KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, July 6, 2012

Wasanii Bongo Movie wamtembelea Mama Maria Nyerere

Mama Maria Nyerere akisalimiana na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Jacob Steven 'JB' wakati wasanii wa kundi hilo walipomtembelea nyumbani kwake Butiama, Musoma mkoani Mara



Mwigizaji wa filamu nchini kutoka Kundi la Bongo Movie,Steven Mangele "Stive Nyerere" jana alikabidhi filamu yake aliyoiigiza kama Mwalimu Nyerere kwa Mama Maria Nyerere ikiwa ni kama shukrani zake, baada ya mama huyo kumsaidia katika kukamilisha filamu hiyo ambayo aliifanyia Butiama.
Stive alisema kwamba kumpa filamu hiyo Mama Maria Nyerere ni kuweka kumbukumbu kwamba anathamini msaada na mchango wake katika filamu hiyo na hana kikubwa cha kumpa wala cha kumfanyia zaidi.
Amesema Mama Maria Nyerere alimsaidia sana katika kumuonyesha vitu gani mwalimu alikuwa akifanya na vitu gani mwalimu alikuwa akivipenda na sehemu ambazo mwalimu alipenda kukaa baada ya kazi zake.
Pia ametoa shukrani kwa wasanii wenzake ambapo waliojitahidi katika hali moja au nyingine kuhakikisha filamu hiyo inakamilika.

No comments:

Post a Comment