KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, July 12, 2012

Diamond, Mwasiti wakumbuka Kigoma

BAADHI ya wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya kutoka mkoani Kigoma, wameamua kuungana na kutunga wimbo wenye vionjo vya moja ya makabila ya mkoa huo.
Wimbo huo unajulikana kwa jina la Leka Dutigite, ukiwa na maana ya Acha kujidai na umerekodiwa kwenye studio za Tuddi Thomas zilizopo mjini Dar es Salaam.
Wasanii walioshiriki kuimba wimbo huo ni pamoja na Naseeb Abdul ‘Diamond’, Mwasiti, Ommy Dimpoz, Baba Levo, Recho, Peter Msechu, Banana Zorro na Linex.
Akizungumzia wimbo huo mjini Dar es Salaam wiki hii, Diamond alisema umelenga kuuenzi utamaduni wa watu wa Kigoma, hasa kabila zao za asili.
Diamond alisema tayari wimbo huo umeshaanza kusikika katika vituo mbalimbali vya redio nchini na tayari kazi ya kutengeneza video yake imeshaanza.
Katika wimbo huo, wasanii hao nyota wameimba kwa kupokezana na kuufanya uwe na mvuto wa aina yake kuusikiliza.
Kwa mujibu wa Diamond, huo ni mwanzo na wataendelea kufanya hivyo mara kwa mara kwa lengo la kuuenzi mkoa wao.

No comments:

Post a Comment