KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, November 12, 2017

UWANJA WA TAIFA RUKSA KUTUMIKA NOVEMBA 21


Matengenezo Uwanja Mkuu wa Taifa, Dar es Salaam, umekamilika na Mheshimiwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison George Mwakyembe, ameambiwa kuwa unaweza kuanza kutumika kuanzia Novemba 21, mwaka huu.

Kwa msingi, Waziri Dk. Mwakyembe ametoa maagizo ya kuandaliwa mchezo maalumu wikiendi ya Novemba 24, 25 au 26 kupata mchezo mmoja wa ufunguzi wa uwanja huo wenye uwezo wa kubeba takribani mashabiki walioketi 60,000 kwa wakati mmoja.

Akipokea ripoti hiyo kutoka kwa Alex – Mtaalamu kutoka Uingereza, Mheshimiwa Waziri Dk. Mwakyembe amesema: “Tuna changamoto kwenye matunzo na matengenezo. Sasa ili kukabiliana na changamoto hii, hatuna budi vijana sita waliofundishwa kazi na mtaalamu huyu, wakafanyiwa mpango wa ajira. Vijana hao wavumilie kwa sasa”

Mtaalamu huyo wa Uingereza, amesema kwamba wakati uwanja unatumika, ukarabati wa mara kwa mara utakuwa ukiendelea ili kuifanya hazina hiyo ya taifa kuendelea kuboreka  kwa wakati wote.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia akizungumzia uboreshaji huo, alisema: “Ni vema wataalamu hao wakatumike pia kwenye viwanja vya mikoani. Huko wataviboresha na kuwafundisha wengine.”

No comments:

Post a Comment