KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, November 2, 2011

Shilole aingizwa mjini


MWANADADA anayekuja juu katika tasnia ya filamu za kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amelalamikia kitendo cha muongozaji mmoja wa filamu nchini kuipa filamu yake jina lake.
Shilole alisema mjini Dar es Salaam wiki hii kuwa, hakuna na makubaliano yoyote na mwongozaji huyo wa filamu, kuipa filamu hiyo jina lake.
Alisema makubaliano yake na wadhamini wa filamu hiyo, yalikuwa ni kushiriki kuicheza, si vinginevyo.
Mwanadada huyo alisema kitendo cha mwongozaji huyo kuipa filamu hiyo jina lake, kimewafanya waandaaji kumtuhumu kwamba ameshirikiana naye kuwatapeli.
Shilole alisema kitendo cha muongozaji huyo wa filamu ni sawa na kumuingiza mjini kwa vile ametumia jina lake kibiashara.
“Mimi niliingia mkataba wa kuigiza, sio jina langu ndilo liwe jina la filamu,”alisema mwanadada huyo.
Shilole alisema baada ya kumaliza kazi ya kuigiza filamu hiyo, alijua mkataba wake ndio umemalizika kwa vile hakukuwa na makubaliano mengine kati yao.
“Kitendo hiki kimenikera sana kwa vile ni cha kitapeli. Namshangaa sana huyu mtu kwa kutumia jina langu katika filamu hiyo bila kunishirikisha,”alisema.
Kwa mujibu wa Shilole, mtu huyo ndiye aliyepewa jukumu la kuandaa filamu hiyo na kutafuta waigizaji nyota na alilipwa pesa zote na waandaaji.
Alisema awali, filamu hiyo ilikuwa na jina lingine, lakini mtu huyo aliamua kulibadili na kuiingiza sokoni bila ridhaa ya waandaaji.

1 comment: