za mwisho za kupata saini ya beki wa APR, Mbuyu Twite kuziba pengo la Kelvin Yondani aliyetimkia Yanga.
Akizungumza jana, Kaburu alisema mpango wao wa kuimarisha kikosi chao unakwenda vizuri na umepata baraka zote za kocha Milovan Circkovic.
Alisema beki huyo amekubali kucheza Simba msimu ujao."Ni mapema kutaja kiasi cha fedha tutakachotumia kukamilisha usajili wake, lakini wiki ijayo atatua nchi kwa lengo la kukamilisha usajili." alisema Kaburu.
Akithibitisha hilo kwa simu jana kutoka Kigali, Rwanda, Twite alisema kuwa anashawishika kuja kukipiga Simba baada ya viongozi wa klabu hiyo kuzungumza naye.
"Ukweli ni kwamba jana (juzi) kabla hatujarudi nyumbani Rwanda nilikutana na watu wa Simba tukazungumza ili nije kuichezea timu yao, niliwaambia nipo tayari ingawa hatukufikia muafaka wa moja kwa moja."Hata hivyo, hakuna shaka kwamba mambo yatakwenda vizuri na hatutashindwana kwa vile binafsi napenda kuja kucheza Tanzania," alisema Twite
Kuhusu dau analohitaji ili aweze kujiunga na Simba,Twite hakuwa tayari kusema. Katika hatua nyingine, Kaburu alisema kabla ya kocha Milovan kuondoka alishauri kuachwa kwa beki Lino Musomba, Haruna Shamte pamoja na Salim Kinje.
"Kocha ameonyesha kutoridhisha na viwango vya wachezaji hao hivyo ameshauri tuwaache," alisema na kuongeza:"Musomba alionekana kama hayuko tayari kucheza, naye Shamte ameshindwa kuonyesha kiwango hivyo ametushauri kuwaacha.
Kuhusu ushiriki wa Simba kwenye michuano ya Kombe la BancABC Supa 8, kiongozi huyo alisema hawatashiriki kutokana na maslahi duni.
Kaburu alisema katika mkataba uliongia kati ya TFF na wadhamini wa michuano hiyo unaonyesha shirikisho lilitapokea asilimia 50."Sisi kama wadau wakubwa wa mashindano hayo tulipaswa kushirikishwa tangu mwanzo ili tufaidike kuliko ilivyokuwa sasa."
Ukiangalia mkataba huo utaona kila timu inapewa Sh5 milioni za maandalizi, na zawadi anapewa bingwa pekee ambayo ni Sh30 milioni."Hakuna zawadi ya mshindi wa pili, watatu sasa hayo ni mashindano gani, hatutoshiriki na endapo tutaamua kucheza basi tutaitumia timu ya vijana chini ya miaka 20.

CHANZO CHA HABARI;MWANANCHI

WATEJA AIRTEL SASA KUTUMA PESA URE KUPITIA AIRTEL MONEY

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kuboresha huduma ya Airtel money kwa kurahisisha upatikanaji wa muongozo (menu) kwa kupiga *150*60# Bure pamoja na kuzindua promosheni kabambe itakayowawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kutuma pesa bure.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo M'eneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema” Airtel tunaendelea kutoa uhuru kwa wateja kupata huduma zetu kirahisi zaidi nchini kote, kuanzia sasa mteja akipiga *150*60# anapelekwa mojakwamoja kwenye horodha yake ya huduma na kuweza kuchagua anachohitaji kufanya ikiwa ni pamoja na kuongeza salio, kufanya malipo, kutoa pesa na mengine mengi.
"Tumefanya hivi hii ili kumwezesha mteja mwenye simu yeyote kupata huduma za kibenki na kuondoa changamoto zozote zitakazojitokeza, sasa mteja anauhuru wa kuchagua kutumia njia ya awali ambayo ni kwenda mojakwa moja kwenye muongozo wa simu yake na kupata horodha(Menu) ya Airtel au kupiga namba *150*60# na kuunganishwa moja kwa moja
vilevile tunayofuraha kuzindua ofa kabambe kwa wateja wetu nchini zima ambapo kutuma au kupokea pesa chini ya kiwango cha 100.000 ni BURE na mteja atakaponunua LUKU kupitia Airtel money ni BURE (hakuna viwango vya miamala vitakavyotozwa).
Tunawajulisha wateja wetu wote na wakala wetu waliosambaa nchi zima kutumia huduma hii iliyorahisi ni rahisi aliongeza” Mmbando
Airtel ni mtandao ulioenea nchini na unatoa huduma za kifedha za Airtel money yenye mawakala zaidi ya 10,000 waliosambaa maeneo mbalimbali mjini na vijijini kwa dhamira ya kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma za kifedha na kusaidia wateja wetu kuokoa muda kwenda mbali kupata huduma za kibenki.
Kupitia Airtel money mteja anaweza kupata huduma mbalimbali ikiwemo: kupokea pesa, kulipa bill kama DSTV, LUKU na DAWASCO, USA visa , kununua salio na huduma nyingine nyingi

