'
Wednesday, July 13, 2016
PAMBANO LA TWIGA STARS VS RWANDA LAAHIRISHWA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA), limeahirisha mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu ya taifa ya wanawake ya Rwanda dhidi ya wageni, Tanzania ‘Twiga Stars’ uliokuwa ufanyike Jumapili Julai 17, 2016.
Mchezo huo uliandaliwa na FERWAFA na Rais Paul Kagame alipendekeza mchezo huo kuwa sehemu ya burudani kwa wakuu mbalimbali wa nchi za Afrika wanaotarajiwa kuwa na mkutano wa viongozi hao kuanzia kesho Julai 14, 2016.
Kwa mujibu wa barua ya Rais wa FERWAFA, Nzamwita Vincent ya Julai 12, 2016 kwenda Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), sababu za kuahirisha mchezo huo ni ratiba ya mkutano huo wa 27 wa wakuu nchi.
“Tunasikitika kuwataarifu kuwa ile ratiba ya kuwa na mchezo wa kirafiki kati ya Rwanda na Tanzania, imefutwa. Tunaomba radhi kwa taarifa hii ya ghafla ambayo iko nje ya uwezo wetu inayowafikia huku tukijua kwamba mlikuwa tayari mmeandaa timu kwa ajili ya mchezo,” ilisema sehemu ya barua hiyo.
“Hata hivyo tunaahidi kuendelea kufanya mawasiliano ili kupanga tarehe nyingine ya kufanyika mchezo huo,” ilisisitiza barua.
Taarifa hiyo imekuja wakati tayari Twiga Stars ilikuwa imeanza maandalizi ya kutosha kwa mchezo huo ambao ulianza kuvutia mamia ya mashabiki wa mpira wa miguu wan chi za Afrika Mashariki.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA), limeahirisha mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu za wanawake za Tanzania ‘Twiga Stars’ na wenyeji Rwanda uliokuwa ufanyike Jumapili Julai 17, 2016.
Mchezo huo uliandaliwa na FERWAFA na Rais Paul Kagame alipendekeza mchezo huo kuwa sehemu ya burudani kwa wakuu mbalimbali wa nchi za Afrika wanaotarajiwa kuwa na mkutano wa viongozi hao kuanzia kesho Julai 14, 2016.
Kwa mujibu wa barua ya Rais wa FERWAFA, Nzamwita Vincent ya Julai 12, 2016 kwenda kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), sababu za kuahirisha mchezo huo ni kuingiliana kwa ratiba ya mkutano huo wa 27 wa wakuu nchi za Afrika.
“Tunasikitika kuwataarifu kuwa ile ratiba ya kuwa na mchezo wa kirafiki kati ya Rwanda na Tanzania, imefutwa. Tunaomba radhi kwa taarifa hii ya ghafla ambayo iko nje ya uwezo wetu inayowafikia huku tukijua kwamba mlikuwa tayari mmeandaa timu kwa ajili ya mchezo,” ilisema sehemu ya barua hiyo.
“Hata hivyo tunaahidi kuendelea kufanya mawasiliano ili kupanga tarehe nyingine ya kufanyika mchezo huo,” ilisisitiza barua iliyosainiwa na Nzamwita Vincent.
Taarifa hiyo imekuja wakati tayari Twiga Stars ilikuwa imeanza maandalizi ya kutosha kwa mchezo huo ulioanza kuvutia mamia ya mashabiki wa mpira wa miguu wa ncza Afrika Mashariki na kati.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment