KOCHA Mkuu mpya wa timu ya soka ya Yanga, Tom Sanffiet kutoka Ubelgiji amewasili nchini kwa ajili ya kazi ya kuinoa timu hiyo.
Tom aliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana saa 7.36 mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia akitokea Nigeria.
Kocha huyo alipokewa na Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesiga aliyekuwa amefuatana na wajumbe wa kamati ya usajili ya klabu hiyo, Abdalla Bin Kleb na Ahmed Seif ‘Magari’.
Akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo, Tom alisema amekuja nchini kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa Yanga ili kuangalia uwezekano wa kuinoa timu hiyo.
Tom alisema alitarajia kufanya mazungumzo hayo na viongozi wa Yanga jana jioni ama leo asubuhi kabla ya kutia saini mkataba wa kuinoa timu hiyo.
Alisema anaifahamu vyema Yanga kama mojawapo ya timu kubwa na kongwe nchini na pia anawafahamu vizuri wapinzani wao wa jadi, Simba.
Mbelgiji huyo alisema anaamini Yanga inaundwa na kikosi kizuri cha wachezaji na kuahidi kufanyakazi bega kwa bega na benchi la ufundi ili waweze kuwa na kikosi imara.
Kocha huyo alisema japokuwa zimesalia siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Kagame, anaamini timu hiyo itaweza kufanya vyema.
“Lengo langu ni kuiwezesha Yanga kutwaa mataji mbalimbali ya hapa nchini na kimataifa,”alisema kocha huyo.
Alipoulizwa kuhusu hatma ya mkataba wake wa kuinoa timu ya taifa ya Nigeria, Tom alisema ulivunjika baada ya kutokea hali ya kutokuelewana kati yake na viongozi wa Chama cha Soka cha Nigeria (NFF).
Mapokezi ya Tom pia yalihudhuriwa na wanachama kadhaa wa Yanga waliofika kwenye uwanja huo kwa mabasi ya kukodi.
Wakati kocha huyo akitoka nje ya uwanja, wanachama hao walisikika wakiimba ‘Nani kaua, Manji. Nani kaua, Manji’ wakiwa na maana kuwa, ujio wake umefanikishwa kwa kiasi kikubwa na mfadhili wa klabu hiyo na mgombea wa nafasi ya mwenyekiti katika uchaguzi mdogo, Yussuf Manji.
Kocha huyo aliondoka uwanjani hapo kwa gari aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili T 316 BEV, linalomilikiwa na Seif. Msafara wa kocha huyo ulihusisha magari takriban sita.
Msafara wa kocha huyo ulikwenda moja kwa moja makao makuu ya klabu hiyo, mitaa ya Twiga na Jangwani, ambako alitia saini kitabu cha mapokezi.
Baada ya kutia saini kitabu hicho, kocha huyo alisalimiana na wanachama mbalimbali wa Yanga wakiwemo wazee wa klabu hiyo.
Kocha huyo amewahi kufundisha soka katika nchi za Ubelgiji, Qatar, Ujerumani, Visiwa vya Faroe, Finland, Uholanzi, Namibia na Zimbabwe akiwa kocha mkuu.

No comments:
Post a Comment