Mshambuliaji Salum Ramadhani ndiye aliyefunga bao hilo la pekee dakika ya 36 baada ya kuunganisha wavuni pasi kutoka kwa Mtalemwa Katunzi.
Temeke ilifanikiwa kumaliza michuano hiyo ikiwa ya tatu baada ya kuichapa Tanga mabao 2-0.
Mabao yote ya Temeke yalifungwa na Rehani Kibingu dakika ya 48 na 86.
Kufuatia ushindi huo, Morogoro imezawadiwa sh. milioni nane wakati Mwanza imepata sh. milioni 4.4 na Temeke sh. milioni 3.2.
Tuzo ya kocha bora ilikwenda kwa kocha wa Tanga, Mohamed Kampira, tuzo ya mwamuzi bora imenyakuliwa na Liston Hiyari, kipa bora ni Shukuru Mohamed wa Temeke, mfungaji bora Mtelamwa Katunzi wa Morogoro na mchezaji bora ni Shiza Kichuya. Kila mmoja alipata sh 750,000. Tanga pia ilipata tuzo ya timu yenye nidhamu na kuzawadiwa sh. milioni moja.
No comments:
Post a Comment