KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, November 9, 2011

Bimbo atuhumiwa kupanga mauaji


LAGOS, Nigeria
MCHEZA filamu Bimbo Akisanya wa Nigeria amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya jaribio la mauaji.
Bimbo alifikishwa mahakamani mwanzoni mwa wiki hii kwenye mahakama ya Ikeja, akituhumiwa kupanga mauaji ya mchungaji Pat Ogechi Dennah.
Chanzo cha habari kimeeleza kuwa, Bimbo anatuhumiwa kumwajiri muuaji kwa ajili ya kumuua mchungaji huyo wa kike Oktoba 28 mwaka huu mjini Lagos.
Hata hivyo, haikuelezwa mahakamani kuhusu sababu za Bimbo kutaka kufanya mauaji hayo.
Kwa mujibu wa habari hizo, muuaji huyo alimfyatulia risasi mchungaji Ogechi, lakini ilimpata begani.
Muuaji huyo anadaiwa kuwa alikimbia mara baada ya tukio hilo wakati Bimbo alikamatwa na polisi.
Bimbo alikanusha tuhuma hizo na aliachiwa kwa dhamana ya Naira 100,000 na wadhamini wawili. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 30 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment