KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, July 5, 2012

OKWI AKANA KUJIUNGA NA YANGA

WAKATI Mshambuliaji Emmanuel Okwi amekanusha kusaini Yanga, uongozi wa klabu yake, Simba umesikitishwa na habari zilizovumishwa kwenye vyombo vya habari kuhusu mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda kujiunga na wapinzani wao wa jadi, Yanga.
Akizungumza na waandishi wa habari mchana wa leo, makamo makuu ya klabu mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, alisema kwamba habari hizo hazina ukweli wowote, ni kinyume cha maadili ya taaluma ya uandishi wa habari na zina lengo la kupotosha ukweli na kuwanyima raha wale wote wenye mapenzi mema na Simba.
“Gazeti kama la Spoti Starehe limekwenda mbali zaidi kwa hatua yake ya kutaka kuufitinisha uongozi na wapenzi na wanachama wake kwa kudai kuwa uongozi unafikiria tu kumuuza Okwi bila ya kuangalia mkataba wake.
"Kwa mujibu wa gazeti hilo, mkataba wa Okwi umemalizika leo na ndiyo maana ameamua kusaini Yanga akiwa mchezaji huru,”alisema Kaburu na kuongeza;.“Ukweli ulivyo. Emmanuel Okwi alisaini mkataba mpya wa kuichezea Simba mnamo mwaka jana na mkataba huo unamfanya kuwa mchezaji halali wa klabu yetu hadi mwaka 2013. Baada ya mkutano huu, nitawaonyesha waandishi nakala ya mkataba wa Okwi na Simba. Hivyo taarifa kwamba mchezaji huyo hana mkataba na Simba ni za uongo, uongo mtupu,”alisema.
“Hivi ninavyozungumza nanyi, Okwi yuko kwao nchini Uganda akishughulikia viza ya kwenda nchini Italia ambako anatarajiwa kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika moja ya vilabu vya Ligi Kuu ya Italia (Serie A),”alisema Kaburu.
Kwa hisani ya http://bongostaz.blogspot.com/)
Wakati huo huo, blogu ya shaffihdauda imeripoti kuwa, Okwi amekana katakata kujiunga na Yanga na kusisitiza kuwa, yeye bado mchezaji halali wa Simba.
Akiongea moja kwa moja na Shaffih kwa njia ya simu kutoka Uganda, Okwi alisema:
"Shaffih hizo taarifa zinazoenea huko Tanzania kwamba nimesaini kuichezea Yanga sio za kweli kabisa. Ni uongo asilimia 100. Mimi bado mwajiriwa mtiifu wa klabu bingwa ya Tanzania Simba. Naipenda na kuiheshimu timu yangu na nitaendelea kuiheshimu saini yangu iliyopo kwenye mkataba ambao bad ninao na Simba. Sasa nimepewa ruhusa ya kwenda nchini Italia kwenda kufanya taratibu za kujiunga na Parma lakini kama mambo yakiwa ndivyo sivyo then mtaawa Msimbazi ndio nyumbani kwangu. Natarajia kwenda Italia ndani wiki hii kwa sababu sasa hivi ninasubiria viza inayotoka ndani ya siku mbili zijazo," - alimaliza Okwi.
kwa hisani ya www.shaffihdauda.com.

No comments:

Post a Comment