TUHUMA ZA HUJUMA ZAMTESA SURE BOY

KIUNGO wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, amesema kwamba anasikitishwa na tuhuma zilizozagaa kwamba yeye ni miongoni mwa wachezaji waliocheza chini ya kiwango katika Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya Yanga, timu yao ikilala
2-0.

Sure Boy Jr. ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba tuhuma hizo zinamnyima raha na kwa mara ya kwanza tangu aanze kuchezea Azam, hivi sasa anajisikia mnyonge.

Sure amekana tuhuma hizo hazina ukweli wowote ndani yake na kwamba wanazungumza dhana tu, kitu ambacho ameonya si kizuri na kitaivuruga timu yao.

“Ukiutazama ule mchezo, utaona sisi tulijituma sana, siwezi kusema nani hakucheza kwa uwezo wake wote, muda mwingi tulikuwa kwenye lango lao na tulitengeneza nafasi nyingi kuliko wao. Ila tu bahati haikuwa yetu.

Kuna bao moja Yanga waliokoa mpira ukiwa unaelekea nyavuni na mimi ndiye nilitoa pasi ya mwisho, sasa unasemaje tulihujumu timu? Au kwa kuwa tumefungwa? Mimi kwa kweli sipendi haya maneno.Sisi tulitaka hilo Kombe, lakini bahati haikuwa yetu. Sisi ndio tumeumia zaidi.

Mimi nawashauri viongozi wetu, wayachukulie haya kama matokeo ya kawaida ya mchezo, tusianze kuvurugana saa hizi mapema, tuanze kujipanga kwa ajili ya mechi ya Ngao ya Jamii na Ligi Kuu,”alisema kiungo huyo bora kwa sasa Afrika Mashariki na Kati.

Jumamosi Azam ilifungwa mabao 2-0 na Yanga katika fainali ya Kagame, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kushindwa kutimiza ndoto zake za kuwa timu ya kwanza nje ya Simba na Yanga kutwaa Kombe hilo.

Lakini wengi wanaamini, Sure anakuwa miongoni mwa wanaotuhumiwa kwa sababu baba yake mzazi, Abubakar Salum ni kocha wa timu ya vijana ya Yanga ni pia mchezaji wa zamani wa klabu hiyo.

CHANZO CHA HABARI: BIN ZUBEIRY

Monday, July 30, 2012

AZAM SASA YATANGAZA KUMUUZA NGASA

Siku chache baada ya mchezaji wa kimataifa wa Tanzania ,Mrisho Ngassa kuonekana akiwa amevaa jezi ya Yanga na kuibusu logo ya klabu hiyo, waajiri wake wa klabu ya Azam kupitia ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa Facebook wamesema yafuatayo.
Azam FCKlabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa rasmi kuwa baada ya baada ya mchezaji wetu Mrisho Ngasa kuonesha wazi kuwa na mapenzi na Yanga kwa kuivaa na kuipiga busu Logo ya Yanga, tuliwapa Yanga nafasi ya upedeleo ya kumnunua lakini hadi leo hakuna ofa iliyokuja toka Yanga. simba wametoa ofa na uongozi unatafakari ofa ya SimbaYanga.... Ngasa anauzwa $50,000 wadau wa Yanga tunajua mnampenda sana Ngasa... fikisheni ujumbe kwa uongozi wenu