KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, November 9, 2011

AKI APATA JIKO, KUFUNGA NDOA NOV 26


LAGOS, Nigeria
MCHEZA filamu machachari wa Nollywood, Chinedu Ikedieze ‘Aki’ anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.
Aki anatarajia kufunga ndoa ya kimila na mchumba wake, Nneoma nyumbani kwao Mbano katika Jimbo la Imo.
Watu walio karibu na mcheza sinema huyo wamesema, ndoa hiyo inatarajiwa kufungwa Novemba 26 mwaka huu.
Kwa mujibu wa watu hao, watu mbalimbali wakiwemo familia, marafiki na ndugu wa karibu wa Aki wanatarajiwa kushuhudia ndoa hiyo.
Ndoa hiyo ya kimila, itafuatiwa na sherehe babu kubwa, zilizopangwa kufanyika Desemba 10 mwaka huu mjini Lagos.
Aki ni mmoja wa wachezaji filamu waliojipatia sifa na umaarufu mkubwa nchini Nigeria, kutokana na umbile lake na uigizaji wake.
Amekuwa akicheza filamu nyingi kwa kushirikiana na pacha wake, Osita Iheme, ambaye wanafanana kwa maumbo na vituko.
Wote wawili walianza kucheza filamu pamoja mwaka 2003 na filamu iliyowapatia umaarufu mkubwa ni Aki na Ukwa.
Aki alizaliwa Desemba 12, 1977 katika mji wa Bende uliopo kwenye Jimbo la Abia. Amewahi kushinda tuzo nyingi za mwigizaji bora wa filamu nchini Nigeria na barani Afrika.

No comments:

Post a Comment