MSOMI wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Viginia Mokiri jana usiku aliibuka kuwa Miss Vyuo Vya Elimu ya Juu katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Club Maisha, Dar es Salaam. Katika shindano hilo, ambalo majaji wake walikuwa ni Kamati ya Miss Tanzania, Fatuma Ramadhani wa Chuo cha Uandishi wa Habari Arusha (ASJ), alishika nafasi ya pili na Fina Recatus wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) alikuwa wa tatu. Pichani ni Viginia katikati, kushoto mshindi wake wa pili, Fatuma na kulia mshindi wa tatu, Fina.
No comments:
Post a Comment