KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager leo
imekabidhi vifaa vya michezo katika mikoa mitano inayoshiriki mashindano ya
Safari Pool Taifa ambayo yanatarajiwa kuanza leo katika mikoa hiyo.
Vifaa hivyo ni t-shirt pamoja pesa za nauli kwa kila timu na pesa za zawadi
kwa timu zitakazoshinda katika fainali za mikoa hiyo ambazo wamekabidhiwa
manahodha wa kila klabu shiriki.
Mikoa iliyokabidhiwa vifaa na pesa hizo ni Shinyanga,Kilimanjaro,Manyara,Tabora na Kagera.
Makabidhiano hayo yalifanywa na wageni rasmi mbalimbali kila mkoa ambapo
Tabora alikuwa Ofisa utamaduni wa wilaya, Mark Katunzi, Shinyanga alikuwa
Ofisa Utamaduni wa Wilaya, Asha Mbwana, Kagera alikuwa, Ibrahim Mabruk,
Manyara alikuwa, Ofisa Elimu ya Watu Wazima, Fausta Akoro na Kilimanjaro
alikuwa Jafari Michael ambao kwa ujumla waliwataka wachezaji wa Pool
kuuheshimu mchezo na kuwa na nidhamu katika kipindi chote cha
mashindano na watambue kuwa kwenye mashindano lazima apatikane
mshindi wa kwenda kushiriki Taifa kuuwakilisha Mkoa.
Aidha waliishukuru Kampuni ya Bia Tanzania kwa kufadhili mashindano hayo
kwani yanawafanya vijana faidike na kiasi cha fedha wanachoshindania licha
ya burudani waipatayo ambayo inawaepusha na mambo mengi yasiyo na faida
mtaani
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kesho na kumalizika Julai 8 mwaka huu
ambapo timu itakayoibuka bingwa kwa upande wa Mkoa itajinyakulia kitita cha
sh. 700,000 huku mchezaji mmoja mmoja akiondoka na sh. 350,000 kwa
upande wa wanaume na wanawake wa kwanza atazawadiwa sh. 250,000
taslimu.
mshindi wa pili kwa upande wa timu, atazawadiwa sh. 350,000, mshindi wa
tatu, 200,000, wa nne sh. 100,000 na kifuta machozi cha sh. 50,000
kitatolewa kwa timu zitakazoshiriki.
Halikadhalika kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja kwa upande wa
wanaume mshindi wa pili atapata sh. 200,000, wa tatu sh. 150,000 na wa nne
sh. 100,000 ambapo wanaume kwa wanawake wanne kati ya wanane
watakaopoteza mchezo katika awamu ya pili watazawadiwa sh. 50,000, na
wakataopoteza katika awamu ya kwanza wanane kati ya 16 wataambulia sh.
20,000.
Aidha kwa upande wa wanawake kwa mchezaji mmoja mmoja mshindi wa pili
atazawadiwa sh. 150,000, wa tatu sh. 100,000 na wa nne ataambulia sh.
50,000.
No comments:
Post a Comment