KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, November 3, 2011

WAPIGIENI KURA WANAMICHEZO HAWA

Kwa kipindi cha wiki nne sasa, blogu yenu ya liwazozito imeamua kuendesha kura ya kumteua mwanamichezo bora wa Tanzania katika miaka 50 iliyopita. Uteuzi wa mwanamichezo huyo ni sehemu ya shamrashamra za miaka 50 ya Uhuru, ambazo zinatarajiwa kufikia tamati Desemba 9 mwaka huu.

Wanamichezo wanaoshindanishwa na blogu hii kwa ajili ya kuwania tuzo hiyo ni mwanariadha nyota na bingwa wa zamani wa mbio za mita 1500 duniani, Filbert Bayi, bondia mkongwe Habibu Kinyogoli, ambaye aliwahi kushinda medali ya fedha katika michezo ya Jumuia ya Madola na wanasoka Jella Mtagwa na Peter Tino, walioiwezesha Tanzania kufuzu kucheza fainali za Afrika za mwaka 1980 zilizofanyika nchini Nigeria.

Nawaomba muendelee kuwapigia kura wanamichezo hawa ili hatimaye tuweze kumpata mshindi. Iwapo mambo yatakwenda vizuri, mshindi wa tuzo hii atapatiwa zawadi maalumu na mmiliki wa blogu hii.

Nawashukuru wale wote, ambao wameshapiga kura zao hadi sasa. Nawaomba wale, ambao hawajafanya hivyo, muda uliobaki ni mchache. Pia nawaomba wale, ambao wangependa kujitokeza kutoa tuzo kwa mwanamichezo bora wa miaka 50, wajitokeze kudhamini tuzo hii.

Mmiliki wa blogu ya liwazozito,
Rashid Zahor (Ramoza).

No comments:

Post a Comment