Hatimaye kocha mkuu mpya wa Yanga, Tom Saintifiet kutoka Ubelgiji ametia saini mkataba wa kuinoa timu hiyo kwa miaka miwili.
Tom ametia saini mkataba huo leo mbele ya Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesiga na wajumbe wa kamati ya usajili, Ahmed Seif na Abdalla Bin Kleb.
Hafla ya utiaji saini mkataba huo imefanyika makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali.
Akizungumza mara baada ya kuingia mkataba huo, kocha huyo amesema anatarajia kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha Yanga inafanikiwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Tom alisema anatarajia kuutumia mkataba huo katika kuleta maendeleo Yanga ikiwemo kukuza vipaji katika soka la vijana.
Katibu Mkuu wa Yanga, Mwesigwa amesema mkataba huo huenda ukawa ni endelevu iwapo uongozi utaridhishwa na mwenendo wa kocha huyo.
No comments:
Post a Comment