Bondia Francis Cheka (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu pambano kati yake na Japhet Kaseba litakalofanyika kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
WACHEZA filamu nyota wa kike nchini, Wema Sepetu na Jacqueline Wolper wametambiana kila mmoja akijigamba kumdunda mwenzake kesho.
Wema na Wolper walitoa majigambo hayo jana walipozungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa hoteli ya Atriums iliyopo Sinza, Dar es Salaam.
Pambano kati ya wanadada hao ni sehemu ya burudani itakayokuwepo wakati wa tamasha la matumaini linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Tamasha hilo limeandaliwa na Kampuni ya Global Publishers na Mamlaka ya Elimu Tanzania.
"Sipendi maneno, napenda vitendo. Nimekuwa nikisikia Wema na rafiki yake wanaongea sana kwenye televisheni. Nataka nikate mdomo wake kwa kumpiga siku hiyo,"alisema Wolper.
Akizungumza kwa niaba ya Wema, kocha wake, Rashid Matumla alisema amejiandaa vyema kushinda pambano hilo kwa kumtwanga Wolper. Akinadada hao watazipiga kwa raundi sita.
Nao mabondia Francis Cheka na Japhet Kaseba kila mmoja alijigamba kuwa, atamdunda mwenzake katika pambano lao linalotarajiwa kuwa la raundi 12.
Cheka alisema hana wasiwasi na Kaseba kwa vile ameshawahi kumdunda mara kadhaa na kusisitiza kuwa, kila mara amekuwa akitafuta visingizio ili kuficha udhaifu wake.
Naye Kaseba aliendelea kusisitiza kuwa, Cheka amekuwa akibebwa kila wanapopambana na kwamba safari hii ameazimia kukata ngebe zake.
(PICHA/HABARI : ERICK EVARIST/GPL)
No comments:
Post a Comment